Watanzania 200 kupata ajira Saudi Arabia

Kampuni ya Bravo Job Centre Agency Limited ya malkia wa urembo nchini Tanzania, Sitti Mtemvu imeweza kutafuta nafasi za ajira 200 kwa Watanzania nchini Saudia Arabia ambapo usahili utafanyika kesho.

Sitti amesema hayo leo Uwanja wa ndege wa JK Nyerere wakati akiwapokea wawakilishi wa Kampuni ya Almarai ambayo inaratibu usahili huo.

 Alisema usahili huo utafanyika nyuma ya National House Temeke, karibu na Uwanja wa Taifa ambapo usaili huo utafanyika kwa makundi hivyo wataokuwa na sifa watachukuliwa na kwenda kufanya kazi nje ya.

Aliongeza kuwa watu wenye fani na sifa za udereva, upishi au daktari wanaombwa wafike kesho ili waweze kupata nafasi za ajira ambazo zitakuwa ni za haki na stahiki zote kama mfanyakazi atakuwa anazipata kupitia mkataba wake .

Comments

Popular posts from this blog