ADEBAYOR AVIANIKA VISA VYA FAMILIA YAKE NA INAVYOMCHUMA FEDHA, BARUA YAKE YASIKITISHA WENGI, IMETAFSIRIWA KISWAHILI HAPA

Mshambuliaji wa Tottenham, Emmanuel Adebayor ameandika maelezo marefu kwenye akaunti yake ya Facebook kuelezea visa anavyofanyiwa na familia yake wakiwemo mama, kaka na dada zake. Adebayor anawashutumu ndugu zake kwa tamaa ya mali zake. Licha ya kuwafanyia mambo mengi ikiwemo kuwajenga nyumba, kuwanunulia magari na kuwapa mitaji ya biashara, wameendelea kumtupia shutuma nyingi. Tumeitafsiri post hiyo kwaajili yako. Sehemu ya maelezo hayo marefu inasema: SEA,
nimezihifadhi habari hizi kwa muda mrefu lakini nadhani leo ni muhimu kuziweka wazi baadhi yake kwenu. Ni kweli masuala ya kifamilia yanapaswa kusuluhishwa ndani kwa ndani na sio hadharani lakini nafanya hivi ili pengine familia zote zinaweza kujifunza kutokana na kile kilichotokea kwangu. Pia weka akilini kuwa hakuna chochote kati ya haya kinahusiana na pesa. Nikiwa na miaka 17, kwa mishahara yangu kama mcheza soka, nilijenga nyumba kwaajili ya familia yangu na kuhakikisha kuwa wapo salama. Kama nyote mnavyojua, nilishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2008. Nilimpandisha pia mama yangu jukwaani kumshukuru kwa kila kitu. Katika mwaka huo huo, nilimleta London kwaajili ya kufanyiwa vipimo mbalimbali. Baada ya mtoto wangu wa kike kuzaliwa, tuliwasiliana na mama yangu kumjulisha lakini muda mfupi alikataa simu na hakutaka kujua chochote. Nikisoma maoni yenu ya hivi karibuni, baadhi ya watu walisema mimi na familia yangu tungemtafuta T.B Joshua. Mwaka 2013, nilimpa mama yangu fedha ili amtafute (Joshua) nchini Nigeria.

Comments

Popular posts from this blog