Posts

Mgambo Atokomea na Milioni 17 za Ushuru

Image
Mgambo mmoja aliyekuwa akikusanya fedha za ushuru wa maegesho ya malori Igunga Mjini mkoani Tabora, Peter Areray amekimbia na fedha hizo Sh milioni 17,253,000. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli amethibitisha mgambo huyo kutoroka na fedha hizo alizokuwa amekusanya katika kipindi cha mwaka 2019.

Profesa Kabudi: Niliandika barua ya kujiuzulu lakini ilichanwa

Image
FRIDAY JANUARY 24 2020         Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Nje nchini Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuna wakati aliandika barua ya kujiuzulu lakini alinyang’anywa na ikachanwa. Mbunge huyo wa kuteuliwa na Rais ameeleza hayo leo Ijumaa Januari 24, 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na kamati ya madini ya Barrick. Kabudi anasema alichukua uamuzi wa kuandika barua hiyo baada ya mchakato wa majadiliano na wajumbe wa Barrick kuwa magumu, kwamba aliona aibu kushindwa kazi aliyotumwa. Amemtaja aliyemnyang’anya barua hiyo ambayo haikuifafanua kwa kina ni Kasmir Simbakuki. “Nilifikia hatua nikafanya dhambi ya kukata tamaa nikasema jambo hili haliwezekani, niliona ni bora aibu na fedheha hiyo niibebe lakini barua niliyoandika sikufanikiwa kuileta.” “Nilisema sijawahi kutumwa kazi na mkuu wangu wa nchi ikanishinda,” amesema Kabudi. Amesema wakati huo aliku...

Mbowe na Viongozi 8 CHADEMA sasa wanasubiria hukumu

Image
Viongozi 9 wa CHADEMA, akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wanasubiri hukumu ya kesi yao baada ya kufunga ushahidi wao wa mashahidi 15. Hata hivyo, mahakama hiyo imempa onyo mbunge wa Kawe, Halima Mdee na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya baada ya kukiuka masharti ya dhamana. Hatua hiyo imefikiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa utetezi, Peter Kibatala kueleza kuwa hawaoni haja ya kuendelea na shahidi mwingine kwa sababu ushahidi uliotolewa na mashahidi wao 15 umejitosheleza. Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 24, 2020 kwa ajili ya kufanya majumuisho ya mwisho kabla ya kutolewa hukumu.

Lulu diva ataja siri kuvaa nusu utupu

Image
K UTOKANA  na hivi karibuni kuonekana kucharuka kwa kuvaa nusu utupu, staa wa muziki wa Bongo Fleva; Lulu Abasi ‘Lulu Diva’ ameibuka na kuanika siri inayomfanya kuwa hivyo.   Akichonga na  Amani,  Lulu Diva alisema siri ya kuvaa nusu utupu ni kwamba anapenda sana kwa kuwa nguo hizo zinamfanya awe huru kila anakokwenda hata mbele za watu anakuwa jasiri zaidi. “Napenda sana kuvaa nguo fupi zinazoonesha jinsi nilivyoumbika kwa kuwa nakuwa huru zaidi, sijali mtu mwingine ataizungumziaje maana watu wamezoea kutoa povu kwa kila kitu kiwe kibaya au kizuri kwa hiyo sijali wala nini, nitaendelea kuvaa ninachokipenda ili mradi niwe huru,” alisema Lulu Diva

Kigwangalla: “Walipanga Kuniangamiza, Walitaka Nitumbuliwe”

Image
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt Hamis Kigwangalla, ameeleza kuwa kwa sasa anaishi kwa hofu na tahadhali kubwa juu ya uhai wake kutokana na kuwepo kwa kundi la watu wanaomuwinda wakitaka kumuangamiza huku wengine wakimfanyia mipango ya kumuharibia ili atumbuliwe uwaziri. Kupitia akaunti yake ya instagram Kigwangala ameweka wazi kuwa hata alivyopata ajali aliwekewa ulinzi mkali wodini ili wabaya wake wasiweze kummalizia kwa namna yoyote. Kupitia instagram yake ameandika hivi; Sikusudii kufanya press conference. Watu wengi wamenishauri niishie hapa. Team yangu imefanya kazi nzuri, imenipa uthibitisho wa majina ya wanaotaka nichafuliwe ili niondolewe uwaziri. Bahati mbaya hakuna cha kunichafua nacho, wanapika hadithi za kitoto na kurudia tu. Walidhani ningekaidi maelekezo ya Mhe. Rais juu ya mgogoro wa ndani ya Wizara yetu ili Rais achukie aniondoe, wakakwama. Sikukaidi. Wakaona wafanye mwendelezo kupitia gazeti, sijataka kujibishana nalo, tutakutana mahakamani ambapo m...

Shiza Kichuya Aanza Kazi Simba SC leo

Image
BAADA ya kuvuna pointi sita muhimu katika michezo miwili ya Ligi Kuu Bara huko Kanda ya Ziwa, kikosi cha Simba leo kinaingia kambini kujiandaa na mchezo wa Kombe la FA, huku kiungo mshambuliaji Shiza Kichuya akiwemo kati yao. Simba inajianda na mechi ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga itakayopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Jumamosi hii. Katika mchezo huo, Simba wataingia uwanjani wakiwa na hasira za kufungwa katika mchezo wa ligi uliopigwa Uwanja wa Kambarage huko Shinyanga ambao ulimalizika kwa Mwadui kushinda bao 1-0. Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja Mkuu wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu alisema kuwa kikosi chao kitaingia kambini leo jioni huko Ndege Beach nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Rweyemamu alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yanakwenda vizuri na wachezaji wote wataingia kambini tayari kwa kuwawinda Mwadui kwa ajili ya kulipa kisasi cha kufungwa katika ligi. Aliongeza kuwa kiungo wao wa zamani Kichuya huenda akawa katika sehemu y...

Mshitakiwa Afariki Mahakamani

Image
SHUGHULI zilisimama kwa muda katika Mahakama Kuu mjini  Mbale  nchini  Uganda  baada ya mtuhumiwa kuanguka na kufariki dunia. Simon Mayuya  mwenye umri wa miaka 54 ambaye ni mkazi wa kijiji  Buyobo  Wilaya ya  Sironko  nchini  Uganda,  alifariki dunia muda mfupi baada ya kuanguka katika chumba cha watuhumiwa kabla ya kupandishwa kizimbani. Mayuya alikuwa amekaa miezi sita rumande katika gereza la  Maluku  ambapo alikua anakabiliwa na tuhuma za jaribio la mauaji. Anatuhumiwa kwa jaribio la kumuua binamu yake ambaye amemuajiri kama dereva wa lori. Mwanasheria wa  Mayuya  aitwaye  David Moli  amesema mteja wake alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya uti wa mgongo kutokana na kunusurika kwenye ajali ya gari aliyopata kabla ya kukamatwa na kuwekwa rumande. Moli ameongeza kuwa kabla hali ya mteja wake kuwa mbaya aliiomba mahakama kumpa dhamana ili apelekwe hospitali kupatiwa matibabu kabla y...

Amkata Kichwa Bosi Wake Kisa Kutomlipa Mishahara

Image
FUNDI makenika wa Halmashauri ya Wilaya ya  Sumbawanga  mkoani Rukwa,  Cathbert Mwangalaba  (47) ameuawa kwa kukatwa mwili wake na kiwiliwili chake, kutenganishwa na kichwa na kitu chenye ncha kali. Mlinzi ambaye alikuwa ameajiriwa na marehemu anadaiwa kumuua mwajiri wake huyo kwa kumchinja na kiwiliwili chake kutenganishwa na shingo yake. Anatuhumiwa kutenda ukatili huo, baada ya bosi wake huyo kushindwa kumlipa msh ahara wa miezi sita unaofikia Sh 360,000. Baada ya kumuua, mwili wake ulifukiwa katika shimo lililochimbwa shambani mwake katika Kijiji cha Kaondo Manispaa ya Sumbawanga. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masonje alithibitisha matukio hayo. Alisema kwamba mauaji ya kikatili ya Mwangalaba, yanadaiwa kufanyika saa 3:00 asubuhi Januari 17, mwaka huu shambani mwake kijijini Kanondo. Mwili wa marehemu ulibainika ukiwa umeviringishwa katika mfuko wa sandarusi, ukiwa umefukiwa katika shimo lililo ndani ya uzio wa shamba hilo. Baada y...

TCU Yavifutia Usajili Vyuo 9 Tanzania

Image
TUME ya Vyuo Vikuu ( TCU ) imefuta hati za usajili wa vyuo vikuu vishiriki vitano, vyuo vikuu vitatu na chuo kikuu kishiriki kimoja. Akizungumza jana Jumanne, Januari 21, 2020, jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa,  amesema vyuo hivyo vimeshindwa kujirekebisha na hata vingepewa muda zaidi visingeweza. Amesema vyuo vishiriki ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mkuu Yakobo (AJUCO), Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Kardinali Rugambwa (CARUMUCo) na Chuo Kikuu cha Theofilo Kisanji (Teku-Dar es Salaam), Chuo kikuu cha Mtakatifu Yohana cha Tanzania Kituo cha St Marks na Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta cha Kilimo tawi la Arusha (JKUA). “Kufuatia mashauriano na maombi yaliyofanywa na wamiliki wa vyuo na tume katika kikao chake cha 97 kilichofanyika Januari 20, 2020,  imeridhia maombi ya wamiliki hao kusitisha utoaji wa mafunzo, hivyo tume imefuta hati za usajili wa vyuo hivyo vishiriki na kuvifutia vibali,” amesema Profesa Kihampa. TCU pia im...

Matokeo Kidato cha Nne, Kidato cha Pili, Darasa la nne Haya Hapa

Image
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta)  leo Alhamisi, Januari 9, 2020 limetangaza matokeo ya mtihani wa upimaji darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne. Matokeo hayo yametangazwa na  Katibu Mtendaji wa Necta ,  Dk Charles Msonde  amesema ufaulu katika mtihani wa upimaji wa darasa la nne umeongezeka kwa asilimia 26.21. Jumla ya watahiniwa 1,531,120 kati ya wanafunzi 1,665, 863 wamepata alama A,B,C na D ikilinganishwa na wanafunzi 1,213, 132 waliofaulu mwaka 2018. Katika mtihani wa upimaji kidato cha pili, wanafunzi 514,251 sawa na asilimia 90.04 kati ya wanafunzi 571,137 wamefanya vizuri katika mtihani huo na kuwawezesha kuingia kidato cha tatu. Dk Msonde amesema mtihani wa kidato cha nne jumla ya watahiniwa 340,914 sawa na asilimia 80.65 ya watahiniwa 422,722 wameefaulu mitihani yao. Watahiniwa hao ni sawa na ongezeko la asilimia 1.38 ikilinganishwa na watahiniwa 284,126 sawa na asilimia 79.27 waliofaulu mtihani huo mwaka 2018. KUTAZAM...

Mbaroni kwa Kusimamisha Msafara wa Rais na Kuomba Kazi

Image
MWANAMME mmoja aliyejulikana kwa jina la Uvinalies Nyabuto amekamatwa leo kwa kuusimamisha msafara wa magari wa Rais Uhuru Kenyatta katika barabara ya kuelekea Ikulu. Kwa mujibu wa Polisi, msafara huo ulikuwa unaelekea Ikulu ukitokea Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) ambapo Rais Kenyatta alitoka kwenye mkutano wa 9 wa Wakuu wa Nchi za Caribbean na Pacific. Nyabuto alisimamisha msafara akiwa ameshika bango lililoandikwa “Mheshimiwa, Tafadhali naomba nafasi ya kujiunga na Majeshi ya Ulinzi. Nisamehe kwa kutoheshimu Ulinzi wako. Samahani Rais. Nyabuto.”. Mara moja alikamatwa na Walinzi walio kwenye msafara wa Rais na baadaye alipelekwa katika Kituo cha Polisi Kilimani ambapo aliendelea kushikiliwa.

Yanga Yataja Hatma ya Sadney, Lamine na Madeni Yake

Image
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla. MWENYEKI wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla, leo Desemba 10, 2019 amezungumzia tetesi za klabu hiyo kutowalipa mishahara wachezaji kwa muda wa miezi miwili na akaweka wazi hatma ya wachezaji Sadney Urikhob na Lamine Moro ambao inasemekana waliandika barua za kutaka kuondoka katika klabu hiyo kwa kutolipwa mishahara yao kwa miezi mitatu. Akiongea na wanahabari alisema ni kweli klabu yake haijawalipa wachezaji mishahara ya miezi miwili ambayo ni Oktoba na Novemba mwaka huu na kwamba iwapo mambo yakienda vizuri watalipwa leo. Aliongeza kwamba habari zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mshambuliaji Sadney Urikhob na beki  Moro Lamine, viongozi wamekubaliana kuachana na Sadney na watabakia na Lamine ambaye atalipwa mishahara yake. Akifafanua hali ilivyo klabuni hapo, amesema walipoingia madarakani mwezi Mei 2019 walikuta madeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na kudaiwa Sh. milioni 800 na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA)....

Rasmi Matola Kocha Msaidizi Wa Simba, Aanza Na Mkwara Huu

Image
SELEMAN Matola, ametangazwa kuwa Kocha Msaidizi wa Simba leo akipokea mikoba ya aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo. Matola amesema kuwa amerejea nyumbani na anaamini kwamba atafanya kazi kwa ukaribu kutokana na uzoefu alionao. “Nimerejea nyumbani na nina imani ya kufanya vema, nahitaji sapoti kwa mashabiki kutokana na kutambua vema falsafa ya Simba. “Nilikuwa ndani ya Simba kwenye timu ya vijana kwa sasa nitaendelea gurudumu kwa kushirikiana na benchi la ufundi,” amesema. Matola alikuwa kocha wa Polisi Tanzania alivunja nao mkataba wake wa mwaka mmoja baada ya kufika makubaliano mazuri na uongozi wa Simba na kwa sasa Polisi Tanzania ipo chini ya Malale Hamsini.

Mfungwa Aliyesamehewa na Rais JPM Agoma Kutoka Gerezani, Ajijeruhi

Image
KATIKA Sherehe za kuadhimishi kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Tanganyika, maadhimisho ambayo hufanyika kila mwaka Disemna 9, jana Rais Dkt Magufuli alitangaza msamaha kwa jumla ya wafungwa 5,533, ikiwa ni sehemu ya sherehe hizo ambapo kila mwaka wafungwa huachiliwa. Licha ya kuwa wengi huamini kwamba mfungwa anapopata taarifa kwamba anaanchiwa huru atakuwa mwenye furaha na kuchangamkia fursa hiyo, lakini kiuhalisi hali huwa haiko hivyo kwa kila mtu. Katika hali ya kushangaza Merad Abraham ambaye ni miongoni mwa wafungwa 70 waliosamehewa na Rais Dkt John Magufuli jana Disemba 9, amekataa kuondoka katika Gereza la Ruanda mkoani Mbeya akidai kuwa hana mahala pa kwenda huku akijijeruhi usoni kwa jiwe kwa nia ya kutaka ahamishiwe katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam. Meradi ambaye alifungwa kwa kesi ya kubaka alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela, Juni 20, 2000 na alitakiwa kumaliza kifungo Juni 20, mwakani. Kwa sasa mfungwa huyo amepelekwa kwenye zahanati ya ...