Lowassa, Membe Uso kwa Uso Nyumbani kwa Gwajima
Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa akiteta na Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani, Bernard Membe walipokutana leo katika msiba wa mama mzazi wa Askofu Josephat Gwajima nyumbani kwake Salasala, Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Vunjo, James Mbatia; Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, Bernard Membe na Lowassa wakiwa kwenye msiba huo. WAZIRI Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa wamekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani, Bernard Membe leo katika msiba wa mama mzazi wa Askofu Josephat Gwajima nyumbani kwake Salasala jijini Dar es Salaam. Lowassa na Membe ni miongoni mwa viongozi waliochukua fomu kusaka ridhaa ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa 2015, ambapo jina la Lowassa lilienguliwa huku Membe akiingia hatua ya tano licha ya kushindwa katika hatua ya tatu bora. Baada ya jina lake kuen