Amkata Kichwa Bosi Wake Kisa Kutomlipa Mishahara
FUNDI makenika wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Cathbert Mwangalaba (47) ameuawa kwa kukatwa mwili wake na kiwiliwili chake, kutenganishwa na kichwa na kitu chenye ncha kali.
Mlinzi ambaye alikuwa ameajiriwa na marehemu anadaiwa kumuua mwajiri wake huyo kwa kumchinja na kiwiliwili chake kutenganishwa na shingo yake. Anatuhumiwa kutenda ukatili huo, baada ya bosi wake huyo kushindwa kumlipa mshahara wa miezi sita unaofikia Sh 360,000.
Baada ya kumuua, mwili wake ulifukiwa katika shimo lililochimbwa shambani mwake katika Kijiji cha Kaondo Manispaa ya Sumbawanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masonje alithibitisha matukio hayo. Alisema kwamba mauaji ya kikatili ya Mwangalaba, yanadaiwa kufanyika saa 3:00 asubuhi Januari 17, mwaka huu shambani mwake kijijini Kanondo.
Mwili wa marehemu ulibainika ukiwa umeviringishwa katika mfuko wa sandarusi, ukiwa umefukiwa katika shimo lililo ndani ya uzio wa shamba hilo. Baada ya kuchunguzwa, mwili ulibainika kuwa na majeraha ya kukatwa na kitu chenye ncha kali. Shingo, miguu na kiwiliwili vilikuwa vimetenganishwa.
Mwili wa marehemu uligundulika majira ya saa 11:30 jioni, baada ya ndugu wa marehemu kulitilia shaka shimo ambalo lilikuwa limefukiwa; “Mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.
Comments
Post a Comment