SIMBA SC WAICHAPA MTIBWA SUGAR BAO 1-0 TAIFA,OKWI AWAPA RAHA
BAO la
Emmanuel Anord Okwi dakika ya 90 ushei limeipa Simba SC ushindi wa 1-0
dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii katika
mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba SC
sasa inafikisha pointi 29 baada ya mechi 18 na kuendelea kukamata nafasi
ya tatu, nyuma ya mabingwa watetezi, Azam FC pointi 30 za mechi 16 sawa
na vinara Yanga SC, wenye pointi 31.
Okwi
alifunga bao hilo, wakati tayari baadhi ya wapenzi wa Simba SC wameanza
kutoka uwanjani, wakiamni matokeo ni sare. Mganda huyo, alifunga baada
ya kupata pasi ya Abdi Banda na kumchambua vizuri kipa aliyefanya kazi
nzuri leo, Said Mohamed Kasarama.
Emmenuel Okwi akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Said Mkopi katika mchezo wa leo
|
Beki wa Simba SC, Hassan Kessy akimtoka kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaaban Nditi
|
Mchezo
huo uliochezeshwa na refa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, aliyesaidiwa na
Yussuf Sekile wa Ruvuma na Abdallah Rashid wa Pwani, Simba SC ndiyo
waliotawala na kutengeneza nafasi nyingi, lakini hawakuwa na bahati ya
mapema.
Mshambuliaji
wa zamani wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi aliiongoza vyema safu ya
ushambuliaji ya Mtibwa Sugar akisaidiana na Ame Ally, lakini wakaishia
kuisumbua tu ngombe ya Simba, iliyoongozwa na beki chipukizi, Hassan
Isihaka.
Kikosi
cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Hassan Kessy, Mohammed Hussein
‘Tshabalala’, Juuko Murushid, Hassan Isihaka, Jonas Mkude, Said Ndemla,
Abdi Banda, Elias Maguri, Emmanuel Okwi na Simon Sserunkuma/Ramadhani
Singano ‘Messi’ dk46.
Mtibwa
Sugar; Said Mohammed, Said Mkopi, Dacis Luhende, Salim Mbonde, Andrew
Chikupe, Shaaban Nditi, Ally Sharrif, Henry Joseph, Ame Ally/Mohammed
Mkopi dk66, Muzamil Selemba/Ally Yussuf dk86 na Mussa Hassan
Mgosi/Vincent Barnabas dk75.
Comments
Post a Comment