Posts

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA ITAKAYOTUMIA UMEME SGR-KUTOKA MOROGORO HADI MAKUTUPORA- DODOMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke wakishuhudia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunga kifuniko mara baada ya kutumbukiza karatasi ya majina ya viongozi mbalimbali

Kauli ya Wakili wa viongozi mtandao wa wanafunzi

Image
Wakili wa viongozi wa  Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Reginald Martine amesema wateja wake wameitwa kuhojiwa na mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili kutoa ushahidi wa tukio la ‘kutekwa’ kwa mwenyekiti wao, Abdul Nondo. Akizungumza na MCL Digital leo Machi 14, 2018, Martine amesema tayari viongozi wawili kati ya wanne wa mtandao huo wameshatoa ushahidi wao, kwamba hakuna vitisho vyovyote walivyopewa na polisi. Amesema kuwa polisi wamemhakikishia kuwa hawatawashikilia viongozi hao na mara watakapomaliza kutoa ushahidi wataruhusiwa kuondoka. “Utaratibu wa wakili mtu anapokuwa anatuhumiwa lazima uwe na mteja wako wakati anapohojiwa lakini kama mteja anatoa ushahidi wakili siyo lazima awepo hivyo wanaendelea kutoa ushahidi muda,” amesema. Amesema walishauriana na  mmoja wa makamishna kuwa yeye asiwepo na viongozi hao wakati wanatoa ushahidi wao. Waliofika kuhojiwa na  DCI ni mkaguzi wa haki za binadamu, Alphonce Lusako; katibu wa mtandao hu

Nyama kutoka Afrika Kusini yateketezwa na ZFDA

Image
Picha ya Mtandao Zanzibar. Mamlaka ya Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA), imeteketeza  kilo 48 za nyama kutoka Afrika Kusini baada ya Serikali kusitisha uingizaji nyama kutoka nchini humo kutokana na mlipuko wa bakteria wa listeria. Ilibainika kuwa nyama hizo ziliingizwa nchini kinyume cha sheria, Nyama hizo ni mali ya kampuni ya Qamar ya Vingunguti jijini Dar es Salaam, ilikamatwa Uwanja wa wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume mwishoni mwa wiki iliyopita. Akizungumza leo Machi 14 wakati wa zoezi hilo, mkuu wa kitengo cha uchambuzi wa hatari zinazotokana na chakula wa ZFDA, Aisha Suleiman amesema kilichosababisha kuteketezwa kwa nyama hiyo ni katazo lililotolewa na ZFDA baada ya kutokea mlipuko wa ugonjwa wa listeriosis. Amesema ZFDA ndiyo yenye majukumu ya kuhakikisha wananchi wanapata chakula salama, Aisha amesema uamuzi ya katazo hilo umetokana na uwapo wa maradhi ya Listeriosis nchini Afrika Kusini, hivyo ofisi yao imepiga marufuku uingizwaji nyama, maziw

ANGALIA MAPOKEZI YA A BOY FROM TANDALE YA DIAMOND PLATINUMZ NCHINI KENYA

Image
Kwanza kabisa Diamond kafanya kitu kizuri kwa kuonesha ni kwa namana gani nchi hizi mbili zipo vizuri na kushirikiana vema si kama ambavyo watu wengine huleta ushirikiano wa maneno Sasa hivi Kenya na Tanzania wamekuwa ndugu kwa kuunganishwa na msanii wetu Diamond planumz. Kwa haraka haraka nimejaribu kupitia taarifa mbali mbali za kwenye media nikaona kenya wanampo support ya kutosha kijana wetu. Kwa pamoja tunapaswa kumsapot na kumpongeza kwa hatua hiyo na kwa ukalimu wa watu wa kenya wanao ufanya kwa ndugu yetu huyu.

Kesi ya Madawa: Shahidi Afunguka Alichokikuta Chumbani kwa Wema

Image
Msanii wa filamu, Wema Sepetu (katikati) akiwa na mama yake mzazi Miriam Sepetu (kulia)  wakitoka kusikiliza kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Mama mzazi wa Wema Sepetu akishuka ngazi za mahakama baada ya kusikiliza kesi inayomkabili mwanaye. Wema Sepetu na mama yake, Miriam Sepetu  wakijadili jambo baada ya kusikiliza kesi nje ya mahakama. MJUMBE wa Shina Namba 39, nyumbani anakoishi msanii wa filamu, Wema Sepetu, Steven Alphonce ambaye ni shahidi katika kesi inayomkabili staa huyo, amedai wakati wa upekuzi walikuta kipande cha sigara wala si bangi. Alphonce amesema hayo leo Jumatatu, Machi 12, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, wakati akitoa ushahidi wake katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema na wenzake wawili na kusema alishiriki katika upekuzi nyumbani kwa Wema na kukuta kipande hicho cha sigara jikoni na chumbani kwa

ASLAY HATIMAYE AANIKA UKWELI KUHUSU KUTOKA NA NANDY,AFICHUA YOTE

Image
Msanii wa muziki Bongo, Aslay amefunguka kuhusu ukaribu wake na Nandy kwa sasa. Muimbaji huyo wa ngoma ‘Natamba’ ameiambia FNL ya EATV kuwa kinachowaunganisha ni kazi tu hakuna mahusiano ya kimapenzi kama inavyokuwa ikiripotiwa. Nafikiri mashabiki zangu ambao wananifuatilia wanajua ni mtu ambaye nina mtoto, kuna mwanamke ambaye nimezaa naye. Nandy tupo kwenye kazi tu, tunafanya lakini hamna chochote kinachoendelea kati yangu na Nandy,” amesema. Aslay na Nandy kwa sasa wanafanya vizuri na ngoma ‘Subalkheri’ ikiwa ni ngoma yao ya pili kutoa pamoja baada ya Mahabuba.

MAUWAJI YA KUTISHA TENA ,MTOTO ATEKWA NA KUUAWA KINYAMA

Image
MASKINI MTOTO HUYU! Atekwa na Kuuawa, Mama Mzazi Hoi! Maskini mtoto wa watu! Ndivyo walivyosikika mashuhuda wa tukio la mwanafunzi, Doricka Majeshi, anayesemekana kutekwa kisha kukutwa akiwa ameuawa na watu wasiojulikana ndani ya nyumba inayoendelewa kujengwa na kuibua simanzi nzito. Kwa mujibu wa mashuhuda hao, mtoto Doricka mwenye umri wa miaka nane aliyekuwa anasoma darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Lukobe mjini hapo alidaiwa kukutwa na mkasa huo tangu Jumanne ya wiki iliyopita kisha kusakwa kwa siku tatu bila mafanikio, kabla ya mwili wake kukutwa ukiwa na majeraha Alhamisi iliyopita nyuma ya nyumba hiyo

Naibu Katibu Mkuu wa BAVICHA Ajiuzuru

Image
Naibu Katibu Mkuu Baraza la Vijana Chama cha Demokrasia na Maendeleo – Chadema (BAVICHA), Getrude Ndibalema amesema amejiuzuru nafasi hiyo na kubaki mwanachama wa kawaida ili kutimiza majukumu binafsi.

WAZIRI MWAKYEMBE AFUNGUA MKUTANO WA 14 WA MAAFISA HABARI, MAWASILIANO NA UHUSIANO SERIKALINI

Image
    Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakati wa ufunguzi mkutano wa 14 wa kikao kazi cha Maafisa hao kilichoanza leo Jumatatu tarehe 12-16 Machi, 2018 Jijini Arusha. Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Susan Mlawi akizungumza na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakati wa ufunguzi mkutano wa 14 wa kikao kazi cha Maafisa hao kilichaonza leo Jumatatu tarehe 12-16 Machi,2018 Jijini Arusha.  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kilichaonza leo Jumatatu tarehe 12-16 Machi,2018 Jijini Arusha.  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gabriel Daqqaro akuzungmza na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wakati wa ufunguzi mkutano wa 14 wa kikao kazi cha Maafisa hao kilich

Man United Vs Liverpool, Salah Aundiwa Tume Manchester Utd

Image
Kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Mo­hamed Salah (kulia) Paul Labile Pogba. MANCHESTER United inatarajiwa kuwa mwe­nyeji wa Liverpool, ke­sho Jumamosi kwenye Uwanja wa Old Trafford, mchezo huo ni mkubwa na unasubiri­wa kwa hamu. Kuelekea mtanange huo, gumzo kubwa ni juu ya uwezo wa kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Mo­hamed Salah ambapo mashabiki wa Unit­ed wameanza kupata hofu kuhusu mchezaji ambaye atamzuia. Kawaida Salah amekuwa akipangwa kushambulia akitokea kulia, kwa aina ya ulinzi wa United beki wa kushoto am­baye atatakiwa kukutana naye ni Ashley Young au Luke Shaw, sasa hapo ndipo patamu, imeibuka hoja juu ya nani mwe­nye uwezo kati yao anayeweza kumficha Salah. Mchezo uliopita timu hizo zilipoku­tanaa ulimalizika kwa suluhu, huku Mar­teo Darmian akipangwa kucheza beki wa kushoto, kwa sasa beki huyo siyo chaguo la kwanza la Kocha Jose Mour­inho. Kutokana na ubora wa Salah kufun­ga, mashabiki wa United kutoka mataifa mbalimbali wamepaza sauti wa

Rais Kenyatta, Odinga Waahidi Kuwaunganisha Wakenya

Image
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto) akiwa na kiongozi wa muungano wa upinzani nchini humo Raila Odinga. RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta amekutana na kiongozi wa muungano wa upinzani nchini humo, Raila Odinga, katika ofisi yake ya Jumba la Harambee, Nairobi,a mba po viongozi hao kwa pamoja wamekubaliana kuunda taifa lenye umoja. “Tumekubaliana tutawaleta pamoja wananchi na kujadiliana kuhusu matatizo yanayoathiri taifa letu na wananchi, na kuunda taifa lenye umoja na lililo imara ambapo hakuna raia anayehisi ametengwa,” alisema Rais Kenyatta baada ya mkutano huo. “Tumekutana na ndugu yangu Kenyatta, tumeongea kwa kirefu na kukubaliana kwamba tunataka kuiunganisha Kenya iwe taifa moja. Mgawanyiko ambao umekuwepo tangu uhuru utakwisha  na sisi tutembee pamoja,” alisema Raila Odinga katika hafla hiyo.