Picha na habari kamili kuhusu vifo vya watu 10 vilivyosababishwa na na ajali ya basi la Allys na Bunda mkoani Mwanza
Ajali hizo zilitokea ijumaa usiku katika barabara kuu ya Mwanza-Shinyanga katika maeneo ya Mitindo wilayani Misungwi na eneo la Buhongwa Dampo wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza. Ajali mbaya zaidi iliyosisimua na kusababisha vilio kuugubika mji wa Usagara wilayani Misungwi, ilitokea majira ya saa 1:40 Buhongwa, ambapo Basi la Allys lenye namba za usajiri T.691 AGP liligonga Daladala (Toyota Hiace) na kusabaisha vifo vya watu tisa ambao kati yao, saba walikufa palepale. Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Valentine Mulowola akithibitisha ajali hiyo, alisema basi hilo lililokuwa na hitilafu ya taa za mbele, lilikuwa likitoka Arusha kwenda jijini Mwanza wakati daladala hiyo ikitoka Buhongwa kwenda Usagara wilayani Misungwi. Baadhi ya abiria waliokuwa katika ajali hiyo akiwemo Shija Francisco ambaye alijeruhiwa mkono wa kulia alisema kuwa ,basi hilo liliwagonga sehemu ya ubavu wa kulia ...