Posts

MSIBA WA MASOGANGE WAZIMA NDOA YA ABDU KIBA

Image
MSIBA wa aliyekuwa video queen mkali Bongo, Agness Gerald ‘Masogange’ aliyefariki Ijumaa iliyopita, umezima tukio kubwa la kufunga ndoa la msanii wa Bongo Fleva, Abdul Kiba ambaye alioa jana alfajiri. Abdul Kiba ambaye amefunga ndoa siku tatu tu baada ya kaka yake, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ aliyemuoa Amina Khaleef huko Mombasa nchini Kenya. Msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake ya Jeraha alifunga ndoa hiyo jijini Dar, jana kwenye Msikiti wa Kichangani, Magomeni ambapo alimuoa mchumba wake wa muda mrefu, Luwada Hassan. Habari zilizolifikia Ijumaa Wikienda jana zilieleza kuwa, huenda Ali Kiba na Abdul Kiba wakafanya sherehe ya pamoja ya harusi Aprili 29, mwaka huu kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar ili kufurahi na watu wao wa karibu kufuatia zoezi la wao kufunga ndoa. Taarifa zilieleza kuwa, baada ya Ali Kiba na Abdul Kiba kuoa, dada yao, Zabibu Kiba, naye anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na beki za zamani wa Timu ya Simba ambaye kwa sasa an

RC GAMBO AONGOZA MAZISHI YA LEYLA ARUSHA

Image
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo , leo ameongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Leyla aliyeuawa na mumewe kwa kuchomwa visu na mumewe huko Uingereza wiki kadhaa zilizopita. Mazishi hayo yamefanyika katika makaburi ya Sinoni jijini Arusha. Kaburi la marehemu Leyla likiwekwa sawa baada ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Sinoni jijini Arusha leo. Mwili wa marehemu Leyla aliyeuawa na mumewe kwa kuchomwa visu na mumewe huko Uingereza wiki kadhaa zilizopita ukipelekwa makaburini. Mazishi yakiendelea. (Habari na Korumba Moshi, Arusha)

Mke mtarajiwa wa Jacob Zuma ajiuzulu kazi Afrika Kusini

Image
Mwanamke ambaye anatarajiwa kuwa mke wa saba wa aliyekuwa rais wa Afrika kusini,Jacob Zuma, Nonkanyiso Conco amejiuzulu kazi nchini Afrika Kusini. Jumamosi iliyopita Nonkanyiso (24) ambaye hivi karibuni alizaa mtoto wa kwanza na Zuma, alitangaza kujiuzulu mpaka ifikapo Jumatatu ya April 23. Conco analazimika kujiuzulu cheo chake akiwa ni afisa mawasiliano wa kampeni ya kukabaliana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa wanawake wadogo, unyanyasaji wa kijinsia na ujauzito kwa watoto wadogo. Leonora Mathe ambaye ni naibu mwenyekiti wa shirika hilo, amethibitisha kuwa Conco ameandika barua hiyo. Hata hivyo mpaka sasa hajazungumza chochote juu ya uhuma hizo za kuhusishwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Zuma. Wakati huo huo mrembo huyo anafanya kazi nyingine kwenye asasi inayohamasisha kampeni ya kuwawezesha mabinti wadogo katika maisha yao ya kila siku na kuacha kuwategemea wanaume wenye umri mkubwa. Taarifa za Jacob Zuma na Nonkanyiso Conco kuwa na mahusian

MZEE GELARD: AGNESS ALINIAGA KABLA HAJAFA, NIKALIA!

Image
MZEE Gerald Waya, ambaye ni baba mzazi wa aliyekuwa Msanii wa Bongo Movies na Model, Agness Gerald ‘Masogange’, amesema mwanaye alikuwa nguzo kubwa katika maisha yake, hivyo kifo chake ni pigo kubwa kwake na familia nzima. Akizungumza nyumbani kwake, Mbalizi wilayani Mbeya, Mzee Waya alisema Masogange ni mtoto wake wa nne katika familia ya watoto sita, wa kike wakiwa ni watano ambapo ameeleza kwamba Masogange alisoma Shule ya Msingi Utengule iliyopo Mbalizi na Sekondari ya Sangu ambapo alikomea kidato cha pili baada ya kupata matatizo. Aliishia kidato cha pili akapata matatizo, hivyo ilibidi aache shule. Tulikosana kidogo lakini tukayamaliza yeye akaenda Dar es Salaam. Agness amekuwa nguzo kwangu, alikarabati nyumba hii ninayoishi kwa sasa na nilikuwa nafarijika sana nikimuona, lakini leo kusikia msiba huu kwa kweli inaniuma sana,” alisema Mzee Waya. Alinipigia simu tukaongea naye akaniambia ‘mimi baba ninaumwa’, nikamuuliza nini tatizo akasema, ‘baba nio

Nafasi za Kazi TANROADS Tanzania

Image
Regional Manager, TANROADS – MOROGORO is looking for suitable qualified Tanzanian candidates for available Posts at Morogoro Weigh Bridge stations. Applications are invited from suitable qualified and competent Tanzanians to apply for the following position: POSITION TITLE: DRIVER (1 POST) A: KEY QUALIFICATION: 1. Holders of Form IV Certificate; 2. Holder of valid Class E driving license 3. Having driving experience of at least five (3) years 4. Must be fluent in both written and spoken English and Swahili languages 5. Age. Not above 35 years of age 6. Must be Tanzanian citizen. B: DUTIES AND RESPONSIBILITIES: 1. Driving Agency’s vehicle in urban and remote areas. 2. Maintaining the vehicle logbook and all accidents records pertaining to the assigned vehicle 3. Keeping the vehicle in good working order and clean condition 4. Reporting repairs or maintenance needs of the vehicle to the Shift In-charge timely 5. Observe good customer care, dignity and integ

Nafasi za Kazi NMB

Image
Senior Manager; Digital Lab Job Purpose The incumbent will be responsible to foster research, testing, and incubating of concepts, products and processes by leveraging on technology to deliver digital products which capture value, enhanced experience and capabilities to our customers. Main Responsibilities: Create, evolve, and scale a new method of delivering digital solutions, adopting a lean, fail fast delivery methodology based on Agile principles. Play a key role of a change agent responsible to influence peers, leaders within the bank to align, adapt to and use these new methodologies/technologies. Innovate from prototyping to testing with an eye towards encouraging speed to market in a dynamic and ever changing environment. Create a digital lab which will facilitate nurturing of new ideas into finalized solutions by establishing and drive the technical execution of the digital products. Create processes in the lab that are rooted in best practices for con

Mazoezi ya Polisi Moshi Mjini Yazua Taharuki

Image
Leo shughuli zimesimama kwa muda katika Mji wa Moshi wakati Vikosi vya Jeshi la Polisi vikipita katika maeneo mbalimbali ya mji huo wakiwa na silaha za moto na kuzua hali ya taharuki kwa baadhi ya wakazi wa Moshi.    

Afande adakwa kwa tuhuma za rushwa

Image
MAMLAKA ya Kuzuia Rushwa na Kuhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) inamshikilia ofisa wa jeshi la polisi kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh. 250,000. Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Uhusiano wa ZAECA, Mwanaidi Suleiman Ally, alisema ofisa huyo Rajabu Juma Simba, mkazi wa Meli Nne-uzi, kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh. 250,000  kutoka kwa vijana wawili ambao majina  yao yamehifadhiwa. Alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 4.30 asubuhi nje ya kituo cha polisi cha Mwanakwerekwe, baada ya kuwakamata na chombo walichokuwa nacho aina ya Pasola, kwa kuwatuhumu wanaenda kununua dawa za kulevya aina ya bangi. Alidai baada ya kuwapekua hakuwakuta nazo na kuwaamuru kwenda nao kituo cha polisi Mwanakwerekwe kwa mahojiano zaidi. Alisema mara baada ya mahojiano, ofisa huyo aliwaamuru vijana hao wampatie Sh. laki mbili ili awaachie na chombo chao, vijana hao walimpatia shilingi laki moja na baadae kuwachiwa wao na kuendele

Yafahamu matatizo ya ngozi yanayotokana na kunyoa ndevu na nywele na jinsi ya kujitibu

Image
Wakati unaponyoa ndevu na nywele, baada ya kunyoa, wakati wa kuota nywele hizo zipo baadhi ya sehemu nywele hushindwa kutoka nje ya ngozi na kuota ndani ya ngozi hali inayopelekea kusababisha uvimbe na vipele. Zipo aina mbili za mapele yanayotokana na Kunyoa nywele na ndevu. Magonjwa haya ni kama ifatavyo 1. Acne Keloidalis Nuchae Acne keloidalis nuchae (AKN) Ni tatizo linalotakana na maambukizi ya bacteria P.Acnes kwenye ngozi baada ya kunyoa,hali inayopeleka vijitundu vya vinyweleo kuziba na kufanya nywele kushindwa kutoka nje ya ngozi na kukulia ndani ya ngozi hivo kusababisha mapele makubwa na makovu. Acne keloidalis nuchae (AKN) mara nyingi hutokea sehemu ya kisogo. Mbali na kunyoa tatizo hili pia huweza kusababishwa na uvaaji wa kofia. 2.Pseudofolliculitis barbae (PFB) Tatizo hili huwapata watu wengi, hili hutokea sehemu za kidevu na mashavu. Hii pia husababishwa na kuziba kwa vinyweleo vya ngozi baada ya kunyoa hivo kupelekea ndevu kukulia ndani ya ngozi na kus

Zari Amlilia Masogange, Akumbuka SMS Zake

Image
Video vixen, Agness Gerald ‘Masogange’ enzi za uhai wake. MPENZI wa zamani wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha video vixen, Agness Gerald ‘Masogange’, kupitia akaunti yake ya Snapchat. Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Zari ameeleza kuwa Masogange alikuwa akimtafuta kupitia simu kila mwezi akimuulizia maendeleo ya watoto wake ingawa hawakuwa marafiki sana. Kupitia Mtandao wa Snapchat Zari ameandika; We were not friends as such but ever since you got my number you’ve been dropping me a text every month and i mean no month passed without you asking how are the kids. in peace sis.

Kipimo Cha Mimba Cha Nyumbani rahisi Kutumia

Image
       Kipimo cha mimba cha nyumbani ni rahisi sana kukitumia wewe mwenyewe kwa wakati wako ikiwa unajihisi umjamzito au kuhisi mwenzi wako ana ujauzito. Unachotakiwa kuwa nacho ni moja, Kipimo hichob‘Pregnancy Test’ ambacho kinapatikana katika maduka yote ya madawa ya Binadamu, na pili mkojo wa anahisiwa au kuhisi ana mimba. mara nyingi ni rahisi zaidi kupata majibu ya uhakika ukitumia mkojo wa kwanza kabisa asubuhi kisha uweka kwenye kikopo kidogo na kisha fuata maelekezo ya kwenye picha hii:- Hatua; 1.    Fungua pakiti iliyo na kipimo cha mimba. 2.    Tofautisha sehemu ya kushika na sehemu utakayotumbukiza kwenye kikopo chenye mkojo. 3.    Acha kwa dakika zipatazo 3, bila kuzidisha sehemu yenye mstari uliyoandikwa MAX. 4.     Toa na kisha soma majibu yaliotokea. Majibu yatatoka kama ilivyo katika picha hii inayofuata ya vipimo viwili tofauti vilivyofanyiwa majaribio:- 1.    Mistari miwili humaanisha ‘POSTIVE’ – Mimba imetunga.

Siri 6 Kiba Kumuoa Mkenya Zaanikwa!

Image
Ali Saleh Kiba ‘King Kiba akiwa na Mkewe Amina N YUMA ya tukio kubwa na la kihistoria kwenye ulimwengu wa burudani, lililogubikwa na kufuru ya fedha la staa wa Bongo Fleva wa Afrika Mashariki, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ kumuoa mrembo mkali kutoka Mombasa nchini Kenya, kuna siri sita (6), Risasi Jumamosi linazianika.  Juzi alfajiri ya Aprili 19, mwaka huu, Kiba alifunga ndoa na mrembo Amina Khaleef katika Msikiti wa Ummul Kulthum uliopo mjini Mombasa, Kenya. Ndoa hiyo ilifungishwa na Sheikh Mohamed Kagera. Hakika ilikuwa ni furaha, shangwe, nderemo na vifijo kwa maharusi hao, wanafamilia na mashabiki wa Kiba mjini Mombasa mara baada ya ndoa hiyo kufungwa. Mara baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo, mitandaoni kulichafuka ambapo baadhi ya mashabiki wa Kiba walikuwa wakihoji ni kwa nini mkali huyo wa Wimbo wa Seduce Me ameacha warembo kibao Bongo na kwenda kwa Amina wa Mombasa? Kufuatia wengi kutaka kujua Amina ni nani au ana nini cha tofauti kilichomteka Kiba, R

Kajala amkimbiza mke wa P Funk

Image
   Muigizaji wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja amedaiwa kusababisha mke wa prodyuza mahiri Bongo, Paul Matthysse, Samira afungashe virago vyake tayari kwa kurudi kwao. Mke huyo wa P Funk amedaiwa kufikia uamuzi huo baada ya mwanaume huyo kuonekana kurudisha majeshi kiaina kwa Kajala aliyewahi kuwa mchumba’ke zamani huku picha na video mbalimbali za kimalovee zikivuja. Mtu wa karibu na mke wa P Funk alivujisha kuwa, Samira amefikia hatua hiyo baada ya kushuhudia matukio mbalimbali ya P Funk na Kajala na kukosa majibu yaliyonyooka. “Unajua P Funk kila alipokuwa akielezwa kuhusu Kajala alikuwa hanyooshi maelezo ingawa machoni alionesha kumpenda Kajala. “Mkewe ambaye kwa sasa ni mjamzito, ameishi kwenye kipindi kigumu sana. Anashindwa kumuelewa P Funk kwani watu kibao wanampigia na kumuambia wamemuona mumewe akiwa na Kajala,” alidai mtu huyo wa karibu. Akizidi kushusha data, mtu huyo wa karibu na Samira alidai kuwa, mara kadhaa P Funk amekuwa akielezwa kuh

TCRA Yaanza Rasmi Usajili wa Blogu, Redio na TV za Mtandaoni

Image
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetangaza kuanza rasmi zoezi la usajili wa wamiliki wa Blogu, Majukwaa ya Mtandaoni (Online Forums), Redio pamoja na Televisheni za mtandaoni kuanzia leo Jumamosi, Aprili 21, 2018 kwa mujibu wa sheria.

Masogange kuagwa Leaders, kuzikwa nyumbani kwa.

Image
Video queen maarufu Bongo Agnes Gerald maarufu Kama Masogange anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwao jijini Mbeya ambako ndiko wazazi wake waliko. Akizungumza na www.eatv.tv dada wa Agnes anayejulikana kama Emma Gerald, amesema mwili wa Agnes  utaagwa jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Leaders,  na kisha kusafirishwa kuelekea mkoani Mbeya kwa mazishi “Tutaaga kesho asubuhi saa 3 pale Leaders, na kisha tutasafirisha kuelekea Mbeya kwa mazishi”, amesema Emma Gerald. Sambamba na  hilo muigizaji Steve Nyerere ambaye yuko karibu na familia ya Agnes amewataka wasanii kujitokeza kwa wingi leaders jioni ya leo, ili kujadili utaratibu wa mazishi na mengineyo. Agnes Masogange amefariki jana April 20, kwenye hospitali ya Mama Ngoma baada ya kulazwa kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta kwa tatizo la pneumonia

NDOA YA KIBA YAACHA VILIO!

Image
DAR ES SALAAM: Wakati mkali wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘AliKiba’ akitarajiwa kuangusha bonge la sherehe baada ya kufunga ndoa nchini Kenya, ndoa hiyo imedaiwa kuacha vilio vikali kwa wanawake ambao waliwahi kushea kitanda na msanii huyo, Ijumaa lina mchapo kamili. Kiba alitarajiwa kufunga ndoa hiyo jana mjini Mombasa nchini Kenya kisha kufuatiwa na bonge la sherehe mjini humo huku sherehe nyingine bab’kubwa ikitarajiwa kufanyika nchini mwishoni mwa mwezi huu. MTU WA KIBA ANENA Mtu wa karibu na AliKiba, amepenyeza habari kuwa, licha ya kwamba wao wanasherehekea harusi ya mkali huyo anayetamba na Wimbo wa Seduce Me, nyuma yake kuna vilio vingi kutoka kwa wanawake ambao walitembea na Kiba kabla. “Kama unavyojua Kiba alishazaa watoto wanne, wale watoto kila mmoja ana mama yake. Sasa mama zao wanalia maana nao walikuwa wana matarajio ya kuolewa,” alisema mtu huyo wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina na kuongeza: BIBI HARUSI NJIA PANDA “Kimsingi wamem

Wenger Aondoka Rasmi Arsenal

Image
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ameridhia kubwaga manyanga mwishoni mwa msimu huu baada ya majadiliano ya kina na uongozi wa klabu hiyo kongwe duniani. “Baada ya kutafakari kwa kina kufuatia mazungumzo na klabu yangu, u mefika wakati sasa nikae pembeni mwisho wa msimu huu, nina furaha sana kwa muda wote niliokaa hapa klabuni. “Ninawashukuru wafanyakazi wenzangu, wachezaji, wakurugenzi na mashabiki kwa kuifanya klabu hii kuwa spesho, nimeitumikia kwa miaka mingi” amesema Wenger kwenye taarifa yake rasmi leo Ijumaa. LONDON, England.