Rais Kenyatta, Odinga Waahidi Kuwaunganisha Wakenya
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto) akiwa na kiongozi wa muungano wa upinzani nchini humo Raila Odinga.
“Tumekubaliana tutawaleta pamoja wananchi na kujadiliana kuhusu
matatizo yanayoathiri taifa letu na wananchi, na kuunda taifa lenye
umoja na lililo imara ambapo hakuna raia anayehisi ametengwa,” alisema
Rais Kenyatta baada ya mkutano huo.
“Tumekutana na ndugu yangu Kenyatta, tumeongea kwa kirefu na kukubaliana kwamba tunataka kuiunganisha Kenya iwe taifa moja. Mgawanyiko ambao umekuwepo tangu uhuru utakwisha na sisi tutembee pamoja,” alisema Raila Odinga katika hafla hiyo.

Comments
Post a Comment