Posts

DK Cheni Afunguka Lulu Kugomea Rufaa

Image
Muigizaji wa muda mrefu nchini, Mahsein Awadh maarufu kama Dk Cheni, akiwa na msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’. DAR ES SALAAM: Muigizaji wa muda mrefu nchini, Mahsein Awadh maarufu kama Dk Cheni, amefunguka kuhusu tetesi zilizozagaa mitandaoni, zikimhusisha kuhusu kugomea rufaa kwa msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’. Katika posti za watu mbalimbali mitandaoni, waliandika kuwa Dr Cheki alisema Lulu ambaye ameanza maisha ya gerezani, alikataa ndugu zake wasikate rufaa kwa kile alichosema, anataka kumaliza kifungo chake mapema ili awe huru kisaikolojia. Lakini juzi, Dk Cheni ambaye alikuwa staa pekee aliyekuwa akihudhuria mahakamani wakati kesi hiyo ikifanyika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, alikanusha kuzungumza na Lulu, kwani hata siku ya hukumu hakuwepo kortini. “Siyo kweli, mimi sijazungumza na Lulu tangu siku ile ya hukumu, kwanza sikuwepo mahakamani na hadi leo ninapoongea na wewe sijaenda kumtembelea gerezani, kwa hiyo hayo maneno siyo yangu,” alisema mui...

IRENE UWOYA ROHO MKONONI RWANDA! ANASWA NA MABAUNSA

Image
Muigizaji Irene Uwoya Siku chache baada ya Hamad Ndikumana ‘Katauti’ kufariki dunia, imedaiwa kuwa, usalama wa mzazi mwenziye marehemu, muigizaji Irene Uwoya ambaye jana alikwea ‘pipa’ kwenda kuhani msiba nchini Rwanda ni mdogo. Uwoya ambaye alifunga ndoa na marehemu na kuishi naye kwa miaka kadhaa kabla ya kutengana, alianza kufanya mipango ya safari Jumatano iliyopita, saa chache mara baada ya kupokea taarifa za kifo hicho kilichotokea Jumanne usiku. CHANZO CHAFUNGUKA Kwa mujibu wa chanzo makini kutoka Rwanda, kuna kikundi cha watu ambacho kimekuwa na hasira na mrembo huyo kwa kile wanachofikiri kuwa kifo cha Ndikumana kimetokana na ‘stress’ zilizosababishwa na mrembo huyo. “Kwa kweli huku usalama wa Uwoya ni mdogo sana maana kama unavyojua kuna mashabiki ambao walikuwa wanamkubali Ndikumana ambaye alikuwa na mchango mkubwa sana katika soka la Rwanda,” kilidai chanzo hicho. WANAAMINI UWOYA NDIYO KIKWAZO Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, wan...

Sababu za Mbowe kutomuheshimu Lipumba hizi hapa

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amedai kwamba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF anayetambuliwa na msajili wa vyama Prof. Ibrahim Lipumba kuwa ni Profesa wa ajabu ambaye anaweza kubomoa chama alichokijenga. Akiwa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo Mtwara, Mh. Mbowe amesema kwamba hana ugomvi wowote na Prof Lipumba ingawa amekiri atakuwa muongo akisema kwamba anamuheshimu kwani anatumika katika kukivuruga chama alichokuwa akikiongoza kwa muda mrefu. Mh. Mbowe amesema kwamba wakati CUF ikishirikiana na UKAWA kwa ujumla kutafuta kura na kuongeza wabunge wa chama hicho bungeni, yeye Prof Lipumba alikuwa mafichoni na anamshanga sasa hivi anavyorudi ndani ya chama hicho na kutaka kukisambaratisha. "Sina ugomvi na Prof Lipumba lakini nikisema namuheshimu nitakuwa muongo sana. Prof Lipumba ni msomi sana tena msimchezee kwenye elimu lakini usomi ni jinsi unavyotumia elimu yako lakini siyo wingi wa vyeti. Ni Profesa wa aja...

Baada ya hukumu Lulu, Mama Kanumba afunguka

Image
Mama wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka na kusema kwamba leo atakwenda makaburi ya kinondonni alipoziikwa mwanaye ili kwenda kumzika upya. Mama Kanumba ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kumhukumu kifungo cha miaka miwili Muigizaji Elizabeth Michael ambaye alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia yaliyopelekea kifo cha muigizaji huyo. "Kwa sasa sina la kusema ila  naishukuru sana Mahakama kwa kutenda haki, pia niishukuru sana Serikali yangu lakini pia nikitoka hapa nitakwenda makaburini kwa ajili ya kumzika upya mwanangu Kanumba". Mama Kanumba. Kwa upande wa Wakili wa Muigizaji Lulu Peter Kibatala ameweka wazi kwamba watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake. Muigizaji Lulu leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake Steven Kanumba usiku wa Aprili 7 2012.

Zitto aizungumzia Bombadier Bungeni

Image
Serikali imekiri kujitoa kwenye Mpango wa Kimataifa wa uendeshaji wa shughuli za serikali kwa uwazi (OGP), ambao serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilijiunga Septemba 21 mwaka 2011. Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mh. George Mkuchika wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe lililohoji kwanini serikali imejitoa kwenye Mpango wa Kimataifa wa uendeshaji serikali kwa uwazi (OGP). Mh. Mkuchika amesema baada ya serikali kushiriki kwenye utekelezaji wa mpango huo kwa muda wa miaka minne imeamua kujitoa, ambapo ameongeza kuwa sio nchi ya kwanza kujitoa kwenye mpango huo. “Baada ya serikali kushiriki utekelezaji wa mpango huo kwa muda wa miaka minne imeamua kujitoa, na Tanzania sio nchi pekee iliyojitoa, zipo nchi kama Hungury na Urusi zilijiunga na baadae kujitoa”, amesema Waziri Mkuchika. Kwa upande mwingine Mh. Zitto ameshauri kuwa serikali ingeendelea kuwa mwanachama wa (OGP) ingefaidi...

Breaking News: Lulu ahukumiwa kwenda jela

Image
Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemhukumu kwenda jela miaka miwili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael (Lulu) ambaye alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia. Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Sam Rumanyika aliyekuwa anaendesha kesi hiyo, na kusema kwamba mshtakiwa amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia kutokana na ushahidi wa mazingira, hivyo atatumikia kifungo cha miaka miwili jela. "Ushahidi wa mazingira unaweza kutumika kama msingi pekee wa kumtia hatiani mshtakiwa tena mshtakiwa pekee, sasa ninapokwenda kuangalia maelezo ya mshtakiwa kama yanakidhi vigezo nilivyosema awali, kwa mujibu wa mshtakiwa alisema alianza kupigwa na marehemu, marehemu alilewa lakini mshtakiwa alitakiwa kutoa maelezo yanayo jitosheleza, kwa hili mshtakiwa alijikanganya", amesema Jaji Rumanyika. Jaji Rumanyika ameendelea kwa kusema kwamba.."mshtakiwa katika maelezo yake hakueleza kuwa marehemu alianguka au laah wakati anamkimbiza, mae...

Orodha kamili ya washindi wa tuzo za AFRIMA 2017

Image
Zoezi la ugawaji wa tuzo za muziki za AFRIMA (All Africa Music Awards) kwa mwaka 2017 limehitimishwa jana nchini Nigeria katika Hoteli ya Eko.Mastaa kadhaa wameweza kujishindia tuzo hiyo kubwa ya muziki kama vile Wizkid, Simi, M.I, Tiwa Savage, Ycee, Orezi, 2Baba, Alikiba na wengineo. Kwa upande wa Wizkid aliondoka tatu ambazo ni Song of the Year, Artist of the Year & Best West African Act (Male), na kwa msanii Alikiba aliondoka na tuzo mbili Best Africa Collaboration na Best Artist or Group in Africa RnB and Soul. Orodha kamili ya washindi; Best Central African Act (Male) – Locko Best Central African Act (Female) – Montess Best East African Act (Male) – Eddy Kenzo Best East African Act (Female) – Nandy Best Southern Africa Act (Male) – Emtee Best West African Act (Male) – Wizkid Best West African Act (Female) – Tiwa Savage Best African Collaboration – Alikiba feat M.I – “AJE“ Best Artist in African Rock – Gilad Millo (Kenya) Best Artist or Grou...

Zitto Kabwe aomba msaada serikalini

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, ameonyeshwa kushangazwa na kitendo cha serikali kutangaza mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya Standard Gauge huku vifaa vingi vikiagizwa kutoka nje ya nchi na kuomba msaada wa ufafanuzi. Kwenye ukurasa wake wa facebook Zitto Kabwe ameandika waraka akitaka maelezo kutoka serikalini, ni kwa namna gani serikali inaendesha mradi mkubwa kama huo bila kuweka vifungu vya kufungamanisha na sekta nyengine nchini, na kudhamiria kuagiza chuma nje wakati nchi ina chuma ambacho bado hakijaanzwa kuchimbwa. Usome ujumbe wote hapa chini.

BASATA yaongea kuhusu Msondo Ngoma kumdai Diamond Milioni 300

Image
Baada ya Band ya Msondo Ngoma kutaka ilipwe shilingi milioni 300 na kundi la WCB kwa kutumia bila ruhusa vionjo vya wimbo wake kwenye wimbo wa “Zilipendwa”  Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Mngereza ameongea yafuatayo. “Unaweza kuitazama katika mitizamo mbalimbali lakini unapoangalia kwamba wanaanza kushtakiana kimsingi ni taratibu ambayo inagusa sana mambo ya haki miliki, kabla ya kuitumia kazi ya mtu ni vizuri ukamuona mwenye kazi mkubaliane” “Ukitumia kazi ya mtu bila utaratibu hiyo moja kwa moja ni kosa, cha msingi hata kabla ya kumuweka Mwanasheria ili kudai haki yako ni vizuri ukawafata au ukawasiliana na alietumia kazi yako bila ruhusa…. katika hili linalojitokeza sasa hivi ni swala la kuamshana kwamba kazi ya sanaa ya mtu flani haina tofauti na mali ya mtu ya aina nyingine, huwezi kutumia gari la mtu bila ridhaa yake” – Mngereza

Ajali yaua na kujeruhi Moshi

Image
Watu kadhaa wanasadikika kufariki na wengine kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyotokea mchana huu mkoani Kilimanjaro ikihusisha roli na gari ndogo aina ya Noah ya abiria ya Sanya Juu - Moshi Ajali hiyo mbaya imetokea mchana  huu maeneo ya Kikavu  karibu na Kwasadala Mkoani Kilimanjaro ambapo Roli kubwa lilikuwa linajaribu kulipita gari lingine  ndipo likakutana uso kwa uso  na Gari ndogo aina ya Noah iliyokuwa imebeba abiria likitokea Moshi mjini kwenda  Sanya Juu. Taarifa kamili za ajali hiyo bado hazijatolewa lakini mashuhuda wa tukio wanasema huenda baadhi ya abiria waliokuwa kwenye Noah wamejeruhiwa. Aidha mashuhuda hao wameeleza kuwa watu wanne ndio wanaonekana kuwa bado ni majeruhi lakini hali zao ni mbaya na taratibu za kuwafikisha hospitali kwaajili ya matibabu zinaendelea. Hata hivyo bado majina ya abiria waliokuwemo kwenye Noah hayajapatikana mara moja tunaendelea kufuatilia taarifa kamili kutoka kwa kamanda wa Polisi mk...

AJALI; Wawili wafariki katika ajali wilayani Ikungi

Image
Watu wawili wamekufa papo hapo na wengine wawili wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Ikungi,kufuatia gari aina ya Toyota Landcruiser kugongana uso kwa uso na basi la Taqwa.                                                                                            Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Sigida SSP Isaya Mbughi amesema,ajali imetokea katika kijiji cha Kideka wilayani Ikungi  majira ya saa tano asubuhi na imehusisha basi la Taqwa lenye usajili wa nambat 159 CWH lilokuwa likitokea Kampala  nchini Uganda na kuelekea jiji Dar-es-Salaam ,kugongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya Toyota Landcruiser yenye usajili wa namba T 862 DJN ilyokuwa ikitokea Dodoma,na kusema chanzo cha ajali ni ...

Wema Sepetu apata pigo hili

Image
  Serikali kupitia mamlaka zake imezifungia rangi za midomo zinazozalishwa na Mwanadada aliyewahi kuwa Miss Tanzania na Muigizaji wa Filamu, Wema Sepetu. Rangi hizo zinajulikana kwa jina la "Kiss". Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) pamoja na Shirika la Viwango Nchini(TBS) wamebaini kuwa rangi hizo hazina ubora kwa matumizi ya binadamu. Kwa upande wa Meneja wa Wema Sepetu, Happy Shame alipotakiwa kuzungumzia suala hilo amefunguka na kusema kwamba taarifa za kufungiwa kwa bidhaa hizo yeye kama Meneja hajazipata bali anachofahamu mzigo ulikuwa haujaingia sokoni na kwamba muigizajin huyo alikuwa bado akifuatilia vibali kutoka mamlaka husika. Rangi hizo za mdomo za muigizaji Wema Sepetu zilizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 usiku wa birthday yake.

Watanzania 200 kupata ajira Saudi Arabia

Image
Kampuni ya Bravo Job Centre Agency Limited ya malkia wa urembo nchini Tanzania, Sitti Mtemvu imeweza kutafuta nafasi za ajira 200 kwa Watanzania nchini Saudia Arabia ambapo usahili utafanyika kesho. Sitti amesema hayo leo Uwanja wa ndege wa JK Nyerere wakati akiwapokea wawakilishi wa Kampuni ya Almarai ambayo inaratibu usahili huo.  Alisema usahili huo utafanyika nyuma ya National House Temeke, karibu na Uwanja wa Taifa ambapo usaili huo utafanyika kwa makundi hivyo wataokuwa na sifa watachukuliwa na kwenda kufanya kazi nje ya. Aliongeza kuwa watu wenye fani na sifa za udereva, upishi au daktari wanaombwa wafike kesho ili waweze kupata nafasi za ajira ambazo zitakuwa ni za haki na stahiki zote kama mfanyakazi atakuwa anazipata kupitia mkataba wake .

Shule iliyotokea mlipuko wa bomu yafungwa

Image
Uongozi wa  Shule ya Msingi  Kihinga umaamua kuifunga kwa muda shule hiyo kwa lengo la kuwajenga kisaikolojia wanafunzi wake baada ya wenzao kupoteza maisha kutokana na mlipuko wa bomu. Akizungumza  Mwananchi leo Novemba 10 ,Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Aidan Makobero amesema   shule hiyo imefungwa kimasomo hadi Jumatatu ili wanafunzi waweze kupata malezi ya  kisaikolojia Aidha amesema kwa shule jirani  ya Nyarukubala iliyo karibu na mpakani na  Burundi mahudhurio yamepungua kutoka wanafunzi 700  na kufikia 100  leo  Novemba 10 “Hata shule nyingine ya Nyarulama nayo wanafunzi wake wamepungua  baada ya tukio la shuleni kwangu na kusalia majumbani wakiogopa kwenda shule wakidai nao wanaweza kukumbwa na tukio  kama la shule jirani’’ amesema  Makobero Pia majeruhi 33 kati ya 42 waliojeruhiwa kwa bomu wameruhusiwa na kurejea makwao baada ya afya zao kuimarika Mganga wa hospitali ya misheni ya R...

Polisi wamnasa muuza risasi za kivita

Image
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia watu wawili kwa mahojiano baada ya kukamatwa na risasi za kivita ambazo wanazimiliki kinyume na sheria. Akitoa taarifa kwa Wanahabari Kamanda Mambosasa amesema kwamba Novemba 6 mwaka huu maeneo ya Serengeti Kigamboni lilipokea taarifa ya kuwepo kwa mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Willy Peter kuwa anafanya biashara ya kuuza risasi mtaani. Amesema kwamba baada ya kupata taarifa hizo Polisi walifanya ufuatiliaji na hatimaye kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na risasi 69 za kivita aina ya FN G3. Kamanda Mambosasa amefafanua kwamba baada ya  mahojiano mtuhumiwa huyo alikiri kuwa risasi hizo alipewa na mtu aliyemtaja kwa jina la Matabu William kwaajili ya kwenda kuziuza na kwamba alimpatia risasi hizo huko nyumbani kwake Kiwalani jijini Dar es salaam. Hata hivyo polisi walifika nyumbani kwa Matabu William Matoke (52) kiwalani ambapo alikiri kufanya biashara hiyo ya risasi na alipopekuliwa katika n...

Saada Mkuya amshukia Waziri wa fedha

Image
Waziri wa Fedha wa utawala uliopita wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Saada Mkuya amemshukia Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango kwa kuandaa mpango wa taifa wa maendeleo pasina kuihusisha Zanzibar. Mkuya ambaye ni mbunge wa Welezo visiwani Zanzibar amesema Dk Mpango amekuwa na kawaida ya kutokujibu hoja ambazo zinatolewa na wabunge wa kutoka Zanzibar jambo ambalo limemsikitisha. Akichangia leo Novemba 10 bungeni mjini Dodoma Mpango wa Maendeleo ya Taifa, Mkuya ambaye katika mchango wake alisikitishwa na jinsi Waziri Mpango anavyoitenga Zanzibar licha ya kuwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. “Nadhani taifa hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaundwa na pande mbili sasa Mheshimiwa Mwenyekiti  (Azzan  Zungu) cha kusikitisha na fedheha kabisa ni kuona hakuna hata eneo moja lililopangiwa mpango angalau tu likaelekezwa katika upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Mkuya “Hili niliseme wazi mheshimiwa mwenyekiti kupi...

MSHTAKIWA SETHI AIOMBA MAHAKAMA IMRUHUSU KWENDA KUPATIWA MATIBABU YA PUTO LAKE NCHINI AFRIKA KUSINI

Image
Mshtakiwa Harbinder Singh Sethi,ameoimba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumruhusu kwenda kupatiwa matibabu ya puto lake lililoisha muda nchini Afrika Kusini kwa daktari wake maalumu kwa madai ya kwamba Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamemueleza kuwa hawawezi kufanya upasuaji huo.Maombi hayo yamewasilishwa mahakamani hapo na wakili wake, Joseph Sungwa leo Novemba 10/2017 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, wakati shauri hilo linalomkabili Sethi na James Rugemarila lilipopelekwa kwa kutajwa na Mawakili wa Serikali, Vitalis Peter na Leonard Swai kudai upelelezi haujakamilika. Ili mshtakiwa aweze kuja mahakamani kuudhuria kesi yake na hatimae kuweza kujitetea, tunaomba kama inawezekana aende kumuona daktari wake ambaye anaishi Afrika Kusini kwa matibabu”, alidai Sungwa.Ombi hilo lilipingwa vikali na wakili wa serikali,Swai akidai Muhimbili haijashindwa kumfanyia upasuaji wa puto mshitakiwa huyo, bali anajicheleweshwa mwenyewe kutokana na kutaka uwep...

HAMISA MOBETTO AANGUKIA PUA KESI YAKE,MAHAKAMA YAAMUA HAYA LIVE

Image
  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Watoto imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Mwanamitindo Hamisa Mobeto dhidi ya Mwanamuzi Naseb Abdull ‘Diamond Platnum’ kuhusu matunzo ya mtoto.Uamuzi huo umetolewa leo mbele ya Hakimu, Devotha Kisoka baada ya kusikiliza hoja za pande mbili ukiwemo wa Diamond ambaye aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto. Katika uamuzi wake, Hakimu Kisoka alisema anakubaliana na hoja za upande wa mlalamikiwa kwamba kulikuwa na upungufu katika ufunguaji wa kesi hiyo.Kwa mujibu wa pingamizi lililowasilishwa na Diamond mahakama hapo, alidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi. Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa na Mobeto kupitia jopo la mawakili wake. Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine aliiomba mahakama imuamuru Diamond atoe matunzo ya mtoto waliozaa.Mobeto aliiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila mwezi ya Sh.mil 5 ambap...

Kagasheki amvaa Kigwangalla

Image
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamisi Kagasheki amemvaa Waziri wa sasa wa sasa wa wizara hiyo Mh. Hamisi Kigwangalla kwa kumtaja kuwa ana mahusiano ya karibu na Mkurugenzi wa OBC ambaye ana kashfa kubwa ya rushwa. Kupitia mtandao wake wa Twitter Balozi Kagasheki alimtaka Mh. Kigwangalla amthibitishie kuhusu ukaribu wake na Mkurugenzi huyo na kuhusu rushwa aliyowahi kupokea ikiwa ni pamoja na kuuza vitalu. Balozi ameandika "Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla alinukuliwa kutaja "muwekezaji OBC" alivo na kashfa za Rushwa. Alinitaja mimi kuwa karibu na OBC. Napenda athibitishe ukaribu huo, vitalu nilivogawa nikiwa Waziri na rushwa niliyopokea," Balozi Kagasheki Hata hivyo baada ya ujumbe huo ambao ulienda moja kwa moja kwa Waziri Kigwangalla naye alijibu ujumbe huo ambao ulielekezwa kwake na kumuomba Mstaafu huyo wayazungumze nje ya mtandao "Mhe. Balozi Kagasheki , wewe ni kaka yangu na unajua nakuheshimu ...

Mchakato Katiba Mpya, Watolewa Majibu na Waziri Mkuu

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa Changamoto za jamii ni nyingi kuliko mahitaji ya Katiba hivyo suala la katiba sio kipaumbele cha serikali kwa sasa. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Bungeni wakati wa kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, ambapo alijibu swali la Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea lililohoji kuwa ‘Serikali ya awamu ya tano imetimiza miaka miwili lakini hakuna jitihada zozote zilizofanywa katika kuendeleza mchakato wa katiba ulioachwa na Serikali ya awamu ya nne. Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amefafanua, “Katiba mpya inahitaji gharama kubwa na sisi tumeanza na kutatua changamoto za jamii kwanza, ikiwemo mahitaji ya maji, changamoto za elimu, na sekta ya Afya”. Amesema Waziri Mkuu Waziri Majaliwa ameongeza kuwa Katiba ni muongozo tu na wakati ukifika serikali yake imemaliza changamoto basi wataanza mchakato huo. “Kila bajeti ina vipaumb...