KAULI YA MANJI BAADA YA KIPIGO CHA JANA TOKA KWA SIMBA CHA BAO 3-1
Mwenyekiti
wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji ameaomba wanachama, wapenzi
na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki
dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa wa
Twiga/Jangwani
Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia sana hakuna
aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe
tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.
"Mechi
ya jana ilikuwa ni bonanza, ndio maana hapakuwa na timu iliyopata
pointi katika mchezo huo zaidi ya kusherehekea, sisi tumepata zawadi ya
milion 98 wakati wenzetu Simba SC wamepata milion 1, hivyo zaidi sisi
tumeendelea kuimarika kiuchumi zaidi wenzetu wameishia kusherehekea"
alisema Manji.
Aidha
amesema wachezaji zaidi ya tisa wa Yanga hawajapata muda wa kupumzika
tangu mwezi Novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi
Kuu kwani walijiungana timu za Taifa na wamekua huko kwa takribani mwezi
mzima bila kupumzika tofauti na wenzetu Simba SC ambao hawana wachezaji
wengi timu ya Taifa.
Manji
pia alisema anaapa hongera kwa kushinda bonanza la jana, anasema mchezo
wa jana walicheza vizuri hivyo wanastahili pongezi kwa hilo.
Akijibu
maswali ya waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyojitokez katika
mchezo wa jana, amesema kamati husika inayafanyia kazi na kwa kuwa yeye
anasafiri leo kwenda nje ya nchi majukumu yote amemkabidhi makamu
mwenyekiti Clement Sanga mpaka yeye atakaporejea
Comments
Post a Comment