YULE BI HARUSI ALIYETOROKA SIKU MOJA BAADA YA KUFUNGA NDOA ANASWA LIVE.


YULE mwanamke Tatu Ally, mkazi wa Kongowe, Mbagala jijini Dar aliyefunga ndoa na kutoroka kwa mumewe aliyetajwa kwa jina moja la Ramadhan, mkazi wa Mbezi-Kimara, amenaswa baada ya msako mkali uliofanywa na polisi kwa kushirikiana na ndugu zake.
Stori ya Tatu kutoroka kwa mumewe siku moja baada ya kufunga ndoa iliripotiwa na gazeti hili wiki iliyopita, ukurasa wa nyuma, ikiwa na kichwa cha habari kilichosomeka:BI HARUSI AFUNGA NDOA, ATOROKA.
Habari kutoka kwa chanzo cha kuaminika kilieleza kuwa, Tatu alikutwa na mwanaume mwingine maeneo ya Toangoma, Kigamboni, Dar na kujitetea kuwa aliamua kutorokea kwa mwanaume huyo kwa kuwa ndiye mchumba’ke wa siku nyingi na alikuwa amesafiri kwa muda tu.
“Kweli Tatu amepatikana na alipelekwa moja kwa moja kwenye Kituo cha Polisi cha Kongowe-Mwisho, huku akiwa na huyo anayedai ni mchumba’ke wa siku nyingi (jina halikupatikana).Ilisemekana kwamba, Tatu akiwa mikononi mwa polisi alinena kuwa mwanaume huyo alikuwa amesafiri kwa muda na hawakuwa na mawasiliano yoyote kati yao.


“Alipohojiwa vizuri na polisi, Tatu alisema kuwa mwanaume huyo aliporudi na kusikia amechumbiwa aliamua kunywa sumu kwa sababu walipanga waoane na hakufikiria kama Tatu angemfanyia hivyo.


“Tatu alisema alitoroka ili akaokoe maisha ya huyo mchum
ba’ke, jambo ambalo alifanikiwa,” kilisema chanzo hicho.


Mbali na yote, baada ya Tatu kufikishwa kituoni hapo, mume aliyefunga ndoa na Tatu (Ramadhan) alikomaa alipwe gharama zake zote alizotumia siku hiyo ya ndoa pamoja na mahari ndipo mchumba huyo wa zamani wa Tatu alisema atalipa deni hilo.


“Jamaa wa zamani wa Tatu ameomba apewe muda ili alipe gharama zote anazodai yule mume mwingine.


“Pia ameahidi kuwa akimaliza kulipa deni hilo atamuoa Tatu lakini baba yake Tatu, Mzee Ally anamng’ang’ania mwanaye arudi nyumbani,” kilisema chanzo. Polisi kituoni hapo walithibitisha kuwepo kwa tukio hilo huku wakigoma kutajwa gazetini kwa kuwa siyo wasemaji wa jeshi hilo

Comments

Popular posts from this blog