Yanga Yataja Hatma ya Sadney, Lamine na Madeni Yake


Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla.
MWENYEKI wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla, leo Desemba 10, 2019 amezungumzia tetesi za klabu hiyo kutowalipa mishahara wachezaji kwa muda wa miezi miwili na akaweka wazi hatma ya wachezaji Sadney Urikhob na Lamine Moro ambao inasemekana waliandika barua za kutaka kuondoka katika klabu hiyo kwa kutolipwa mishahara yao kwa miezi mitatu.

Akiongea na wanahabari alisema ni kweli klabu yake haijawalipa wachezaji mishahara ya miezi miwili ambayo ni Oktoba na Novemba mwaka huu na kwamba iwapo mambo yakienda vizuri watalipwa leo.

Aliongeza kwamba habari zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mshambuliaji Sadney Urikhob na beki  Moro Lamine, viongozi wamekubaliana kuachana na Sadney na watabakia na Lamine ambaye atalipwa mishahara yake.

Akifafanua hali ilivyo klabuni hapo, amesema walipoingia madarakani mwezi Mei 2019 walikuta madeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na kudaiwa Sh. milioni 800 na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).

Miongoni mwa madani hayo, alisema,  ni pesa za usajili kwa muda wa miaka miwili iliyopita ambazo ni Sh. mil. 250, pamoja na malipo ya makocha walioondoka, ambao ni  Hans Van Der Plujm na George Lwandamina.  Pia wamo  wachezaji Obrey Chirwa, Youthe Rostand na Donald Ngoma.

Kwa upande wa mapato ya klabu, alisema ni kutoka KCB, Vodacom, SportPesa, viingilio na haki za matangazo ya  televisheni ambapo wameingiza Sh. bilioni 2 wakati matumizi yamefikia Sh. bilioni 4.
video source: GP


Comments

Popular posts from this blog