WADAU WA MFUKO WA BIMA YA AFYA MKOA WA NJOMBE WATAKA KUWEPO KWA UTARATIBU WA KUUNGANISHWA KTK MFUKO HUO
Kaimu Mkurugenzi mkuu wa NHIF Hamisi Mdee akitoa taarifa ya Utekelezaji ya kuanzia 2001 hadi June 2013, |
Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Balozi Ali Mchumo akitoa salamu za NHIF kwa washiriki wa mkutano |
Meneja uendeshaji wa NHIF, Salome Manyama akiwasilisha mada katika mkutano huo, picha ya tano wadau wa mkoa a Njombe wakifuatilia mada..
Na FrancisGodwin Blog Njembe
Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Njombe, wameushauri kuwepo kwa utaratibu wa kuunganisha huduma za Mfuko huo na ule wa Afya ya Jamii (CHF) ili kuondoa dhana ya ubaguzi katika ugawaji wa dawa kwenye vituo vya matibabu.
Ushauri huo umetolewa mjini Njombe katika mkutano wa wadau wa NHIF wa mkoani humo.
Kukosekana kwa dawa kwa wanachama wa CHF wakati wale wa NHIF wanapata dawa hizo kumeonekana Kuwa Kero kwa Wananchi Wengi Mkoani Njombe Katika Mpango wa Kujiunga na Mifuko Hiyo Hali Inayopelekea Wanachi Wengi kusita Kujiunga na Mifuko Hiyo.
Akizungumza Wakati wa Kufungua Kikao cha Wadau wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Njombe Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bi.Mgeni Baruani Amesema Kuwa Serikali Inaendelea na Mkakati wa Kuhakikisha Jamii Inapata Huduma Stahiki Kadri ya Michango yao.
Pamoja na Mambo Mengine Bi.Baruani pia Ameeleza Kuwa Serikali Inaendelea kuwashukulia hatua za kisheria Wauguzi wanaoshindwa Kuwahudumia Wagonjwa Kwa Mujibu wa Kanuni na maadili ya Uuguzi Hapa Nchini.
Katika Hatua Nyingine Baadhi ya Wadau Kutoka Katika Wilaya Mbalimbali za Mkoa wa Njombe Wamelalamikia Uhaba wa Dawa Kwenye Vituo Hivyo, Hali Inayosababisha usumbufu na gharama za ziada kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambao wanachangia huduma za matibabu kupitia makato ya mishahara yao ya kila mwezi.
Wameongeza Kuwa ni Vyema Serikali Ikapanua Wigo wa Upatikanaji wa Huduma za Afya Kupitia Mifuko ya Afya ya Jamii Ili Kumpa Fursa Mwananchi wa mfuko huo Kupata Huduma Mahali Popote Anapokuwepo Tofauti na Sasa ambapo mwanachama hupata Huduma Hiyo Kwenye halmashauri alilojiunga tu.
Comments
Post a Comment