MADEREVA WAPEWA KIPAUMBELE KWENYE KAMATI YA KUSIMAMIA USAFIRISHAJI.
Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na wandishi wa habari
hawapo pichani ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
wandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano wa wandhi wa habari na
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda jijini Dar es Salaam
leo.(Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Madereva
wamepewa kipaumbele kwenye tume itakayokuwaikisimamia usafirishaji,kwani
tume hiyo itakuwa na wajumbe watano kutoka Umoja wa madereva tuu na
kutoka sekta nyingine watakuwa wajumbe watatu .
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakati
akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam
leo.
Makonda
amesema kuwa kamati hiyo haitaundwa na serikali, wajumbe watatokana na
uchaguzi wa madereva wenyewe pia na wajumbe wengine watatoka Mamlaka ya
usafirishaji (SUMATRA), TABOA , TATOA, Wizara ya Ajira, wizara ya na
mambo ya ndani.
Makonda
ameongezea kuwa Mgomo wa madereva hautakuwepo tena milele, madereva
wachague wajumbe ambao wanaweza kuhakikisha haki zao kinasimamiwa vizuri
na kutatua matatizo yao.
Comments
Post a Comment