“Kuna kitu MUNGU anataka kutuambia kupitia Waraka wa Maaskofu” Askofu Shoo
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli, Askofu Frederck Shoo amewata baadhi ya watu kuacha kupotosha ukweli wa waraka wa maaskofu kwa kuupaka matope na kusema anae fanya hivyo ni mjinga. Askofu Shoo ametoa kauli hiyo leo April 1, 2018 katika Usharika wa Moshi Mjini Dayosisi ya kaskazini, mkoani Kilimanjaro wakati akitoa salamu za Pasaka. Askofu Shoo amenukuliwa akisema “Wapo wanaotumia nguvu nyingi kutaka kupotosha ujumbe wa waraka wa Maaskofu na wamekuwa wakilipaka Kanisa matope ili waweze kurejea katika waraka ule, watu hawa naweza kuwaita ni wajinga lakini pamoja na hilo nataka wakayatafakari na kama wanaona kuna hatua za kuchukua wachukue.” “Kanisa limekuwa linapata kejeli za aina mbalimbali kutoka kwa watu hao na kuwatuhumu kuwa maskofu walifikia maamuzi ya kuandika waraka huo kutokana na sababu za kimaslahi kwa maana ya sadaka makanisani kupungua jambo ambalo si la kweli.” -As