Man United Vs Liverpool, Salah Aundiwa Tume Manchester Utd

Kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Mo­hamed Salah (kulia) Paul Labile Pogba.

MANCHESTER United inatarajiwa kuwa mwe­nyeji wa Liverpool, ke­sho Jumamosi kwenye Uwanja wa Old Trafford, mchezo huo ni mkubwa na unasubiri­wa kwa hamu.
Kuelekea mtanange huo, gumzo kubwa ni juu ya uwezo wa kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Mo­hamed Salah ambapo mashabiki wa Unit­ed wameanza kupata hofu kuhusu mchezaji ambaye atamzuia.

Kawaida Salah amekuwa akipangwa kushambulia akitokea kulia, kwa aina ya ulinzi wa United beki wa kushoto am­baye atatakiwa kukutana naye ni Ashley Young au Luke Shaw, sasa hapo ndipo patamu, imeibuka hoja juu ya nani mwe­nye uwezo kati yao anayeweza kumficha Salah.

Mchezo uliopita timu hizo zilipoku­tanaa ulimalizika kwa suluhu, huku Mar­teo Darmian akipangwa kucheza beki wa kushoto, kwa sasa beki huyo siyo chaguo la kwanza la Kocha Jose Mour­inho.

Kutokana na ubora wa Salah kufun­ga, mashabiki wa United kutoka mataifa mbalimbali wamepaza sauti wakitoa maoni kuwa ni bora akaanza Shaw kwa kuwa ni beki halisi wa kushoto na hata­takiwa kupanda mara kwa mara, huku wakidai Young ambaye ndiye anay­etumika mara nyingi siyo beki halisi mch­ezo uliopita United ilicheza mbinu y a ku­zuia zaidi ki­tendo amba­cho kilimkera Kocha wa Liver­poo, Jurgen Klopp. Kwa sasa United haita­rajiwi kuendeleza staili hiyo kwa kuwa inahitaji ushindi na ipo nyum­bani.

Liverpool ina kasi kubwa ya kufunga ma­bao lakini imekuwa ikiruhusu kufungwa mabao mengi pia tofauti na United ambayo im­ekuwa ngumu kufungika hasa inapokuwa nyum­bami.
Young ni winga lakini amekuwa aki­tumika kama mlinzi wa kushoto.

Mbali na Salah mas­taa wengine wa Liverpool ambao wata­takiwa ku­chungwa ni Sadio Mane na Roberto Firmino ambao wamekuwa na kasi kubwa ya kufunga hivi karibuni.

Comments

Popular posts from this blog

PICHA ZA UTUPU ZILIZOPIGWA NA MWANAFUNZI WA UDOM ILI KUTANGAZA SOKO LA MWILI WAKE. TAZAMA HAPA

ZITTO KABWE AWAPONDA LOWASSA NA MAGUFULI