SHAA AKIRI KUTEMBEA NA MASTER JAY ... AANIKA SIRI ZAO NZITO NZITO
Akihojiwa katika kipindi cha ng'ari ng'ari, Shaa alisema," mimi sikuwa sababu ya kuachana kwa wao wawili (master jay na mama watoto wake),kwani ugomvi au kuachana kwa watu wawili huwa inahusu wao wenyewe wawili ila sio mtu watatu, na kwakuwa mimi nilikuwa nimetoka kutendwa ilichukua muda kidogo hadi kuja kuwa na mahusiano na Master Jay hata yeye pia aliniambia alikuwa na maumivu yake ndio mana ilichukua muda hadi kuwa na mahusiano. Hivyo kwanini niachie bahati yangu, Nampenda sana Master"
Mtangazaji: Huwa unapika ukiwa nyumbani, ili kumpagawisha mzee
Shaa: Nashukuru sana kwani Master anapenda sana kupika kwakweli na mara nyingi huwa anapika yeye kuliko mimi, na Inshalah namshukuru sana Mwenyezi Mungu
Comments
Post a Comment