Mapigano yazuka tena Kongo
Mapigano yanayoendelea baina ya waasi
wa M23 na wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
katika eneo la Kibati karibu na mji wa Goma, yanatajwa kuwa yamewaathiri
raia katika eneo la mapigano.
Mji wa Goma ulipigwa na mshituko jioni
jana, pâle mabomu yalipokuwa yanavurumishwa katika mji huo. Ni kata za
Katindo ya kushoto pamoja na Murara ndizo ziliathirika na mabomu hayo.
Katika kata la Murara, duru toka machifu wa kata hizo zadokeza, kuwa
watu watano ndio walijeruhiwa mukiwemo watoto watatu ambao hali yao ni
mahututi.
Ili kuwakinga raia, mwakilishi maalumu
wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo, Martin Kobler,
aliwaamuru wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kuhakikisha kuwa wanawalinda
raia hao, huku msemaji wa Tume ya Umoja wa Mataifa katika Kongo hasa
katika miji ya Beni na Butembo, Moussa Demba Dialo, akipewa muda wa
masaa 44 kuondoka eneo hilo. Ilani hiyo imetolewa na mashirika ya
kiraia.
Vita vya maneno vimezuka baina ya
serikali za Rwanda na DRC. Rwanda kupitia msemaji wa jeshi lake Joseph
Nzabamwita imesema kuwa Kongo kwa maksudi ilivurumisha roketi katika
ardhi yake, jambo alilolitaja kuwa ni uchokozi mtupu.
Kwa upande wake msemaji wa serikali ya
Kongo Lambert Mende Omalanga, ametangaza kuwa, mabomu yaliyoanguka Goma
nakusababisha mahafa katika mji huo, yalitokea katika nchi jirani ya
Rwanda. Navyo vita vikiwa bado vinaendelea baina ya jeshi la serikali ya
DRC na waasi wa M23 katika kijiji cha Kibati, na ilikuwazuia waasi wa
M23 kuuteka mji wa Goma pamoja na kuwakinga raia, muwakilishi maalumu wa
katibu mkuu wa UN katika DRC Martin Kobler, aliamuru majeshi ya UN
kufanya hima ilikuwakinga raia.
Kauli hiyo inatokea, baada ya vituo
vya Monusco pamoja na makaazi ya raia kulengwa na mashambulizi. Msemaji
wa jeshi la UN katika DRC luteni kanali Félix Basse, akizungumza na
redio ya UN Okapi alisema, kuwa tayari jeshi la UN liko kwenyi
tahadhari, na kuwa liko tayari kukabiliana na waasi wa M23 ikiwa
watasubutu kuusogelea mji wa Goma. "Kwa kweli tumezidisha mipango yetu
ya ukingo na tumekuwa tukipiga doria katika viunga vya mji wa Goma na
upande wa Sake, na huko Munigi tumeongeza idadi ya wanajeshi wetu, na
Tuko tayari kukabiliana na waasi wa M23 ikiwa watasubutu kuelekea katika
mji wa Goma," alisema Basse.
Wakati huo huo mashirika ya kiraia
katika mji na wilaya ya Beni, yamempatia muda wa ma saa arubaini na
nane, msemaji wa Monusco katika DRC hasa katika miji ya Beni na Butembo
Bwana Moussa Demba Dialo. Mashirika ya kiraia katika mji na wilaya ya
Beni, yamemupatia ma saa arubaini na nane kuondoka eneo hili. Na ikiwa
hatatii amri ya mashirika ya kiraia, kwa madhara yatakayotokea atajijuwa
mwenyewe.
Msemaji wa Monusco katika miji ya Beni na Butembo, anashukiwa na mashirika ya kiraia kuwatusi na kuita hatua yao yakutaka magari ya UN kutozunguka katika mitaa ya Beni kuwa ya utoto, na kuwa haikuathiri tume ya UN katika kazi zake.
Msemaji wa Monusco katika miji ya Beni na Butembo, anashukiwa na mashirika ya kiraia kuwatusi na kuita hatua yao yakutaka magari ya UN kutozunguka katika mitaa ya Beni kuwa ya utoto, na kuwa haikuathiri tume ya UN katika kazi zake.
Mwandishi: John Kanyunyu
Comments
Post a Comment