ANGALIA JINSI ZITTO ALIVYOITEKA KIGOMA,MAPOKEZI YAKE YASHTUA WENGI
Mh zitto kabwe baada ya chama chake cha CHADEMA kutangaza kumfukuza
uanachama ndani ya chama hicho ameamua kufanya ziara ya siku tatu ndani
ya kigoma kuzumgumza na wananchi wake juu ya hali ya kisiasa
inayomkabili kwa sasa,hizi hapa ni baadhi picha za mapokezi yake
kigoma
Ikiwa
bado sakata la kufukuzwa uanachama kwa mbunge wa kigoma kaskazini
(CHADEMA) mh ZITTO KABWE linaendelea kuchukua nafasi katika vichwa vya
watanzania na wapenda siasa,mbunge huyo ameanza kufanya ziara ya siku
tatu jimboni kwake kuzungumza na watanzania mbalimbali.
Akiwa
katika ziara yake MBUNGE wa Kigoma Kaskazini,Zitto
Kabwe(Chadema),amewataka wakazi wa mkoa wa kigoma wasisikitishwe na
mambo yanayomkabili kwa sasa kwa kile alichoeleza kuwa asilimia kubwa ya
wanasiasa makini walishapitia misuko suko kama yake.
Amewaeleza
kuwa jambo la msingi ni kumuunga mkono katika hatua yoyote
atakayochukua kwa ajili ya wanakigoma na Taifa kwa ujumla katika
kumaliza mgogoro uliopo baina ya Chama chake na yeyeZitto ametoa kauli
hiyo leo mjini Kigoma alipokutana na viongozi 250 kwenye mkutano wa
ndani uliohusisha viongozi kutoka katika kila kijiji kwenye jimbo la
Kigoma kaskazini yenye jumla ya vijiji 45.Aliwataja baadhi ya wanasiasa
waliopita katika hatua kama yake na baadae wakageuka washindi kuwa ni
Maalim Seif Sharif Hamad(Tanzania),Mahathir Mohamed(Malaysia na Indira
Gandhi wa India.“Msinililie mimi kwa kuwa haya ni mapito ya kila
mwanasiasa Makini,wengi walio makini walitofautiana na vyama vyao kwa
sababu ya maslahi ya mataifa yao,wapo walioanzisha vyama baada ya hali
hiyo na wakashinda na wapo waliopigiwa magoti na vyama vyao baada ya
kugundua walichofanya si sahihi, hivyo jukumu kubwa ni kuniunga
Mkono”alisema Zitto.
Alisema
mpaka sasa hajapewa taarifa yoyote ya kusitishwa kwa Ubunge wake na kama
hali hiyo ikijitokeza atarudi kuwafahamisha juu ya hatua atakayochukua
Zitto
yupo mjini Kigoma kwa ziara ya siku tatu,ambapo atawatembelea wakulima
wa mradi wa Kahawa walio katika mfuko wa hifadhi ya Jamii(NSSF), pamoja
na kukabidhi gari aina ya Ambulance katika kituo cha Afya Nyarubanda na
kisha kufanya mikutano miwili ya hadhara.
Juzi
Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu,alitangaza hadharani kuvuliwa
uanachama kwa Zitto kutokana na kushindwa katika kesi aliyofungua
kupinga asijadiliwe na Chama Chake
Comments
Post a Comment