Posts

RAIS KIKWETE KUHUTUBIA BUNGE LEO

Image
Rais Jakaya Kikwete, leoo anatarajiwa kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Habari zilizopatikana Mjini Dodoma jana na kuthibitishwa na uongozi wa Bunge pamoja na Ikulu, Dar es Salaam zinasema atahutubia mchana. Kutokana na ujio huo, Serikali imewaelekeza Mawaziri na Manaibu Waziri kutotoka nje ya Dodoma hadi hapo Rais atakapokuwa amehutubia Bunge. Kadhalika safari zote za Kamati za Bunge ambazo zilikuwa katika mchakato wa kutekelezwa zimeahirishwa hadi baada ya leo, ili kutoa fursa kwa wabunge wote kuwapo wakati wa hotuba hiyo. Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema jana kuwa hata yeye amesikia taarifa kuwa Rais atazungumza bungeni lakini hajui atazungumza kitu gani... "Hata mimi nimesikia kuwa atazungumza lakini sijui atazungumza jambo gani kwa kuwa siyo miongoni mwa watu wanaomwandalia hotuba," alisema Balozi Sefue. Kadhalika, Mkurugenzi w

Watu 35 wakamatwa baada ya kutuhumiwa kuhusika na mauaji ya waandishi wa habari wawili ya RFI mjini Kidal kakazini mwa Mali

Image
Na Ali Bilali Operesheni maalumu ya jeshi la Mali na vikosi vya Ufaransa nchini Mali, imefanikisha kukamatwa kwa watu zaidi ya 35 wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya waandishi wawili wa habari rais wa Ufaransa, Ghislaine Dupont na Claude Verlon waliouawa mwishni mwa juma mjini Kidal.  Kukamatwa kwa watu hawa kunakuja saa chache baada ya kuwasili kwa miili ya waandishi wa habari jijini Paris tayari kwa taratibu nyingine za mazishi. Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita wakati akitoa heshima zake za mwisho kabla ya kusafirishwa kwa miili ya waandishi hao, alielezamaskitiko yake na kulaani kundi lililohusika kwenye mauaji yao. Kwa upande wake mkurugenzi anayehusika na masuala ya Afrika kwenye idhaa ya RFI, Yves Rocles amesema kuwa RFI imepoteza watu muhimu kwenye tasnia ya habari lakini amefarijika kwakuwa msiba huu haukuwa wa nchi ya Ufaransa pekee bali kwa dunia. Katika hatuwa nyingine, serikali ya Ufaransa imesema kuwa imepel

AUWAWA KWA KUCHOMWA MOTO KWA WIZI WA PIKIPIKI MBALIZI MBEYA

Image
Wananchi wakishuhudia  mwili wa mtu aliyetuhumiwa kuiba pikipiki ukiteketea kwa moto Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtakuja Mbalizi Mbeya vijijini, Ambonisye Masinga mwenye koti wakiwa eneo la tukio Polisi wakiondoka na mwili wa marehemu MTU mmoja asiyefahamika jina wala makazi yake, amepoteza maisha baada ya kupigwa na kuchomwa moto na wananchi ambao wameamua kujichukulia sheria mkononi. Wananchi hao ambao ni wakazi wa eneo la Mtakuja Mbalizi, walifanya tukio hilo jana majira ya saa mbili asubuhi. Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtakuja Mbalizi Mbeya vijijini, Ambonisye Masinga, alisema kuwa  marehemu huyo alidaiwa kuiba pikipiki  eneo la Utengule. Alisema, baadhi ya madereva wa bodaboda(pikipiki) walianzisha msako na kufanikiwa kumtia nguvuni marehemu huyo na kuanza kumshushia kipigo huku mwili wake ukiwa umefungwa kwenye pikipiki na kuuburuza barabarani umbali wa kilomita moja. Alisema, mwili huo uliburuzwa na kufikish

MKUTANO WA KIMATAIFA WA ADHABU MBADALA YA KIFUNGO GEREZANI WAFUNGULIWA DAR ES SALAAM

Image
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi, akiisoma hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ambaye alimuakilisha katika mkutano wa siku tatu wa masuala wa adhabu mbadala wa kifungo gerezani unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Holiday Inn, jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo uliojumusiha nchi ya Ethiopia, Kenya, Malawi, Rwanda, Afrika Kusini, Sudani ya Kusini, Uganda, Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania. Kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu nchini, Shabani Lila na Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Jamii, Fidelis Mboya. Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Huduma kwa Jamii, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na Maboresho ya Sheria za Adhabu la Penal Reform International. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Wacheza ngoma wa

Mbunge wa CHADEMA afutiwa dhamana na kutupwa selo kwa siku 14

Image
  DHAMANA ya  mbunge wa  jimbo la Ukerewe, Salvatory Machemli (CHADEMA) imefutwa na ameamuriwa na mahakama kwenda rumande  siku 14 kwa kuwa wadhamini wake wamekosa sifa baada ya mshitakiwa na wadhamini wake watatu kushindwa kufika mahakamani ili kuwezesha kesi ya  uchochezi  inayomkabili kusikilizwa kama ilivyopangwa.   Pia, Mbunge huyo ametakiwa  kuwasilisha  vitambulisho vyake katika kituo cha polisi na amezuiliwa kutoka nje ya wilaya  bila  kibali cha mahakama.    Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya hiyo Faustine Kishenyi alitoa uamuzi huo jana baada ya upande wa mashitaka kuomba mshitakiwa afutiwe dhamana.  Wadhamini ambao ni Shellifu Ngelezya, Max Mhogo na Konsolata Machemli wamepoteza sifa hivyo udhamini wao umefutwa. Mwendesha mashitaka wa jeshi la  polisi, Inspekta   Samweli Onyango  amesema mshitakiwa kwa makusudi  ameshindwa kufika mahakani  zaidi ya mara tano bila kutoa taarifa wakati  kesi yake  ikitajwa. Mwishoni mwa mwezi  uliopita, h

WADAU WA MFUKO WA BIMA YA AFYA MKOA WA NJOMBE WATAKA KUWEPO KWA UTARATIBU WA KUUNGANISHWA KTK MFUKO HUO

Image
Kaimu Mkurugenzi mkuu  wa NHIF Hamisi Mdee akitoa taarifa ya Utekelezaji ya kuanzia 2001 hadi June 2013, Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Balozi Ali  Mchumo akitoa salamu za NHIF kwa washiriki wa mkutano Meneja uendeshaji wa NHIF, Salome Manyama akiwasilisha mada katika mkutano huo, picha ya tano wadau wa mkoa a Njombe wakifuatilia mada.. Na FrancisGodwin Blog Njembe Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Njombe, wameushauri kuwepo kwa utaratibu wa kuunganisha huduma za Mfuko huo na ule wa Afya ya Jamii (CHF) ili kuondoa dhana ya ubaguzi katika ugawaji wa dawa kwenye vituo vya matibabu. Ushauri huo umetolewa mjini Njombe katika mkutano wa wadau wa NHIF wa mkoani humo. Kukosekana kwa dawa kwa wanachama wa CHF wakati wale wa NHIF wanapata dawa hizo kumeonekana Kuwa Kero kwa Wananchi Wengi Mkoani Njombe Katika Mpango wa Kujiunga na Mifuko Hiyo Hali Inayopelekea Wanachi Wengi kusita Kujiunga na Mifuko Hiyo. Akizungumza Wakati wa Kufu

MFANYAKAZI WA TBC AUAWA KWA KUPIGWA RISASI MAENEO YA UBUNGO MAZIWA JIJINI DAR

Image
Mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji Nchini  TBC, pichani,RAMADHAN GIZE ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosaidiwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo katika eneo la UBUNGO Maziwa Jijini DSM. Tukio hilo limetokea baada ya watu hao kuvamia duka moja katika eneo hilo la UBUNGO MAZIWA kwa lengo la kupora, ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la MWARAMI RAJABU amejeruhiwa na watu hao wanasadikiwa kuwa ni majambazi

Mpango wa kumtimua Zitto Kabwe ndani ya CHADEMA wafichuka....

Image
  Habari  yako  Mpekuzi. Kuna  mpango  wa  kumung'oa Zitto kwenye nafasi yake ya naibu katibu mkuu- CHADEMA  ambao  ulisukwa kiufundi sana   ndani  ya kikao  kilichoitishwa  na  Mbowe... Nimekuwa  nikihangaika  sana  kuufichua  ukweli  bila  mafanikio.Jana  niliiweka  habari  hii  JF  lakini  waliitoa  kwa  maslahi  yao  binafsi....Naomba  ujumbe  huu  uwafikie  wanachama  wote  wenye  mapenzi  ya  dhati  na  Chama  chetu.   Kikao hicho kilifanyika nyumbani kwa Mbowe katikati ya mwezi octoba mwaka huu na  kilihudhuriwa na LEMA, MNYIKA, SUGU, WENJE, MSIGWA na BAUNSA mmoja aitwaye  SWAI, Katika kikao kile Mbowe aliwadhihaki wabunge wake aliokuwa nao kikaoni kwa kusema wanamuogopa zitto  na  kwamba  amewakalia  kichwani  utadhani  *****   Kauli  hiyo iliamsha hasira za Wenje na kuanza kuporomosha matusi kwa Zitto bila yeye kuwepo pale. Mnyika alionekana mwenye hofu sana juu ya mipango ile na baada ya mipango kuanza aliamua kuzuga kuwa amepigiwa simu na

HII NI LAANA....!!! PICHA ZA UCHI ZA MKE WA MTU NA KIGOGO WAKIFANYA "NGONO" ZANASWA

Image
  Kigogo mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja, anayefanya kazi  katika kampuni ya simu za mkononi  na mwanamke aliyetajwa kwa jina la Mwamvua anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu wamerekodi video wakifanya uchafu na ‘clip’ hiyo imevuja. Habari za kuaminika kutoka kwa chanzo chetu makini zinasema kwamba mke wa kigogo huyo aitwaye Zainab ndiye anayesambaza video hiyo kwenye mitandao mbambali na mitaani. Inaelezwa kwamba, Zainab alianza kupatwa na wasiwasi na tabia ya mumewe muda mrefu, hivyo akaanza kumfuatilia kwa karibu, ambapo alifanikiwa kunasa meseji za mapenzi kati ya mumewe na Mwamvua.    Zainab alivumilia bila kumwambia mumewe, lakini aliendelea kumfuatilia ili apate uhakika. “Aliamua kuchukua namba za simu za yule mwanamke kisha akampigia na kumuonya amuachie mumewe, lakini akamjibu mbovu,”  alitutonya mnyetishaji wetu   Akaongeza:  “Lakini siku moja aliona

JE! NI KWELI RAY C NA RECHO WANAFANANA SAUTI NA SURA???TUPE MAONI YAKO

Image
Mara ya kwanza tu Recho alipoanza kusikika, sauti yake ilianza kufananishwa na ya Ray C. Kuanzia kwenye Kizunguzungu, Upepo na Nashukuru Umerudi, Recho alikuwa Ray C mtupu. Hata hivyo hiyo haikumsumbua, Ray C ambaye alisema kuwa ni faraja kumsikia Recho akiimba kama yeye na tangu hapo wamekuwa marafiki. Lakini wawili hawa, hawafanani sauti tu. Picha hii (hapo juu) iliwekwa na Ray C kwenye Instagram na wengi walidai kuwa, warembo hao, USISAHAU KULIKE KURASA ZET ZA FACEBOOK/ TWITTER KWA HABARI ZAIDI

M23 WASALIMU AMRI NCHINI KONGO.

Image
Kundi hilo la waasi limesema katika taarifa yake kuwa "limeamua kuanzia leo kumaliza uasi wake" na badala yake litatimiza malengo yake "kupitia njia za kisiasa pekee".  Waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesema wamesalimu amri baada ya kukabiliwa na mashambulizi makali na jeshi la serikali linalosaidiwa na Umoja wa Mataifa ili kuwaondoa mashariki mwa nchi hiyo   Hatua hiyo inamaliza uasi ambao umedumu miezi 18 na kuliharibu eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa raslimali na maliasili, lililokuwa kitovu cha mojawapo ya migogoro mibaya zaidi barani Afrika katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.     Majeshi ya Congo yakisheherekea katika eneo la Kibati, karibu na Goma baada ya kuwafurusha waasi Awali, serikali mjini Kinshasa ilidai "ushindi kamili" dhidi ya M23 baada ya kuyakomboa maeneo mawili ya milima yaliyokuwa yametwaliwa na wapiganaji hao. Lambert Mende, waziri wa mawasiliano na msemaji wa serik

NAPE ATIMIZA AHADI KWA WANANCHI WA NYAMONGO

Image
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifafanua jambo wakati wa kikao maalum cha ndani na wakazi wa eneo la Nyamongo, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa wakieleza kero zao na wamiliki wa mgodi wa North Mara .   Ndugu Elizabeth Malembela akielezea jinsi utaratibu ulivyombovu wa kuwahamisha na kuwalipa fidia wakazi wanaoishi kando kando ya mgodi wa North Mara.   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisikiliza kwa makini malalamiko ya wananchi wa Nyamongo juu ya ukiukwaji wa utaratibu na mikataba baina ya wawekezaji na Wanavijiji.  Mkuu wa Wilaya ya Tarime Ndugu John Henjewele akiwaelezea wakazi wa Nyamongo kazi za kikosi kazi (Task force) katika kurahisisha shughuli za kutathimini ardhi na kuchukua malalamiko ya wananchi dhidi ya wawekezaji wa mgodi wa North Mara.  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye akiangalia moja ya eneo linaloaminika kuti