WIVU WA MAPENZI WASABABISHA ANG'ATWE SIKIO NA KUNYOFOLEWA KABISAAAA

Hivi karibuni hapa jiji mwanza mkazi mmoja wa Igoma Aliefahamika kwa jina moja la Consolata amepigwa na mmewe na kung’atwa sikio na mtu anaedaiwa kuwa ni hawara wa mumewe bi consolata amesema alikuwa akigombana na mumewe ndipo hawara yake huyu alipokuja na kusema ngoja tukuonyeshe maana hutujui ndipo alipong’atwa sikio na kuondolewa sikio zima

Mara baada ya kufanyiwa ukatili huo alienda kulipoti katika kituo cha polisi lakini kwa madai yake ni kwamba watuhumiwa waliachiwa huru kwa kuwa walikuwa wakijuana na baadhi ya askari waliokuwepo kituoni .Ndipo bi consolata alipochukua hatua za kutafuta wasamalia wema kama waandishi ili waweze kumsaidia aweze kupatiwa matibabu kwani ni mgeni jiji mwanza toka kigoma na alikuja mwanza kwa ajili ya kumsalimu mumewe.

Baada ya kuzungumza na waandishi alipelekwa kwenye taasisi ya kivulini ambao mpaka sasa wanampatia huduma ya matibabu ukatili huu kiukweli ni aibu kubwa kwa taifa letu









Comments

Popular posts from this blog