Mbowe na Viongozi 8 CHADEMA sasa wanasubiria hukumu

Viongozi 9 wa CHADEMA, akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wanasubiri hukumu ya kesi yao baada ya kufunga ushahidi wao wa mashahidi 15.
Hata hivyo, mahakama hiyo imempa onyo mbunge wa Kawe, Halima Mdee na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya baada ya kukiuka masharti ya dhamana.
Hatua hiyo imefikiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa utetezi, Peter Kibatala kueleza kuwa hawaoni haja ya kuendelea na shahidi mwingine kwa sababu ushahidi uliotolewa na mashahidi wao 15 umejitosheleza.
Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 24, 2020 kwa ajili ya kufanya majumuisho ya mwisho kabla ya kutolewa hukumu.

Comments

Popular posts from this blog