NISHA NAYE PIA APATWA NA GONJWA LA AJABU


Maskini! Staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ anateseka baada ya kupata gonjwa la ajabu linalomsababishia maumivu makali.


Hali ya Nisha ilivyo kwa sasa. Hapa akilazimishwa kula chakula.
Akizungumza rafiki yake ambaye pia ni msanii mwenzake, Happy John ‘Nyatawe’ alisema Nisha alianza kulalamika kwamba anasikia vitu vikimtembea mwilini na maumivu makali ya kichwa kinachomuuma mfululizo.
“Alianza kulalamika kuumwa kama mchezo lakini siku zinavyozidi kusonga ndivyo hali yake inavyozidi kuwa mbaya, hata hatuelewi ni nini,” alisema Nyatawe.

Paparazi wetu alifanikiwa kuzungumza na Nisha akiwa nyumbani kwake huku akilishwa chakula kama mtoto ambapo alisema anasikia maumivu makali ya kichwa na tayari ameshaenda hospitali akapewa dawa lakini ugonjwa unaomsumbua haukujulikana.
Nisha akilishwa chakula.
“Kichwa kinaniuma sana na vitu vinanitembea mwilini sijielewi kabisa, muda mwingine ninakandwa na maji ya baridi kutokana na maumivu makali, nimeenda hospitali nimepima kila kitu lakini ugonjwa hauonekani,” alisema Nisha akitokwa machozi kutokana na maumivu aliyokuwa akiyasikia.
Wakati paparazi wetu akiendelea na mazungumzo hayo alimshuhudia Nisha akiweweseka kama mtu aliyechanganyikiwa.
KUNA MKONO WA MTU?
Baadhi ya wasanii ambao hawakutaka kutajwa walisema kutokana na hali aliyonayo Nisha inawezekana kuna mkono wa mtu kwani wasanii wamezidi kwa kulogana hivyo anatakiwa kuombewa kwa Mola kwani hali ya afya yake si shwari.


                GPL

Comments

Popular posts from this blog