David Cameron Ajiuzulu
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron ametangaza kujiuzulu wadhifa huo baada ya Uingereza kupiga kura ya kujitoa rasmi kwenye Umoja wa Ulaya (EU).
Cameron ametangaza uamuzi huo wakati akitoa hotuba yake ambapo amesema Uingereza inahitaji uongozi mpya.
Itachukua miezi mitatu kuandaa serikali ijayo.
Wakati hayo yakitokea, Paundi ya
Uingereza yaanguka dhidi ya dola ya Marekani baada ya kura ya kujitoa
EU, anguko hilo halijapata kutokea tangu mwaka 1985.
Matokeo yaonesha asilimia 52% ya
Waingereza wamepiga kura kutaka kujitoa katika Umoja wa Ulaya huku 48%
wakitaka kubaki katika umoja huo
Comments
Post a Comment