Posts

Mwalimu atiwa mbaroni kwa kumuua mtoto wa miezi 7

Image
Mwalimu wa sekondari Stephen Wachira Wangara mwenye umri wa miaka 43, amefikishwa Mahakamani kwa kosa la kumuua mtoto wake wa miezi 7 kwa kumchinja na panga nchini Kenya. Mashahidi watano wa tukio hilo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Jimbo la Kirinyaga, Maina Muriuki wamemweleza Jaji Lucy Gitari wa Mahakama Kuu ya Kerugoya, jinsi mtuhumiwa alivyoua mtoto wake, Maina ameieleza Mahakama kuwa mwili wa mtoto huyo ulikuwa umewekwa ndani ya gunia ukiwa na damu, nje ya nyumba ya Wangara na pembeni ya mwili huo kuliwa na panga ambalo lilitumiwa kumuua mtoto huyo. Shahidi mwingine Joseph Muriithi amesema wakati wa tukio hilo alikuwa shambani kwa Wangara akifanya kibarua na alimwona mtuhumiwa akiwa na madoa ya damu na muda mfupi baadaye alisikia kelele kutoka kwenye nyumba ya mwalimu huyo. Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi March 1, 2018, ambapo itasikilizwa tena. Wangara ambaye ni mtuhumiwa ni baba mwenye watoto wawili na mwalimu katika shule ...

AMBAKA ASKARI MWENZAKE ‘AKIMRINGISHIA’ UUME MREFU

Image
  Luteni-Kanali Chris Davies anayeshitakiwa kumbaka askari mwanamke baada ya kupiga vileo na wenzake huko Canada. ASKARI wa Uingereza aliyewahi kuwa shujaa wa vita nchini Afghanistan, hivi majuzi alimbaka askari mwenzake wa kike baada ya kujigamba kwamba alikuwa na uume mrefu. Haya yalisema mahakamani ambapo Luteni-Kanali Chris Davies anashitakiwa kwa kumbaka askari ambaye ni mama wa watoto wawili na  umri wa miaka 53 katika tukio linalodaiwa kufanyika huko Kingston, Ontario,  Canada. Davies anasemekana kumwambia mwanamke huyo kwamba: “Nina uume wenye urefu wa inchi nane (sentimita 20.3) ambao unaweza kuubomoa ulimwengu wako.” Davies anadaiwa kumwambia mwanamke huyo kwamba: “Nina uume wenye urefu wa inchi nane (sentimita 20.3) ambao unaweza kuubomoa ulimwengu wako.”  Jina na utambulisho wa mwanamke huyo vimehifadhiwa. Mwanamme huyo anadaiwa alimfuata mwanamke huyo hadi hotelini kwake baada ya mwanamkehuyo ‘kubugia’ pombe mbalimbali za...

MWANAMKE AMWAMBIA MUMEWE ANATAMANI WANAUME WENGINE

Image
ANITA CASSIDY (40) mwanamke ambaye amekuwa katika ndoa kwa miaka ipatayo kumi, alimwambia mumewe aitwaye Marc (46) kwamba anaona maisha na ndoa ya mume na mke yamemchosha na alitaka kuwa na wenza wengine wa kufanya nao mapenzi. Katika mazungumzo ya wawili hao ambao ni raia wa Italia, mumewe alikubali kwamba wote wawili kila mmoja angekuwa na wapenzi wengine.    Lakini, je, katika ndoa moja panawezekana kuwa na watu zaidi ya wawili? Anita Cassidy (katikati) akiwa na mpenzi wake wa kiume Andrea (kushoto) na mumewe Marc (kulia) wakichangia penzi la watu watatu. “Mwaka mmoja uliopita niliweka kila kitu bayana kwenye mtandao wa Facebook kwa picha niliyokuwa na mume wangu na watoto wetu wawili.  Marafiki zangu wakaanza kuniuliza kwamba mwanamme mwingine aliyekuwa katika picha alikuwa nani.  Niliwaambia alikuwa Andrea – mpenzi wangu wa kiume. … Watatu hao wakiwa pamoja kando ya bahari wakipunga upepo. “Nafahamu wengi watashangaa kwani w...

Akukumiwa Kwa kumwingilia mwanaume kinyume cha maumbile

Image
Mahakama ya Mkoa wa Mwera imemuhukumu mshtakiwa Simai Khamis Salum mwenye umri wa miaka 30 mkaazi wa Uzini wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kutiwa hatiani kwakosa lakumuingilia mwanamme mwenziwe kinyume na maumbile. Imedaiwa Mahakamani hapo namuendesha mashtaka Rahima Kheir mbele ya hakimu Muhammed Ali Muhammed kwamba mnamo tarehe 2/3 /2015 huko Uzini bila ya ridhaa kwamakusudi amefanya kitendo hicho kwakijana mwenye umri wa miaka 20 jinalimehifadhiwa na kumsababishia maumivu makali huku akijua jambo hilo ni kosa kisheria. Akisoma hukumu Hakimu Muhammed amesema Mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa kwa upande wa mashtaka na kumuona nimkosa wakosa hilo ndipo Mahakama hiyo ilipomtia hatiani kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka saba pamoja na kumlipa fidia mtendewa yashilingi Milioni mbili ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama hiyo.

Mawakili wa Sugu wajiondoa kwenye Kesi

Image
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi-Mbeya, Michael Mteite, amegoma kujitoa katika kusikiliza kesi inayowakabili Mbunge Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga. Mapema leo Alhamisi Januari 25,2018 Sugu na Masonga waliwasilisha ombi mahakamani wakimkataa hakimu huyo wakitaka ajitoe kusikiliza kesi kwa maelezo kuwa hawana imani naye. Hakimu Mteite amesema sababu zilizotolewa na akina Sugu hazipo kisheria na hazimfanyi kujitoa. Baada ya hakimu kukataa kujitoa, mawakili Boniface Mwabukusi, Hekima Mwasipu na Sabina Yongo wanaowawakilisha washtakiwa walitangaza kujitoa katika shauri hilo. Sugu, mwenzake wamkataa hakimu Sugu na Masonga wameiomba Mahakama kuwapatia wiki mbili za kutafuta mawakili wengine. Hakimu Mteite ameahirisha kesi hadi Februari 2,2018 na ameamuru washtakiwa kurejeshwa rumande.

Lowassa, Membe Uso kwa Uso Nyumbani kwa Gwajima

Image
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa akiteta na Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani, Bernard Membe walipokutana leo katika msiba wa mama mzazi wa Askofu Josephat Gwajima nyumbani kwake Salasala, Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni  Mbunge wa Vunjo, James Mbatia;  Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema,  Bernard Membe  na Lowassa wakiwa kwenye msiba huo. WAZIRI Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa wamekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani, Bernard Membe leo katika msiba wa mama mzazi wa Askofu Josephat Gwajima nyumbani kwake Salasala jijini Dar es Salaam. Lowassa na Membe ni miongoni mwa viongozi waliochukua fomu kusaka ridhaa ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa 2015, ambapo jina la Lowassa lilienguliwa huku Membe akiingia hatua ya tano licha ya kushindwa katika hatua ya tatu bora.  ...

Mama wa Askofu Gwajima afariki Dunia

Image
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo Januari 21, 2018 amepata pigo kwa kuondokewa na mama yake mzazi Ruth Basondole Gwajima ambaye amefariki asubuhi ya leo. Gwajima amesema kuwa mama yake mzazi amefariki akiwa na umri wa miaka 84 na kuwa mazishi ya mama yake mpendwa yatafanyika siku ya Alhamisi ya Januari 25, 2018 Salasala jijini Dar es Salaama. "Leo Saa mbili asubuhi mama yangu Mzazi, Bi Ruth Basondole Gwajima ametwaliwa na Bwana. Karudi Mbinguni akiwa na Umri wa Miaka 84. Kuna Furaha ya Ajabu Shujaa Wangu Amerudi kwao. Kwasababu katika maisha yake alimtumikia Mungu. Mazishi yatafanyika Alhamis Tarehe 25/01/2018; Salasala Dar es Salaam" alisema Gwajima. EATV.

Julitha Kabete Kukanyaga Miss World ni Mungu tu!

Image
Mrembo ambaye aliiwakilisha Tanzania katika mashindo ya Miss World 2017, Julitha Kabete. MREMBO ambaye aliiwakilisha Tanzania katika mashindo ya Miss World 2017, Julitha Kabete amesema kuwa mpaka kuweza kupata nafasi ya kwenda kuiwakilisha nchi yake sio kazi ndogo kama watu wanavyodhani kwani ameenda kuonesha ulimwengu kuwa hata taifa lake linaweza, haliko nyuma kitu ambacho kilimfanya asilale kwa ajili ya kuhakikisha anarudi na kitu ambacho kitaacha alama ya nchi yetu. Mrembo huyo amefanya mahojiano na Mikito Nusunusu na kuongea mengi kama ifuatavyo hapa chini: Mikito Nusunusu: Ni kitu gani kilikufanya uamue kwenda kushiriki Miss World nani alikusuma kufanya hivyo? <span style="display: inline-block; width: 0px; overflow: hidden; line-height: 0;" data-mce-type="bookmark" class="mce_SELRES_start"></span> Julitha: Miss World ilikuwa ndoto yangu tangu niko mdogo sana. Pia nilivyozidi kukua niliona kua plat...

Faiza ampa somo Diamond

Image
Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Faiza Ally amempa ushauri msanii wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz kuwa kwa sasa ni muda wake wa kula ujana na kuizunguuka dunia na sio muda wa kujipa majukumu mazito ile hali umri wake bado mdogo. Faiza Ally amesema Diamond bado hajamaliza hata robo ya dunia hivyo ingawaje ana jina kubwa barani Afrika hivyo angefanya kwanza vitu kama hivyo kuizunguuka dunia ikibidi ajiweke kando na mambo ya mahusiano. “Diamond kijana mdogo sana anahitaji kuhave funny na watoto wenzie na sisi wadada wazima lazima taungalie watu wa kutoka nao, Go baba have a funny enjoy the world ndio useto down,“ameandika Faiza Ally kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumshauri kuwa ikibidi ajiweke mbali na mahusiano. “Jiachie uwe huru ikibidi usiwe na mahusiano, bado hujaiona dunia hata robo wewe ni star hela ipo there is alot to see nasema with clean heart no hate kwa Zari au kwa yeyote.“ameandika Faiza. Ushauri huo umekuja ikiwa ni wiki sasa imepi...

FT: RUVU SHOOTING 0-1 YANGA, KUTOKA UWANJA WA TAIFA

Image
Kiungo mahiri wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi (kushoto) akifanya yake na wachezaji wa Ruvu Shooting. MPIRA UMEKWISHA DAKIKA YA 93 SUB Dk 81 Abdulrahman Mussa anakwenda nje Hamisi Mcha anachukua nafasi yake Dk 80, Yanga wanacheza kindava nje kidogo ya nje ya lango lao. Inachongwa faulo, shuti kali linapigwa, goal kick Dk 78, Bofu anageuka vizuri, anapiga krosi safi, al manusura iingia nyavuni Dk 73, Ruvu wanapata kona hapa, inachongwa vizuri, Kanduru anaachia mkwaju, goal kick Dk 71, Dante yuko chini baada ya kusukumwa na Kanduru Tambwe akiwa kaweka mtu kati. DK 88, krosi safi ya Martin, Mahadhi yeye na nyavu, anapaishaa puuuuuu SUB Dk 86 Daud anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Pato Ngonyani, Yanga wakiimarisha ulinzi SUB Dk 81 Abdulrahman Mussa anakwenda nje Hamisi Mcha anachukua nafasi yake Dk 80, Yanga wanacheza kindava nje kidogo ya nje ya lango lao. Inachongwa faulo, shuti kali linapigwa, goal kick SUB Dk 70 Buswita analambwa kadi ya njano ba...

Waziri Mpina awasilisha majina ya Viongozi waliokaidi agizo la Serikali

Image
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewasilisha majina ya viongozi wa halmashauri ambazo hazijaanza kutekeleza upigaji chapa mifugo na zile ambazo ziko chini ya asilimia 10 ya utekelezaji, Kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo ili zichukuliwe hatua. Mpina alibainisha hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa upigaji chapa mifugo nchini, mjini Dodoma. Alisema kwa tathmini iliyofanyika hadi sasa jumla ya ng’ombe 10,306,359 sawa na asilimia 59.3 wamepigwa chapa huku asilimia 40.7 wakiwa hawajapigwa chapa na zoezi hilo linatarajiwa kukamilishwa Januari 31, mwaka huu. “Halmashauri 100 zimepiga chapa zaidi ya asilimia 50, halmashauri 54 zimepiga kati ya asilimia 10 hadi 50, halmashauri 14 zimepiga chini ya asilimia 10 na Halmashauri 9 hazijaanza kupiga chapa,” alisema Mpina. Alizitaja halmashauri ambazo hazijaanza kabisa ni Tandahimba,...

Anayecheza Na Moyo Wako ni Sawa Na Muuaji; Utamjuaje?

Image
WENGI wamejikuta kwenye majuto kwa kuwakabidhi watu wasiofaa mioyo yao. Wameambulia mateso makali, wamejikuta wamepoteza muda kwani wameachwa solemba wakati ambao hawakuutarajia. Ndugu zangu mapenzi yanauma. Yanauma kwelikweli hasa linapokuja suala la kumkabidhi mtu moyo wako ukiamini atakupenda, atakuthamini kama vile wewe unavyomthamini. Unakuwa na matumaini kwamba nipo na mtu sahihi. Mtu ambaye nitafanya naye maisha, mtu ambaye nitadumu naye katika shida na raha, mtu ambaye nitaingia naye kwenye ndoa mwisho wa siku anaingia mitini, inauma sana. Mapenzi ni uwekezaji. Unawekeza nguvu, akili na maisha. Unapokuwa na mwenzi wako unamuamini. Unapanga naye mipango ya kufika mbali kwani kila ambaye anawaza maisha, lazima atakuwa anaifikiria ndoa na mtu sahihi. Atafikiria familia kwa maana ya kupata watoto, kusomesha na mambo mengine yahusuyo familia. Hiyo ndio safari ya wapendanao, inayoanzia kwenye urafiki, uchumba na hata baadaye ndoa. Wahusika wanapoikamilisha safa...

Waziri Mkuu atoa agizo kwa TAKUKURU

Image
Waziri Mkuu .Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa ameaagiza TAKUKURU kumkamata Meneja wa TBA wilaya ya Butiama mkoani Mara kutokana na uzembe na kutumia fedha za Serikali kinyume na maelekezo. Waziri Mkuu amefanya maamuzi hayo baada ya Serikali kupeleka fedha zaidi ya milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la halmashauri lakini mpaka sasa fedha ujenzi huo haujaanza na fedha hizo kutumika katika miradi mingine ambayo haijapangwa na Serikali. "Tumeleta fedha milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la halmshauri lakini mmezipeleka kwenye shughuli nyingine, kwanini hajajenga jengo hili ikiwa fedha zimeshaletwa? Tumeleta fedha milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya, DAS na nyumba ya watumishi lakini mmejenga nyumba moja tu ya DC, nyumba zingine mbona hamjaanza kujenga? Waziri Mkuu baada ya kukosa majibu yanayoridhisha kutoka kwa viongozi hao ndipo alipoagiza TAKUKURU kumchukua moja ya mtumishi wa halmshauri hiyo na kusema kuwa serikali haiwezi ku...

WAZIRI MKUU KUZAA BAADA YA KUINGIA OFISINI

Image
WAZIRI Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern anategemea kujifungua mwezi Juni mwaka huu na kumfanya kuwa kiongozi wa kwanza duniani tangu 1990 kujifungua akiwa ofisini, jambo ambalo watu wengine wanadai ni tatizo. Tukio hilo hili halimhusu aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, Tony Blair,  ambaye alipata mtoto aitwaye Leo, kutoka kwa mkewe Cherie,  jambo ambalo lilimfanya Blair ajikute ‘akimnyonyesha’ mtoto wake huyo kwa njia fulani huku akiwa anaendelea na kazi zake. Akiwa na mwenza wale, Clarke Gayford, wakitangaza ujauzito wake. “Mwaka huu tutaungana na wazazi wengi wanaovaa kofia mbili.  Nitakuwa waziri mkuu na mama, ambapo Clarke (Gayford) atakuwa Mwanamume wa Kwanza (mume wa waziri mkuu),” alitangaza Ardern mwenye umri wa miaka 37, akimtaja mwanamume huyo, mtangazaji katika kituo kimoja cha televisheni, kuwa ndiye mwenza wake katika ujauzito huo. Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern. Clarke, ambaye pia ni mpenzi wa kuvua samaki, wata...

Snura: Mwanamke anayelea watoto mwenyewe ni elimu tosha Duniani

Image
MWANAMUZIKI anayefanya vizuri kwenye miondoko ya mduara, Snura Mushi, ameibuka na kudai kuwa mwanamke anayelea watoto mwenyewe ni elimu tosha duniani. Akizungumza na Mikito Nusunusu, Snura alisema kuwa, amepata changamoto nyingi sana kwenye kulea watoto wake lakini anashukuru amesimama vyema kama mwanamke shujaa na amejifunza mengi ikiwa ni pamoja na kuwa jasiri ambapo anaweza kusimama popote sasa na kujiamini. “Yaani kulea watoto mwenyewe kama mwanamke ni elimu tosha ya duniani na mimi najivunia hilo sana, mwanzo ilikuwa ni ngumu sana na sisi wanawake tumekuwa tukiwategemea sana wanaume wakiwepo lakini ukiyajaribu maisha ya ulezi peke yako na kuyashinda unajikuta jasiri ambaye unaweza

Joyce Kiria amwaga siri za mumewe hadharani

Image
Mwanaharakati na mwanamke shujaa nchini Tanzania, Joyce Kiria ameweka hadharani kuwa mahusiano yake kwa sasa na mumewe Henry Kileo ambaye alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali CHADEMA. Joyce Kiria amesema kuwa kwasasa mahusiano yake hayapo sawa kwani yeye amekuwa ndiye baba na mama wa familia kwa kila kitu yaani kuhudumia familia nzima pamoja na mumewe. Akitoa taarifa hiyo kwa umma kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akibubujikwa na majozi, Kiria amesema huwa anamshauri mumewe atafute japo kazi itakayowaingizia kipato ili kusaidiana kutunza familia lakini mumewe anakuwa mkali na kumpiga. “Sikutegemea kama ipo siku kwa mkono wako ungeunyanyua kunipiga (@kilewo2020mwanga) ukasahau kabisa! ukasahau yooote. Nimeharibu career yangu kupigania ndoto yako kwa kugawa watu wangu kwenye biashara zangu, nimepoteza ndugu jamaa na marafiki, umeniachia nimebeba mzigo wa familia kwa muda wote, Malipo yako ni kunipiga/ kunidhalilisha na kunitoa machozi, umenipiga kwa sababu...

Waziri Mkuu Akagua Shamba La JKT

Image
Waziri Kassim Majaliwa amekagua shamba la uzalishaji wa mbegu bora za mihogo aina ya mkombozi linalomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Rwamkoma wilayani Butiama. Amekagua shamba hilo linalomilikiwa na Kikosi cha JKT Rwamkoma leo (Jumamosi, Januari 20, 2018) alipowasili wilayani Butiama akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mara. Kikosi hicho kimewezeshwa na Halmashauri ya Butihama. Waziri Mkuu amewakipongeza kikosi cha JKT Rwamkoma kwa uamuzi huo wa kuzalisha mbegu bora za mihogo ambazo baadae zitasambazwa kwa wakulima wa zao hilo wilayani hapa.Pia amewataka wakazi wanaoishi karibu na shamba la kikosi hicho hilo kulitumia kama shamba darasa kwa ajili ya kujifunza namna bora ya kulima zao hilo. Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Kanali David Msakulo alisema shamba hilo linaukubwa wa ekari 60, na mbegu zitakazozalishwa zitatosha kupanda ekari 900.Mkuu huyo wa kikosi hicho aliongeza kuwa mbegu hizo zinazozalishwa katika shamba hilo zi...

Tahadhari Kuhusu Homa ya Chikungunya, Hakuna Tiba Mahusi Wala Kinga

Image
Serikali kupitia Wizara ya Afya imeutahadharisha umma kuhusu ugonjwa wa Homa ya Chikungunya ambao huambukizwa na mbu aina ya aedes na hauna tiba mahsusi wala kinga. Isome taarifa hii kuelewa zaidi kuhusu ugonjwa huo.    

Waziri Aagiza Kaimu Mkurugenzi Wa Maji Kusimamishwa Kazi

Image
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Kitila Mkumbo kumsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Maji Mijini, Clement Kivegalo. Pia, Kamwelwe amemwagiza mkurugenzi wa utawala wa wizara hiyo, Barnabas Ndunguru  kuwahamishia Dodoma watumishi 178 wa wizara ifikapo Januari 30, 2018 la sivyo atamchukulia hatua. Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 20, 2018 jijini Dar es Salaam, Waziri Kamwelwe amesema jana Januari 19, alizivunja bodi  za maji safi za Mkoa wa Arusha na Musoma baada ya kujiridhisha kuwa utendaji wao si mzuri. “Juzi tu niliuondoa utendaji wa Lindi, kuna tatizo la utendaji wa wakandarasi hapa Dar es Salaam, Chalinze na tuna tatizo Kigoma, mamlaka za maji za miji ya mikoa  zinasimamiwa na mkurugenzi wa maji mijini, hapa tuna idara kama tatu au nne zinasimamia utekelezaji wa miradi hiyo,” amesema Mhandisi Kamwelwe na kuongeza, “Idara ya maji mijini inaongozwa na Kaimu Mkur...

Nicole Aingilia Ishu Ya Wastara Kuchangiwa Pesa

Image
Msanii wa filamu Bongo, Nicole Francklyn. MSANII wa filamu Bongo, Nicole Francklyn amewataka wasanii wenzake kuungana na kuendesha kampeni ya kumchangia msanii mwenzao, Wastara Juma kutokana na maradhi ya mguu yanayomsibu, kwa kuwa hakuna aijuaye kesho. Wastara Juma Akizungumza na Star Mix , Nicole alisema, kama wasanii wangekuwa na umoja na kuungana katika hilo, kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakijionyesha kumwaga pesa kwenye mambo ya starehe, endapo wangejitoa kwa moyo mmoja kwenye suala hilo, basi kivyovyote vile michango ingekuwa imetimia. “Niwasihi wasanii wenzangu tuungane kumchangia Wastara michango iweze kutimia akamilishe matibabu yake, naamini sapoti ya wasanii iliyopo bado haitoshi waongeze nguvu kwenye hili, hata kama mtu ana visasi naye aweke kando kwa sasa, kwa sababu matatizo yanaweza kumfika yeyote yule,” alisema