MKUTANO WA KIMATAIFA WA ADHABU MBADALA YA KIFUNGO GEREZANI WAFUNGULIWA DAR ES SALAAM
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi, akiisoma hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ambaye alimuakilisha katika mkutano wa siku tatu wa masuala wa adhabu mbadala wa kifungo gerezani unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Holiday Inn, jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo uliojumusiha nchi ya Ethiopia, Kenya, Malawi, Rwanda, Afrika Kusini, Sudani ya Kusini, Uganda, Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania. Kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu nchini, Shabani Lila na Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Jamii, Fidelis Mboya. Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Huduma kwa Jamii, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na Maboresho ya Sheria za Adhabu la Penal Reform International.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Wacheza ngoma wa Jeshi la Magereza, Dar es Salaam, wakitoa burudani kwa washiriki wa mkutano wa masuala wa adhabu mbadala wa kifungo gerezani unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Holiday Inn, jijini Dar es Salaam. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman aliufungua mkutano huo unaojumusha nchi ya Ethiopia, Kenya, Malawi, Rwanda, Afrika Kusini, Sudani ya Kusini, Uganda, Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania. Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Huduma kwa Jamii, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na Maboresho ya Sheria za Adhabu la Penal Reform International. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (watatu kushoto-waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (katikati-waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa kutoka nchi ya Ethiopia, Kenya, Malawi, Rwanda, Afrika Kusini, Sudani ya Kusini, Uganda, Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania. Mkutano huo ambao umeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Huduma kwa Jamii, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na Maboresho ya Sheria za Adhabu la Penal Reform International umefunguliwa katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Holiday Inn, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (wapili kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya adhabu mbadala ya kifungo gerezani kwa waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano wa siku tatu wa masuala wa adhabu mbadala wa kifungo gerezani katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Holiday Inn, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi, ambaye alimwakilisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi katika mkutano huo. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Jamii, Fidelis Mboya, na kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendelezaji wa Magereza wa Jeshi la Magereza, Dk Juma Malewa. Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Huduma kwa Jamii, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na Maboresho ya Sheria za Adhabu la Penal Reform International. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Comments
Post a Comment