Posts

Prince William, Kukutana na Rais Magufuli

Image
Mwanamfalme William wa Uingereza Mwanamfalme  (Prince) William wa Uingereza anapangiwa kukutana na Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli wiki ijayo wakati wa ziara yake ya siku saba Afrika. Anatarajiwa kuzuru pia Kenya na Namibia katika ziara hiyo ambayo si ya kikazi. Ziara hiyo itafanyika kuanzia 24 Septemba hadi 30 Septemba. Lengo kuu litakuwa kufuatilia juhudi za kukabiliana na ujangili na uhifadhi wa wanyama. Atafanya ziara hiyo katika wadhifa wake kama rais wa mashirika yanayotetea uhifadhi wa wanyama ya United for Wildlife na Tusk Trust. Amekuwa pia mlezi wa shirika la Royal African Society linalolenga kukuza uhusiano kati ya Afrika na Uingereza na hushiriki sana juhudi za kukabiliana na ujangili. Akiwa ziarani Tanzania, atafanya mashauriano na Rais Magufuli kuhusu juhudi zinazopigwa na taifa hilo katika kukabiliana na ujangili kwa mujibu wa shirika la habari la Press Association. Kadhalika, atazuru bandari ya Dar es Salaam kujifahamisha zaidi kuhusu ju...

Tamko la Masoud Djuma kuhusiana na kuzikosa safari mbili

Image
Baada ya kuzikosa safari mbili za Klabu ya Simba kuelekea Mkoani, Kocha Msaidizi wa timu hiyo Masoud Djuma,  amesema kuwa amebakia Dar es Salaam kwa majukumu makubwa mawili. Taarifa imeeleza kuwa Djumma amesema hakuweza kuambatana na Kikosi cha Simba kuelekea Mtwara pamoja na Mwanza kutokana na kupewa majukumu na Kocha Mkuu, Patrick Aussems ya kuwasoma Yanga wakicheza Taifa. Djuma alihudhuria mechi ya Yanga jana dhidi ya Coastal Union ili kujua timu hiyo mbinu inazozitumia kuelekea mechi yao ya watani wa jadi Septemba 30 2018. Mbali na kuwapigia chapuo Yanga, Djuma amesema amesalia Dar es Salaam kuendelea kuwanoa wachezaji ambao hawasafiri na kikosi kwenda Mwanza kucheza na Mbao ili kuwaweka fiti zaidi. Juuko Murushid pamoja na Haruna Niyonzima, ni baadhi ya wachezaji ambao wapo kwenye program hiyo chini ya Djuma wakijifua kurejesha makali yao baada ya kutokuwa na timu kwa muda mrefu.

Dogo Janja, Uwoya wamwagana rasmi? Madee atoa majibu

Image
Kufuatia kusambaa kwa taarifa za kumwagana chini kwa wanandoa mastaa, Dogo Janja na Irene Uwoya, Baba wa muziki wa Janjaro, Madee amekanusha tetesi hizo akiziita ni uvumi na kwamba wawili wao hawana tatizo lolote. Stori za mastaa hao kumwaga zimezidi kuenea zaidi siku za hivi karibuni zikichagizwa na kitendo cha Uwoya kutoonekana Hospitalini alipokuwa amelazwa Janjaro ambaye anaumwa. " Hakuna taarifa kama hizo, Janja na Uwoya wapo kama kawaida hawajatemana kama ambavyo inaenezwa, hizo ni tetesi tu au niite ni uzushi, nachokuambia wale bado ni mtu na mke wake hizo stori za kuachana mnazipika nyie," amesema Madee. Lakini leo Uwoya alizidisha kasi ya watu kuamini kuwa hakuna ndoa baina ya wawili hao baada ya kujibu comment ya shabiki wake kwenye Instagram aliyeandika, " Dogo Janja atakufa Irene" kisha Uwoya kujibu, " hapana, simlisema wenyewe nitafute wa umri wangu yeye bado mdogo? sasa nimefuata ushauri jamani...au kashakua?"  Masta...

Mwili wa Dk Misanya Bingi waagwa Dar, kuzikwa Dodoma

Image
MWILI wa aliyekuwa mtangazaji mahiri nchini na Mhadhiri wa Shule ya Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) iliyo chini ya Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Misanya Bingi (47) umeagwa leo katika Kanisa Katoliki la Makongo Juu liliopo Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea Mjini Dodoma kwa ajili ya mazishi siku ya kesho. Dkt Misanya Bingi alifariki dunia siku Jumapili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na wakati wa uhai wake alifanya kazi kwenye kituo cha Radio One ambapo alitangaza vipindi mbalimbali kikiwemo kipindi cha Chemsha Bongo siku za Jumanne na Ijuma saa tatu usiku. Hadi umauti unamkuta alikuwa akifundisha SJMC, tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. na kabla ya hapo Misanya Bingi alikuwa mtangazaji kwenye kituo cha Radio One kazi aliyoanza kuifanya mwaka 1996.

Tazama ‘FLYOVER’ Inavyofanya Kazi TAZARA

Image
Septemba 15, 2018 daraja la juu ‘flyover’ lililopo katika makutano ya Tazara lilifunguliwa na magari yakaanza kupita na uzinduzi rasmi unategemea kufanywa na Rais Magufuli mwezi ujao. Mradi huu ambao ni wa thamani ya Sh bilioni 95 unatekelezwa na kampuni ya Oriental Consultans Global na Eight Japan Engineering Consultants, zote za Japan. Rais John Magufuli alizindua ujenzi wa ‘flyover’ hii Aprili, 2016 na kueleza kuwa lengo ni kupunguza kero ya foleni jijini Dar es Salaam pindi itakapomalizika na kuanza kutumika. GLOBAL TV imefunga safari mpaka maeneo ya Tazara jijini Dar es Salaam kushuhudia ile barabara ya juu (FLYOVER) iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na Watanzania ambao hivi sasa imesaidia kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa. Baada ya kufika eneo la Tazara na kuona uzuri wa barabara hiyo na jinsi ambavyo magari yanapita, tukaamua kukielekeza kipaza sauti chetu na Wananchi wanaoishi kandokando ya barabara hiyo na kuwasikiliza wanalipi la kusema mara ba...

Faida tatu za kusamehe

Image
Katika tafiti ambazo zimewahi kufanywa na wanasaikolojia miaka ya nyuma, waligundua ya kwamba watu wengi hawana maendeleo yao binafsi kwa sababu hawatambui nguvu ya msamahama iliyovyo na nguvu katika safari ya Mafanikio. Tafiti hizo hizo zinaendelea kusema watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wamebeba mizigo mizito ndani nafsi zao. Mizigo hiyo mizito ambayo inawezekana kuna mtu alisabibisha mtu kuwa katika hali hiyo. Kwa mfano inawekana kuna ndugu,rafiki, mzazi aliwahi kufanya au kukutamkia maneno mazito ambayo yanakufanya Leo, kesho mpaka kesho kutwa usiwe kuyasahau. Maneno au vitendo hivyo vimekusababisha kwa kiasi kikubwa hupunguza hamasa za kiutendaji, magonjwa na mawazo mengi (stress). Hebu tuangalie japo kwa uchache ni kwa kiasi gani madhara ya kutokusamehe yanavyoweza kukuathiri. Msipo msamehe mtu kunakupekea kwa kiwango kikubwa kuweza kupunguza uwezo wa kufikiri vitu vipya, hata hivyo pamoja na kupunguza uwezo wa kufikiri kunakupelekea kuzama kati...

MAGAZETI YA LEO 19/9/2018

Image

Wassira Ateuliwa Mwenyekiti Bodi Kumbukumbu ya Nyerere

Image
Stephen Wassira. RAIS John Magufuli amemteua Stephen Wassira kuwa Mweyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,  nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Prof. Mark Mwandosya. You May Like

Manji kuisuka Yanga upya

Image
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Matawi ya Yanga Dar es Salaam, Boas Ikupilika, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji amewaahidi kuisuka Yanga mpya kwenye dirisha dogo la Novemba. Manji pia ameahidi kumpa sapoti kubwa Kocha Mwinyi Za­hera kuhakikisha sifa ya Yanga inarejea kwani amewakubali wachezaji baada ya kuwaona kwenye Uwanja wa Taifa hivi ka­ribuni alipokwenda kuwaangalia. Usajili wa dirisha dogo umepangwa kuanzia Novemba 15 hadi Desemba 15, mwaka huu ambapo timu hupata nafasi ya kuongeza wachezaji wach­ache kulingana na upungufu wao. Ikupilika amethibitisha kuwa Manji amekuwa akihusika katika mambo mbalimbali ndani ya klabu, amemuahidi Zahera kuwa, atamsaidia kutimiza ma­hitaji yake kwa kufanya usajili wa wachezaji ambao atahitaji kwenye dirisha dogo. “Manji aliomba muda kidogo kabla ya kurejea rasmi wakati wowote, lakini kuna baadhi ya majukumu ambayo amekuwa ak­itekeleza kama kiongozi wetu. Amekuwa akishauri mambo mengi kuhusu timu yetu,” alidokeza kion­go...

Utapeli mkubwa waibuka 40 ya Mzee Majuto

Image
AMA KWELI kufa kufaana! Hayo ndiyo maneno unayoweza kusema endapo yatakufikia madai ya utapeli mzito unaofanywa na baadhi ya watu wakiwemo wasanii wa kuchangisha pesa kinyume na taratibu wakidai eti ni kwa ajili ya kufanikisha 40 ya marehemu Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni. Taarifa hiyo ya kushtua ilipenyezwa na mmoja wa wasanii wa komedi Bongo, Jabir Ally ‘Wajajo’ ambaye alidai kuwa, akiwa katika mishemishe zake Mitaa ya Kariakoo jijini Dar alikumbana na baadhi ya wafanyabiashara waliohoji juu ya uhalali wa watu hao kuchangisha michango ya 40 hiyo. Alisema: “Kuna jambo la kushangaza sana nimekutana nalo huku Kariakoo, kuna watu wanapita kwenye maduka na kuomba michango ya kufanikisha 40 ya Mzee Majuto, mimi sikuwa na taarifa ya utaratibu huo, nikahisi kuna utapeli unafanyika. “Lakini katika kufuatilia nikagundua yupo pia msanii aliyewahi kufanya kazi kwa karibu na Majuto, Bi Rehema, naye anapita kuomba michango, nilipomuuliz...

Rais Magufuli - Huyu ndiye Mkuu wa Mkoa kinara anayepiga kazi hana mfano

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtaja mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka, kuwa ndiye mkuu wa mkoa kinara anayepiga kazi na kwamba hana mfano licha ya kupuuzwa kabla  hajamteua. Hayo ameyasema leo mkoani Simiyu wakati akihutubia wananchi wa mkoa huo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni hii ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 7 katika mikoa ya kanda ya ziwa. Rais Magufuli ameeleza kuwa, wakati anajaribu kutafuta wakuu wa Wilaya na wakuu wa mikoa aliambiwa na vyombo vyake kuwa Mtaka hafai hata U-DC lakini yeye akaamua kumteua kuwa mkuu wa mkoa kwasababu anajua watu wazuri huwa wanapigwa vita sana. ''Nilipotaka kumteua niliuliza vyombo vyangu nikaambiwa hafai kabisa lakini nimeuliza ripoti ya Wakuu wa Mikoa wanaofanya kazi vizuri, wakaniletea Mtaka ndio namba moja na namba mbili ni yeye kwa kifupi hana mfano'', amesema. Aidha Rais Magufuli ambaye atakamilisha ziara yake katika mikoa hiyo siku ya ...

BAD NEWS: AJALI YA MAGARI MATANO MBEYA, WALIOFARIKI WAFIKA 15

Image
IDADI ya watu waliokufa katika Ajali ya lori iliyogonga Magari mengine manne kabla ya kupinduka na kuwaka moto kwenye mteremko mkali wa Iwalanje, eneo la Igawilo jijini Mbeya imefikia 15, baada ya majeruhi wengine wawili kufariki dunia wakati wakipewa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya. Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda, Dk. Petro Seme amesema kuwa majeruhi wengine 13 wanaendelea na matibabu hospitalini hapo na kati yao wawili hali zao ni mbaya. Ajali hiyo imetokea jana tarehe 07 Septemba, 2018 majira ya saa 10 jioni katika mteremko wa mlima wa Igawilo Jijini Mbeya baada ya Lori lililokuwa na shehena ya viazi, likitokea Tukuyu kwenda Mbeya Mjini kuyagonga magari matano likiwemo basi dogo lililokuwa na abiria.

Ugomvi wa DC na Mkuu wa Mkoa wamkera Rais Magufuli

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amekemea tabia ya wakuu wa wilaya na mikoa kugombana wakati wanapotumikia wananchi. Ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi wa wilaya ya Tarime mkoani Mara wakati wa ziara yake ya kikazi, ambapo kuna mgogoro mkubwa kati ya DC wa wilaya Glorius Luoga na mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Daud Ngicho na mkuu wa mkoa huo Adam Malima. Rais Dkt. Magufuli ameonyesha kukerwa na misiguano ya viongozi wa mkoa wa Mara unaofanya hata miradi mbalimbali ya maendeleo kukwama kufuatia DC Luoga na RC Malima kutofautiana. “Kwanini mnagombana, wewe DC uko chini ya RC Malima, umheshimu na si kugombana kila wakati mpaka shughuli za maendeleo zinakwama,”amesema JPM Hivi karibuni  Rais pia alikemea mgogoro kati ya mkuu wa wilaya ya Chemba na Naibu waziri wa Fedha, Dkt. Ashatu Kijaji na viongozi wa wilaya hiyo wakati wa kuzindua barabara inayounganisha Afrika.

Chozi la Mkurugenzi wilaya ya Serengeti lamuokoa kutumbuliwa na Mh. rais

Image
Mkurugenzi wilaya ya Serengeti bwana Juma Hamsini ameepuka rungu la Mh. rais Magufuli la kutumbuliwa baada ya mbunge wa wilaya hiyo kupitia chama cha Chadema bwana Marwa Ryoba kumtaka Rais kuchukua uamuzi wa kumuondoa mkurugenzi huyo. Bwana Marwa amedai kuwa mkurugenzi huyo ni mwizi sana ndio tatizo la wilaya hiyo kutoendelea mbunge huyo alisema:-“Mimi nakupenda Mh rais lakini kwa mkurugenzi huyu tuna mkurugenzi mwizi, naomba niseme ameenda WMA akawalaghai wakampa milioni ishirini akaenda akakutana na aliyekuwa rasi wa mkoa akampa rasi wa mkoa milioni tatu akarudi milioni kumi na sana akaweka mfukoni eti anaenda kumugawia mkuu wa wilaya hakuwagawia akaweka mfukoni mpaka leo,Takukuru mkoa wanajua wilaya wanajua” mbunge huyo aliongeza ” Mh. rais sio hilo tu juzi kwenye kamati ya bunge mkurugenzi huyu wamefukuzwa na kamati ya bunge kutokana na fedha za miradi ya maendelea ambazo hazionekani kwa mujibu wa taarifa za CAG kwenye vikao pia haji,kwahiyo mh;rais mimi sio kw...