Kipimo Cha Mimba Cha Nyumbani rahisi Kutumia
Unachotakiwa kuwa nacho ni moja, Kipimo hichob‘Pregnancy Test’
ambacho kinapatikana katika maduka yote ya madawa ya Binadamu, na pili
mkojo wa anahisiwa au kuhisi ana mimba.
mara nyingi ni rahisi zaidi kupata
majibu ya uhakika ukitumia mkojo wa kwanza kabisa asubuhi kisha uweka kwenye
kikopo kidogo na kisha fuata maelekezo ya kwenye picha hii:-
Hatua;
1.
Fungua pakiti iliyo na
kipimo cha mimba.
2.
Tofautisha sehemu ya
kushika na sehemu utakayotumbukiza kwenye kikopo chenye mkojo.
3.
Acha kwa dakika zipatazo
3, bila kuzidisha sehemu yenye mstari uliyoandikwa MAX.
4.
Toa na kisha soma
majibu yaliotokea.
Majibu yatatoka kama
ilivyo katika picha hii inayofuata ya vipimo viwili tofauti vilivyofanyiwa
majaribio:-
1.
Mistari miwili humaanisha
‘POSTIVE’ – Mimba imetunga.
2.
Mistari mmoja humaanisha
‘NEGATIVE’ – Mimba haikutunga.
Muonekano wa nje wa
Kipimo cha Mimba kwa kutumia mkojo kinachopatikana kwa wingi katika maduka ya
madawa mengi.
Ikiwa hujaamini matokeo
yaliyotoka unashauriwa uende Hospitali kwa majibu kamili na sahihi kutoka kwa
Daktari.
Comments
Post a Comment