Posts

Mpenzi wa Cristiano Ronaldo ametumia Kiswahili leo

Image
Lugha ya Kiswahili inaonekana kuzidi kukuwa na kuwavutia watu mbalimbali dunia kuitumia, leo April 1 2018 moja kati ya post za mitandao ya kijamii zilizochukua headlines ni post ya mwanamitindo  Georgina Rodríguez ambaye ni mpenzi wa staa wa soka wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Georgina Rodríguez ni mwanamitindo na ndio mpenzi wa sasa wa Ronaldo na wamefanikiwa kupata mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Alana Martina , hivyo katika insta story yake amepost picha yake na Ronaldo na kuandika ‘Hakuna Matata’ Msemo wa hakuna matata ni msemo wa Kiswahil i ambao umeonekana kupendwa na umekuwa msemo maarufu sana kwa wageni wanaopenda kujua lugha ya Kiswahili, huo huwa ni msemo wao wa kwanza kujifunza lakini haijajulkana bado  Georgina Rodríguez ameujulia wapi msemo huo.

PRETTY KIND AWAIBUA WABONGO TENA,KISA MABADILIKOYA AJABU

Image
Mrembo Suzan Michael ‘Pretty Kind’ aliyekuwa Bingwa wa picha za utupu mtandaoni ameonesha kubadilika kitabia hasa katika mitandao ya kijamii na hilo limeonekana baada ya kuanza kuutumia mtandao wake wa kiijamii wa Instagram. _ Ikiwa ni siku chache za msanii huyo kuwa huru baada ya kusamehewa kwa adhabu yake ya kifungo cha kutojihusisha na masuala ya muziki kwa muda wa miezi sita kutokana na hatua za Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo dhidi ya kukiuka maadili kupitia Naibu wa wizara hiyo Mhe. Juliana Shonza mwezi Januari mwaka huu.   Hizi ni picha baadhi za Msanii huyo ambazo anaonekana kubeba kitabu kitakatifu ‘Biblia’ na kuandika kuwa Mwenyezi Mungu kwa sasa anaweka sawa mambo ya kila kilichotoka katika mstari wake.

Rais Magufuli Aungana na Wakristo Kuadhimisha Misa ya Pasaka Kanisa la Mt. Joseph Dar

Image
Rais Magufuli leo ameungana na Wakristo wote Tanzania katika maadhimisho ya Misa Takatifu ya sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakilakiwa kwa furaha na Paroko Msaidizi Venance Tegete walipojumuika na waumini wengine katika Maadhimisho ya Misa ya Sikukuu ya Pasaka katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Jumapili Aprili 1, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli na waumini wengine wakisikiliza kwa makini mahubiri ya Paroko Msaidizi Venance Tegete katika Maadhimisho ya Misa ya Ibada ya sikukuu ya Pasaka katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Jumapili Aprili 1, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa sadaka katika Maadhimis

Meli ya abiria ya Uingereza iliyozamishwa mwaka 1942 yaondolewa baharini

Image
Meli ya abiria ya Uingereza iliyozamishwa wakati ilishambuliwa kwa bomu na ndege za Japan wakati wa vita vya pili vya dunia, imeinuliwa kutoka baharini pwani mwa Sri Lanka baada ya miaka 75. SS Sagain, ambayo abiria wake wengi na mizigo iliokolewa mwaka 1942, imeinuliwa na kundi la wapiga mbizi kutoka kwa jeshi la wanaji wa Sri Lanka, Ilikuwa karibu umbali wa futi 35 chini ya bahari katika bandari ya Trincomalee. Shughuli ya kuiinua meli hiyo ilichukua miezi kadhaa na ilifanywa na kikosi cha wanamaji cha Mashariki mwa Sri Lanka.

RAY C ATIBUKA VIBAYA,ATOA MANENO TATA KISA LADY JAY DEE,ASEMA BORA ATIWE MIMBA AZAE

Image
Muimbaji Ray C amefunguka mazito kwa kile anachoona kinaenda ndivyo sivyo katika muziki wa Bongo Flava kwa sasa. Ray C amefikia hata hatua ya kutumia maneno makali kueleza hisia zake kwa yale ambavyo hakubaliani nayo kwenye tasnia hiyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika; Kuna muda huwa nafikiria mambo mengi sana! kuna muda najiskia kuamua kutiwa mimba, nizae niwe tu mama wa nyumbani! maana kuna muda nikiangalia wasanii wenye maendeleo kwenye Bongo Flava ni wachache saaaaana! na sijiongelei mimi maana mimi mwenyewe kuna wakati nilivurunda mwenyewe! Nakubali nilibugi na nikagundua nimebugi haswa na ndio maana nimepambana mpaka hapa niliko baada ya kugundua baraka tele nilizozawadiwa na Mungu ni kubwa mno kuliko starehe za muda za ndogo na za kibwege!!! Ila huwa nakaa najiuliza miaka kama sita ambayo nilipotea kwenye industry! kuna wasanii nilianza nao na wana vipaji vya ajabu maskini lakini wengi wao wamezimwa kama taa!!! Namkumbuka Nature, Joseline, B

Halima Mdee Akamatwa na Polisi Akitokea Afrika Kusini

Image
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee. Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee. Mdee amekamatwa leo alfajiri uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini Afrika Kusini inakoelezwa alilazwa kwa matibabu. Meya wa Ubungo, Boniface Jacob amethibitisha kukamatwa kwa Halima Mdee ambapo amesema; “Ni kweli amekamatwa leo Saa 9 alfajiri Airport, akitokea Afrika Kusini alipokuwa amelazwa kwa matibabu na sasa yupo Central.” Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) huenda akaunganishwa na vigogo wengine sita akiwamo Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe katika kesi inayowakabili. Vigogo hao wengine tayari wamekwisha kupandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa mashtaka nane. Kukamatwa kwa Mdee kunafikisha watuhumiwa saba kati ya nane ambao wamekwisha kuhojiwa mwingine ambaye bado na huenda anatafutwa na jeshi hilo ni mbun

ZARI THE BOSS LADY AKINUKISHA KUTUA BONGO NA KUTOENDA MADALE.MAMA YAKE DIAMOND ATIBUKA

Image
DAR ES SALAA: Zarinah Hassan ‘Zari The Boss lady’, aliyekuwa baby mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu abdul ‘Diamond Platnumz’, amekinukisha ile mbaya baada ya kutua Bongo na kutokwenda nyumbani kwa jamaa huyo, Madale-Tegeta jijini Dar, risasi Jumamosi limenyetishiwa. ATUA USIKU WA MANANE, AFIKIA HOTELINI Zari alitua Dar usiku wa manane wa Jumanne iliyopita na kufikia katika Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro, zamani Kempinski iliyopo Posta, Dar na mapema kesho yake (Jumatano iliyopita), alisaini dili nono na Kampuni ya Softcare. Zari alisaini dili hilo la mamilioni, tukio lililofanyika mbele ya vyombo vya habari kwenye ukumbi wa hoteli hiyohiyo na sasa akawa ndiye balozi mkuu wa pampers za watoto zinazosambazwa na kampuni hiyo. Zari The Boss lady akiwa na Diamond. AULIZWA KUHUSU DIAMOND Katika zoezi hilo la kusaini dili hilo, ulipofika muda wa maswali, Zari aliulizwa juu ya uhusiano wake na Diamond ambapo ‘aliwaka’ na kusema kwamba, kilichomleta Bongo ni dili

Nafasi za Kazi 30 Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma

Image
Mkurugenzi  wa Halmashauri  ya Manispaa ya Dodoma , kupitia kibali cha Ajira anapenda kuwatangazia wananchi wote wa Tanzania wenye sifa za kuajiliwa katika Utumishi wa Umma kuleta maombi ya kazi kwa nafasi ya Mtendaji wa Kijiji kama ifuatavyo

Madhara ya kujichubua

Image
Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu.Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini ya kiwango, hii hupelekea watu hawa kutumia ving´arisha ngozi kama krimu, vidonge au nyenzo zingine kubadilisha ngozi zao.  Tafiti zinaonyesha kwamba wavulana na wasichana hupendelea kutumia bidhaa zinazong´arisha ngozi ili waweze kupata hadhi nzuri katika kundi la familia zao, na jamii. Kwa kweli,hata matangazo yanayoonyeshwa kwenye televisheni mbalimbali huonyesha kitu hiki. Mambo hayo yote huwa na athari kubwa juu ya mawazo ya vijana wa kiume na wakike ambayo hupelekea kuwafanya wachague chochote wanachomudu kati ya krimu au vidonge. Madhara ya kujichubua ni yapi? Mtu anaeyejichubua anaweza kupata kansa ya ngozi, chunusi, uvimbe katika ngozi, ngozi kuwa nyembamba,Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito,kutokwa na mabaka, pumu, kupata watoto wenye kasoro, kupata ma

MAGAZETI YA LEO 29/3/2018

Image

ANGALIA MAELFU WAMZIKA KIJANA ALIYEDAIWA KUUAWA KWA KIPIGO CHA POLISI

Image
Maelfu ya vijana mbeya wamemsindikiza kwenye makazi ya milele kijana Allen Mapunda (20) aliyekuwa mfanyabiashara wa machungwa mkoani Mbeya anayedaiwa kufariki muda mfupi baada ya kuachiwa na polisi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga amesema Jeshi hilo halihusiki kwa namna yoyote na kifo cha Allen ambaye anadaiwa alitoka rumande Machi 25, saa 4 asubuhi na ilipofika saa 12 alifariki dunia. Awali, Mkuu wa Mkoa Mbeya, Amos Makala alimuagiza RPC Mohamed Mpinga kuunda kikosi kazi kitakachochunguza tukio zima lilipolekea kifo cha Allen Mapunda. Amesema kikosi hiko kijumuishe wanafamilia na jamii ambayo inamfahamu Allen kisha kumkabidhi ripoti ili hatua zichukuliwe kwa mujibu wa sheria. Kijana Allen Mapunda ambaye alikuwa mkazi wa Kata ya Iyela, anadaiwa alifariki Machi 25, 2018 saa chache baada ya kuachiwa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi mkoani Mbeya alipokuwa amekamatwa na jeshi hilo.

NORAH: NAMZIMIA KWELI GABO!

Image
Nuru Nasoro ‘Norah’. MKONGWE wa sinema za Kibongo, Nuru Nasoro ‘Norah’ amesema kati ya waigizaji wa kiume anaowakubali kutoka Bongo Movies ni muigizaji Gabo Zigamba. Norah alifunguka hilo hivi karibuni alipokuwa akipiga stori mbili tatu na mwanahabari wetu ambapo alipoulizwa kuhusu listi ya wasanii wa kiume anaowakubali Bongo, moja kwa moja alianza kwa kumtaja Gabo. Gabo Zigamba. “Wapo wengi ninaowakubali na listi yangu inaongozwa na Gabo namzimia kweli. Wengine ninaowakubali ni JB, Frank Mwikongi, Chiki Mchoma na Dude,” alisema Norah. Alipoulizwa nini kinamvutia zaidi kwa waigizaji hao, alisema ni namna wanavyojua kubadilika kulingana na matakwa ya filamu husika.

Mahakama Yaamuru mmiliki wa IPTL Akatibiwe Muhimbili

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mmiliki wa IPTL, Harbinder  Sethi akatibiwe katika Hospital ya Taifa Muhimbili baada ya mshtakiwa huyo kulalamika afya yake imearibika sana. Mbali ya Sethi, mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara James Rugemarila ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60 na Bilioni 309. Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi leo March 28, 2018 kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na pia wanafatilia vielelezo vya upelelezi nje ya nchi. Baada ya kueleza hayo, Seth alisimama na kumueleza Hakimu Shaidi kuwa; 'Afya yangu imearibika sana, nahitaji kupelekwa hospitali.' Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Shaidi amesema ni dhahiri afya ya mshtakiwa ikiangaliwa hata kwa macho inaonekana ni dhahifu. “Naamuru mshtakiwa akatibiwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ili afya yake iwe njema,” amesema

BASATA Yakanusha Kuzifungulia Nyimbo Mbili za Diamond

Image
Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz. Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limesema nyimbo mbili za Diamond, hazijafunguliwa kama inavyodhaniwa. Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Godfrey Mngereza amesema nyimbo za Wakawaka na Hallelujah hazijafunguliwa na jambo hilo halina ukweli wowote na kuwataka wananchi kulipuuza. Kadhalika, Mngereza ametoa ufafanuzi kwa nini msanii Diamond amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na Naibu wake, Juliana Shonza na sio wasanii wengine. Mngereza ametoa ufafanuzi huo baada ya kusambaa kwa taarifa iliyoeleza msanii huyo kakutana na mawaziri hao. Baada ya taarifa hizo, kulizuka gumzo mitandaoni ambapo watu walihoji kwa nini wakutane na msanii huyo wakati kuna waliofungiwa nyimbo zao kama yeye na wengine kufungiwa kufanya muziki kwa miezi sita. Mngereza amesema hatua hiyo imetokana na majibizano yaliyokuwa yanaendelea kati ya Diamond na naibu waziri Shonza na ndio sababu iliyowafan

Vyakula vya Kukufanya Usizeeke

Image
KIINI CHA YAI L EO kwenye safu hii nitakuletea vyakula ambavyo ukila vitakufanya usizeeke kwani siku hizi watu wanazeeka haraka licha ya kuwa na umri mdogo.  Kama unataka kusafisha ubongo wako ambao huchoka mara kwa mara tumia kiini cha yai, kina wingi wa Klorine ambayo ni virutubisho muhimu vinavyowezesha ubongo kufanya kazi. COCOA Kama unafanya urembo wa ngozi hasa chini ya macho kwenye ngozi inayoweka weusi paka cocoa ina wingi wa vitamin itakayosaidia kulinda ngozi yako isizeeke. KAHAWA NA MAFUTA YA NAZI Kama unataka kuwa na nguvu kwa siku chukua kahawa yako iweke na vijiko viwili vya chai vya mafuta ya nazi kisha kunywa. Mafuta ya maboga kwa kuondoa msongo wa mawazo, Kama wewe ni mtu mwenye msongo wa mawazo mara kwa mara tumia mafuta ya maboga yana wingi wa asidi ya amino na glutamate ambayo yanasaidia ubongo kukaa sawa na wewe kujisikia vizuri. Mafuta haya ni mazuri kuyatumia hata kwa mtu mwenye mba kichwani ili kuzitibu yapake kwenye ngoz

JK' kuwa mgeni rasmi katika harambee

Image
RAIS mstaafu, Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee ya kukusanya fedha kiasi cha Sh. bilioni moja, kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Sekondari Lindi iliyoungua Julai 2016. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alisema harambee hiyo itafanyika kesho jijini Dar es Salaam. Zambi alisema maandalizi yote kwa ajili ya harambee hiyo yamekamilika na inatarajia kuhudhuriwa na wadau wa sekta ya elimu nchini. Alisema harambee hiyo imepanga kukusanya Sh. bilioni moja ikiwa ni karibu nusu ya mahitaji ya Sh. bilioni mbili zinazotakiwa kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo kongwe. “Kutokana na fedha tutakazokusanya, tumepanga ujenzi uanze wakati wowote. Zoezi hili litakwenda sambamba na mpango wa mkoa kuboresha mfumo mzima wa masuala ya elimu toka ngazi ya awali,” alisema Zambi. Mkuu wa mkoa huyo alikiri kuwa mkoa wake ni mmoja kati ya inayofanya vibaya kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa,

Rungwe aliomba Jeshi la Polisi kusaidia upatikanaji wa ndugu zake

Image
Mwanyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) Hashim Rungwe ameliomba jeshi la polisi kusaidia upatikanaji wa Mpwa wake Saida Hilal (40) na mumewe Abdallah Kutiku ambao hawajaonekana tangu Machi 26, 2018 majira ya asubuhi. Hashim Rungwe amesema hayo leo Machi 27, 2018 na kudai Saida Hilal aliaga wenzake ofisini na kwenda kituo cha polisi kufuatilia suala la mume wake Abdallah Kutiku ambaye alichukuliwa na polisi "Huyu binti alikuwa anafuatilia habari za mumewe polisi kwa kuwa mumewe alikuwa amekamatwa na polisi hivyo naye hapatikani kwa hiyo wote wawili hawaonekani kwani tulipofika kituo cha polisi walisema hawa watu hatuwafahamu na wala hawajafika pale, tangu hapo Bi. Saida Hilal hapatikani kwenye simu zake na tumefanya jitihada kumtafuta kwenye vituo vya polisi na mahospitali kama Muhimbili, Mwananyamala na sehemu zingine za usalama bila mafanikio" Rungwe aliendelea kuelezea kuwa "sehemu zote ambazo alikuwa anapenda kutembelea zote tumepita na

Linex azungumzia ishu ya kupotezwa na Ulevi

Image
Sunday Mangu ‘Linex’ MSANII wa Bongo Fleva, Sunday Mangu ‘Linex’, ameibuka na kufungukia tetesi zinazozagaa dhidi yake kuwa ulevi ndiyo umempoteza kimuziki na kusema siyo kweli bali wanaozungumza hivyo ni wabaya wake ambao hawana nia nzuri kwake. Akipiga stori na Risasi Vibes, Linex alisema kuwa muziki ni kama biashara nyingine na mtu anaweza kushuka na kupanda hivyo kilichompoteza ni changamoto za maisha kuwa nyingi na kushindwa kuzimudu ila anaamini atarejea tena na kuwa kama alivyokuwa zamani. “Wanaosema kwamba nimepotea kimuziki kisa ulevi hawana nia njema na mimi, mwanamuziki yeyote anaweza kupotea bila kujali umaarufu alionao, ndiyo maana hata Bill Gates leo anaweza kuwa namba moja kwenye listi ya matajiri duniani na baada ya muda hata kwenye kumi bora akawa hayumo tena,” alisema Linex. Linex azungumzia ishu ya kupotezwa na Ulevi Muungwana Blog 5 Wednesday, March 28, 2018 Sunday Mangu ‘Linex’ MSANII wa Bongo Fleva, Sunday Mangu ‘Linex’, ameibuka na kufu

MAKONDA: UKIMPA UJAUZITO MWANAMKE DAR UJIPANGE

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza na wataalamu hao. . …Makonda akiendelea kuzungumza katika tukio hilo. Baadhi ya wataalamu wa masuala ya kisheria waliohudhuria kwenye hafla hiyo. Mkutano huo na wataalamu wa kisheria ukiendelea. JOPO la Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Maofisa Ustawi wa Jamii, Wanasheria pamoja na askari Polisi kutoka Dawati la Jinsia  wamemuhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, kuwa wamejidhatiti vyema kuwasikiliza akinamama waliotelekezwa na hawapatiwi pesa ya matunzo ya mtoto kwenye zoezi la siku tano za kuwapatia msaada wa kisheria linalotaraji kuanza Aprili 9 mwaka huu. Akizungumza na wataalamu hao leo, Makonda amesema tatizo la wamama waliotelekezwa ni kubwa na limekuwa likisababisha kinamama na watoto kuishi maisha ya tabu na kusababisha ongezeko la watoto wa mitaani na vizazi vya watoto wenye chuki na baba zao. Makonda amesema lengo la zoezi hilo sio ugomvi bali ni kumw

Mbowe, Mashinji, Mnyika na Wengine Wawekwa Mahabusu Sentro

Image
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe na baadhi ya viongozi wengine waandamizi wa chama hicho akiwepo Katibu Mkuu Dkt Vincent Mashinji, John Mnyika, Salum Mwalimu na Ester Matiko wamewekwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha polisi Dar es Salaam. Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha hilo na kusema kuwa viongozi hao wamewekwa mahabusu leo Machi 27, 2018 baada ya kuripoti Kituo Kikuu Cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao. “Viongozi Wakuu wa Chama pamoja na wabunge waliokuwa wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao, wamewekwa mahabusu. Polisi hawajaeleza sababu ya kufanya hivyo. Mawakili wetu wanashughulikia. Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi,” alisema Makene.