Posts

BREAKING NEWS : GOODLUCK OLE MEDEYE AIKIMBIA CHADEMA,AHAMIA UDP

Image
​ Kada wa CHADEMA na mbunge wa zamani wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye leo ametangaza kuhamia UDP. Asema inasimamia haki na demokrasia. Anasema anataka demokrasia ya kweli na jukwaa la haki ktk kuleta haki na maendeleo kwa Watanzania. Ameyasema haya akiongea na waandishi wa habari muda mfupi uliopita.

Utafiti umeonesha wanaume wenye vipara ni wanaume wenye mvuto zaidi kimapenzi!

Image
Kuna vitu vingi humvutia mtu inapokuja swala la kumchagua mpenzi, siwezi taja sifa zote, kila mtu anasifa zake na vigezo vyake, ila ngoja tuongelee mvuto wa kipekee unaopatikana kwa wanaume wenye vipara. Nikiongelea vipara naongelea wale walio na vipara asili, achilia mbali wale wanaopenda kunyoa vipara japokuwa kuna baadhi ya sifa hapa wanaweza wakawa nazo pia. Muonekano wa kiume: wanaume wenye vipara wengi huwa na muonekana wa kiume zaidi,muonekano nadhifu  sina maana kama wanaume wengine walio na nywele ndefu ama wastani hawana mvuto lah, nauongelea mvuto zaidi ama mvuto wa kipekee. Ujasiri: wanaume wa aina hii wengi huonekana ni wajasiri kwa muonekano wao tu, hii huwafanya kuwa kivutio kwa wanawake. Wana hisia kali za kimapenzi: daktari kutoka Chuo cha Yale Marekani , James B. Hamilton alisema katika utafiti wake wanaume wengi walio na vipara miili yao huwa inazalisha mbegu nyingi za kiume kuliko wanaume wenye nywele, japokuwa si kwa asilimia 100 alisema pi

SERIKALI YATANGAZA UTARATIBU MPYA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, PIA YAFAFANUA FEDHA ZILIZOOKOLEWA KUTOKANA NA WATUMISHI HEWA

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah Kairuki akiongea na waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2016.   Na. Aron Msigwa – Dar es salaam. SERIKALI imetangaza utaratibu mpya utakaofuatwa wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kuanzia Juni 16 hadi 23, 2016 ambapo imewaagiza Watendaji Wakuu katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisi za Serikali kutenga siku moja ya kukutana na watumishi katika sehemu zao za kazi kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi. Aidha, imewaagiza watendaji hao kutenga siku nyingine moja kwa ajili ya kukutana na wananchi, kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero zao zinazohusiana na huduma zinazotolewa na Taasisi zao. Akitangaza utaratibu huo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa Serikali imeamua kubadili mfumo wa maadhimisho h

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AONGOZA MATEMBEZI YA WAFANYAKAZI WA BENKI KUU.

Image
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na wasanii wa Benki Kuu baada ya kuongoza matembezi  kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu hadi viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016.  Zaidi ya shilingi milioni263 zilichangwa. Bendi ya Poli ikiongoza matembezi  ya kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu hadi viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016.Zaidi ya shilingi263 milioni zilichangwa.    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza matembezi ya kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu ha viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 11, 2016.Kushoto kwake ni Gavana wa Benki Kuu, Benno Ndulu na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. Zaidi ya shilingi milio

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI

Image
Aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.   Mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba ameteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.  

Wawili wawachinja wake zao, mwingine amuua mama yake!

Image
Matukio ya Dodoma Samson Joramu(44), mkazi wa Chololo, Kata ya Kikombo, alimchinja mke wake, Rehema Joram (43) kabla ya kujiua kwa kunyonga katika shamba lake. Watu walioshuhudia walisema, Joramu baada ya kumuua mkewe alijinyonga na aliandika ujumbe uliokutwa mfukoni kwake, ukisomeka: “Mama tunza wanangu, mimi nimekufa.” Kadhalika aliandika orodha ya watu anaowadai. Katika tukio jingine, Amos Kalenda, mkazi wa Kikombo, Dodoma anadaiwa kumuua mama yake mzazi, Joyce Kalenda kwa kumchinja. Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa ni mama huyo kumnyima chakula. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa akizungumzia tukio hilo alisema kuwa: “Ni kweli taarifa za vifo kutoka Kikombo ninazo, yule mmoja alimuua mama yake kwa kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili jana (juzi), na huyu mwingine alimuua mke wake asubuhi ya leo (jana) kisha naye akajinyonga,” alisema. Tukio la Tarime Mkoani Mara katika Wilaya ya Tarime, Wambura Mariba (50) mkazi wa Matongo, Nyamongo, T

ANGALIA PICHA ZA SHEREHE UFUNGUZI WA MICHUANO YA EURO 2016

Image
Michuano ya UEFA Euro 2016 ilianza rasmi kufanyika Ufaransa usiku wa June 10 2016 kwa kupigwa mchezo kati ya Ufaransa dhidi ya Romania, kabla ya kuanza kwa mchezo huo kulifanyika sherehe mbalimbali za kuashiria usiznduzi wa michuano hiyo. Wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo kulikuwa na burudani mbalimbali ikiwemo perfomance za muimbani Zara Larsson na David Guetta walikuwepo pia kuburudisha watu katika michuano hiyo kwa mwaka 2016.

RAIS DKT. MAGUFULI AAGANA NA BALOZI WA OMAN ANAYEMALIZA MUDA WAKE HAPA NCHINI.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Oman hapa nchini Soud Al Ruqaishi ambaye anamaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Oman hapa nchini Soud Al Ruqaishi ambaye anamaliza muda wake wa kufanyakazi hapa nchini.

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA JAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI PAMOJA NA JAJI KIONGOZI, PIA AAGANA NA BALOZI WA OMAN ANAYEMALIZA MUDA WAKE HAPA NCHINI.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Shaaban Ali Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Jaji Shaaban Ali Lila mara baada ya kumuapisha kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali mara baada ya kumuapisha kuwa Jaji Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Read more »  

Kesi ya Bosi wa TRA na Wenzake Yarudishwa Tena Mahakama Kuu

Image
                 Mahakama ya Rufani Tanzania, imeamuru jalada la kesi inayomkabili Kamishna Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake kurudishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa rufani ya Jamhuri. Pia, imeagiza jalada hilo lipangiwe kusikilizwa kwa jaji mwingine dhidi ya rufaa ya kupinga kuondolewa shtaka la utakatishaji fedha katika kesi ya kujipatia Dola za Marekani milioni 6. Hukumu hiyo ilisomwa jana na Msajili wa Mahakakama ya Rufani, Zahra Maruma baada ya kusikilizwa na jopo la majaji watatu, likiongozwa na Mwenyekiti Salum Masati akisaidiana na Kipenka Musa na Augustine Mwarija. Msajili Maruma alisema mahakama hiyo imeona kwamba Jaji Mfawidhi Moses Mzuna alikosea kukubali pingamizi la utetezi na kutupilia mbali kusikiliza rufani ya kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wa kuliondoa shtaka la kutakatisha fedha dhidi ya Kitilya na wenzake. “Mahakama hii imebatilisha uamuzi uliotolewa na Jaji Mzu

Pichaz: Muhammad Ali Alivyoagwa Kiislamu

Image
                  Maombi ya Kiislamu ya kuswaliwa kwa jeneza la marehemu bondia mashuhuri duniani Mohammed Ali yamefanyika katika jimbo la Kentucky, Marekani. Ali alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 74.  Maelfu ya watu, wakiwemo Waislamu kutoka maeneo mengi duniani, wamehudhuria swala hiyo katika ukumbi wa Freedom Hall, mjini Louisville.  Swala hiyo inapeperushwa moja kwa moja kupitia runinga na Waislamu wengi duniani wanatumai kwamba itaashiria mchango mzuri kwa dini ya Kiislamu nchini Marekani. Muhammad Ali alisilimu akiwa kijana. Alikuwa kwanza mwanachama wa madhehebu ya Nation of Islam, kundi lililotetea haki za watu weusi, lakini baadaye akakumbatia imani ya kawaida ya Kiislamu. Mazishi yake yatafanyika leo Ijumaa <a href='http://kwanza.co.tz/login/www/delivery/ck.php?n=a397efbc&cb=INSERT_RANDOM_NUMBER_HERE' target='_blank'><img src='http://kwanza.co.tz/login/www/delivery/avw.php?zone