Mpango wa kumtimua Zitto Kabwe ndani ya CHADEMA wafichuka....


 
Habari  yako  Mpekuzi.
Kuna  mpango  wa  kumung'oa Zitto kwenye nafasi yake ya naibu katibu mkuu- CHADEMA  ambao  ulisukwa kiufundi sana   ndani  ya kikao  kilichoitishwa  na  Mbowe...

Nimekuwa  nikihangaika  sana  kuufichua  ukweli  bila  mafanikio.Jana  niliiweka  habari  hii  JF  lakini  waliitoa  kwa  maslahi  yao  binafsi....Naomba  ujumbe  huu  uwafikie  wanachama  wote  wenye  mapenzi  ya  dhati  na  Chama  chetu.
 
Kikao hicho kilifanyika nyumbani kwa Mbowe katikati ya mwezi octoba mwaka huu na  kilihudhuriwa na LEMA, MNYIKA, SUGU, WENJE, MSIGWA na BAUNSA mmoja aitwaye  SWAI,

Katika kikao kile Mbowe aliwadhihaki wabunge wake aliokuwa nao kikaoni kwa kusema wanamuogopa zitto  na  kwamba  amewakalia  kichwani  utadhani  *****
 
Kauli  hiyo iliamsha hasira za Wenje na kuanza kuporomosha matusi kwa Zitto bila yeye kuwepo pale.

Mnyika alionekana mwenye hofu sana juu ya mipango ile na baada ya mipango kuanza aliamua kuzuga kuwa amepigiwa simu na mama yake mzazi anamuhitaji nyumbani.

Baada ya Mnyika kuondoka Lema alisema: ''Mnyika hana msaada wowote hapa maana   ni muoga  sana''

Mbowe alianza kuwauliza kila mmoja ana mbinu gani ya kumzuia Zitto asigombee nafasi yoyote ya chama.

Lema alinyanyuka na kusema: "Huyu Zitto lazima tumkalishe chini kiakili sana, kwanza tumpe psychological disambiguate zitakazomfanya ashindwe kuwaunganisha watu wake, mimi nitaifanya hiyo kazi....."

Baada  ya  kauli  ya  Lema, Wenje  naye  alitoa  njia mbadala kwa kusema:

"Watu wa zitto si tunawafahamu, sasa tuwapige chini kisha uchaguzi uitwe haraka kwa kuwatumia viongozi watakaokuwa wamekaimu nafasi za wajumbe wa mikutano mikuu,

Wakati huo Sugu na Msigwa wao walikuwa kimya huku Msigwa akitikisa kichwa kwa kukubaliana nao.

Mbowe alimalizia kwa kusema kuwa  ni lazima Zitto avurugwe kiakili ili aropoke awatukane au awaseme viongozi wa taifa.....

"Akisha wataja na kuwahusisha na tuhuma atakazopewa tu, tutaitisha kamati kuu kisha tutajadili na ikiwezekana tutapiga kura ya kutokuwa na imani nae ili asimamishwe uongozi..

"Wakati akihangaika kusubiri  kikao cha baraza kuu kukata rufaa tutakuwa tumeshaitisha uchaguzi wa chama  na  yeye  hataruhusiwa kugombea kwa sababu atakuwa hajamaliza mzozo wake."Alisema Mbowe  na  kuongeza:

"Kuanzia sasa mimi nitazunguka maeneo yenye mtandao wake, nitawaondoa wanaomuunga mkono na kusimika viongozi wa muda wenye mlengo wetu ambao watasaidia kushinda uchaguzi wetu."

Kauli  ya Mbowe  imeshaanza  kutekelezwa  ambapo  mpaka  sasa Mbowe  amemsimika  Kasulumbai  kanda  ya  Mashariki .Kasulumbai  aliagizwa  akusanya watu kwa basi toka vyuo vilivyo shinyanga  na kisha wakapewa uongozi wa wilaya bandia hata kama hawajui wilaya zenyewe ziko mikoa gani.

Pamoja  na  hayo, Mbowe  amemtimua  mwenyekiti wa  Mara, kawafukuza  viongozi  wengi  wa  wilaya  na  Kata  ambao  walikuwa  upande  wa  Zitto. 

( Tumetumiwa  habari  hii  na  ndugu  aliyejitambulisha  kwa  jina  moja  la  Konga.)

Comments

Popular posts from this blog