Watu 35 wakamatwa baada ya kutuhumiwa kuhusika na mauaji ya waandishi wa habari wawili ya RFI mjini Kidal kakazini mwa Mali


Na Ali Bilali
Operesheni maalumu ya jeshi la Mali na vikosi vya Ufaransa nchini Mali, imefanikisha kukamatwa kwa watu zaidi ya 35 wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya waandishi wawili wa habari rais wa Ufaransa, Ghislaine Dupont na Claude Verlon waliouawa mwishni mwa juma mjini Kidal. 
Kukamatwa kwa watu hawa kunakuja saa chache baada ya kuwasili kwa miili ya waandishi wa habari jijini Paris tayari kwa taratibu nyingine za mazishi.
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita wakati akitoa heshima zake za mwisho kabla ya kusafirishwa kwa miili ya waandishi hao, alielezamaskitiko yake na kulaani kundi lililohusika kwenye mauaji yao.

Kwa upande wake mkurugenzi anayehusika na masuala ya Afrika kwenye idhaa ya RFI, Yves Rocles amesema kuwa RFI imepoteza watu muhimu kwenye tasnia ya habari lakini amefarijika kwakuwa msiba huu haukuwa wa nchi ya Ufaransa pekee bali kwa dunia.

Katika hatuwa nyingine, serikali ya Ufaransa imesema kuwa imepeleka zaidi ya wanajeshi mia moja na hamsini kaskazini mwa nchi ya Mali na hasa kwenye mji wa Kidal kwa lengo la kuimarisha usalama na kuwasaka wapiganaji wenye silaha ambao wanaendesha vitendo vya uasi kwenye maeneo hayo.




Hatua ya ufaransa kutangaza kuongeza nguvu ya wanajeshi 150 kaskazini mwa nchi hiyo, inakuja kufuatia kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama kwenye maeneo hayo pamoja na kuuawa kwa waandishi wa habari wawili rais wa Ufaransa.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius amesema hatuwa hiyo ya kuongeza majeshi zaidi katika eneo hilo, itasaidia hata serikali ya Mali kuongeza wigo wa utawala wake baada ya usalama kurejea.


Comments

Popular posts from this blog