Posts

Gharama za kumtunza Faru Fausta kupunguzwa

Image
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imeanza kulima majani aina ya lusini ambayo ni chakula cha Faru Fausta ili kupunguza gharama za kumtunza mnyama huyo. Faru Fausta mwenye miaka 54 anahifadhiwa kwenye banda ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni hatua ya kumlinda asiliwe na wanyama wengine kutokana na jicho lake kutoona. Amekuwa akitumia bandali 250 za majani kila baada ya miezi minne yanayoigharimu mamlaka hiyo Sh5 milioni. Majani hayo hununuliwa kutoka nchi jirani ya  Kenya. Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Idara ya Malisho na Usimamizi wa Wanyama NCAA, Hillary Mushi amesema mamlaka imeandaa shamba lenye ukubwa wa eka mbili na imepanda mbege za lusini. Amesema ndani ya miezi saba majani hayo yataanza kuvunwa. Mushi amesema NCAA imechukua hatua hiyo ili kupunguza gharama za kumtunza faru huyo, ambaye amekuwa moja ya kivutio cha watalii na watafiti kutokana na kuwa ndiye faru mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani kati ya wanaoi

Tumia kitunguu swaumu ili kuzua kuwahi kufika kileleni mapema

Image
Hivi karibuni kumekuwapo na tatizo la wanaume wengi kuwahi kufika kileleni, huku kitendo hicho kikichangawa na sababu mbalimbali ikiwamo mawazo na sababu nyinginezo. Ikiwa wewe unatatizo la kuwahi kufika kileleni basi inasadikika ya kwamba kitunguu swaumu ni tiba tosha. Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na sifa zifuatazo: Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu. Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na hivyo kupunguza madhara ya kisukari. Ukivikata vipande vidogo vidogo hivi (chop), vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo kwa kitaalamu kama ‘Allicin’ ambayo ni dawa dhidi ya bakteria, na ‘Phytoncide’ ambayo

Heri ya Kuzaliwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Image
Rais John Pombe Magufuli. Siku kama ya leo, Oktoba 29, 1959, Rais John Pombe Magufuli alizaliwa. Kampuni ya Global Publishers, uongozi na wafanyakazi wote, wanakutakia heri ya siku ya kuzaliwa. Tunakuombea Mungu akulinde, akupe afya njema na kuendelea kuwatumikia Watanzania katika kipindi cha uongozi wako.

Dogo Janja Afunga Ndoa na Irene Uwoya?

Image
Msanii wa Filamu, Irene Uwoya. HABARI zilizoenea katika mitandao ya kijamii ni kwamba msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Dogo Janja, amefunga ndoa kimyakimya na mnyange wa filamu, Irene Uwoya. Baada kuenea kwa uvumi huo, mtandao wa Global Publishers ulifuatilia kujua ukweli juu ya ndoa hiyo iliyowashitua wengi. Hatua ya kwanza jana ni pale mwandishi wa mtandao alipowaendea wahariri wa Magazeti Pendwa ya Global Publishers yanayohusiana na habari za wasanii wa Bongo Muvi, Bongo Fleva na wengineo ambapo walijibu kwamba walikuwa wamemtafuta msanii Hamad Aly ‘Madee’ aliyewajibu kwamba alikuwa hajui chochote kuhusu suala hilo. Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Dogo Janja. Mambo hayakuishia hapo kwani wahariri haohao walipowasiliana na Dogo Janja alijibu kwamba na yeye hakujua kinachoendelea. Mwishoni wahariri wakamalizia kwa kuongea kwenye simu na Irene Uwoya ambapo alipopokea aliulizwa kuhusu suala hilo la kufunga ndoa na Dogo Janja.  Jibu la kwanza la mrembo hu

Nafasi za Kazi Kutoka Wizara Ya Fedha

Image
VACANCIES ANNOUNCEMENT President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat on behalf of the Ministry of Finance and Planning, invites qualified Tanzanians to fill twelve (12) vacant posts as mentioned below; 1.0 BACKGROUND 1.1 MINISTRY OF FINANCE AND PLANNING The Ministry of Finance and Economic Affairs manages the overall revenue, expenditure and financing of the Government of the United Republic of Tanzania and provides the Government with advice on the broad financial and economic affairs of Tanzania in support of the Government’s economic and social objectives. GENERAL CONDITIONS i.        All applicants must be Citizens of Tanzania of not more than 45 years of age; ii.        Applicants must attach an up-to-date Curriculum Vitae (CV) having reliable contacts; postal address/post code, e-mail and telephone numbers; iii.        Applicants should apply on the strength of the information given in this advertisement; iv.        Applicants must

MATUKIO YA SHEREHE HARUSI YA JOTI YAZIDI KUFANA USIKU HUU UKUMBI WAMLIMANI CITY,THE COMEDY WOTE NDAN.

Image

Mbunge:Bobi Wine Amekataa Fedha Milioni 29 Alizohongwa

Image
Mwanamuziki Uganda, ambaye ni Mbunge Kyadondo East , Bobi Wine amekataa fedha milioni 29 za Uganda alizohongwa na serikali ili aweze kukubaliana na mapendekezo ya kufanyia marekebisho kipengele cha katiba na kuondoa ukomo wa miaka 75 kuongoza nchi. Bobi Wine ameiamuru benki ambayo amewekewa fedha hizo kuzirudisha kwa watu ambao wameziweka na kusema kutokana na taarifa ya mawasiliano wabunge wote wa Uganda 449 wamepewa fedha hizo ili waweze kukubaliana na hoja hiyo na kuoandoa ukomo wa miaka 75 ili kuweza kumpa nafasi tena Yoweri Kaguta Museveni (73) kugombea nafasi ya Urais tena kwa awamu ya sita 2021. “Oktoba 24, 2017 Milioni 29 wa Uganda ziliwekwa kwenye Account yangu ya benki, pesa hizo walipewa wabunge wote wa Uganda kwa mujibu wa taarifa rasmi pesa hizo walizopewa wabunge ni ili kukubaliana na pendekezo la kufanyia marekebisho kipengele cha 102 (b) cha Katiba ya Uganda na kuondoa ukomo wa miaka 75 kama sifa ya kusimama kama Rais wa Uganda” alisema Bobi W

ZARI THE BOSS LADY NA HAMISA MOBETTO MAPYA TENA,WAONYWA VIKALI,WAWEKWA KITI MOTO

Image
Warembo waliokuwa kwenye vita ya maneno, Hamisa Mobeto na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wamedaiwa kuwekwa kitimoto ili waache kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii. Risasi Jumamosi limeelezwa kuwa, kwa nyakati tofauti wawili hao waliwekwa kitimoto na ndugu wa msanii wa Mzazi Mwenzao na kutakiwa waache malumbano hayo mitandaoni kwani hayaleti picha nzuri kwao na ukizingatia kosa limeshafanyika na msanii kukiri hadharani. “Walichoelezwa tu ni kwamba, waache kutupiana vijembe mitandaoni maana wao sasa hata kama hawatakuwa wake wenza lakini tayari msanii ana damu yake kwa Mobeto. Amekiri kwamba aliteleza na kujikuta ameingia kwenye uhusiano naye hadi kufikia hatua ya kupata mtoto. Zarinah Hassan. “Mtoto ameshazaliwa na ni damu ya msanii na mwisho wa siku msanii atalazimika kumpa mahitaji yake kama mwanaye hata kama yeye hataendeleza uhusiano na mama wa mtoto. Zari ni mama wa watoto wake wawili, wamedumu muda mrefu hivyo yeye ataendelea tu kushikilia usuk

Mambo 10 Utayaona Leo Uwanja wa Uhuru…Simba vs Yanga

Image
Kikosi cha timu ya Simba. . YANGA na Simba zinakutana leo Jumamosi kila moja ikiwa imepania kushinda mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Pamoja na yote, watani wanapokutana kunakuwa na burudani nyingi sana ambazo zinatofautisha aliye uwanjani na atakayeangalia katika runinga. Kwenye Uwanja wa Uhuru, idadi ya mashabiki wanaotakiwa kuingia ni 23,000 tofauti na 60,000 kwenye Uwanja wa Taifa. Pia kumbuka mechi hii ya watani inarejea kwenye uwanja huo baada ya kipindi kirefu. Kutakuwa na mengi ambayo yatajitokeza ndani na nje ya uwanja, lakini nakupa 10 tu ambayo kwa asilimia 90 utayaona. Kikosi cha timu ya Yanga Wasio na tiketi: Watu watajitokeza wengi zaidi kuliko idadi ya wale walio na tiketi na watajazana nje ya uwanja na kusababisha kero kubwa nje ya uwanja. Bado kuna tabia ya watu kuamini kuwa wanapokwenda uwanjani kuna nafasi ya kuingia angalau kwa njia za mkato. Hivyo hawatakubali kuondoka mapema badala yake watae

SHAHIDI AELEZA WALIVYOAHIDIWA MAMILIONI KWAJILI YA KUMUUA BILIONEA MSUYA

Image
Mahakama Kuu Kanda ya Moshi imeelezwa kuwa washtakiwa katika kesi ya mauaji ya bilionea Erasto Msuya waliahidiwa kulipwa Sh17 milioni kila mmoja. Hayo yamo katika maelezo ya mshtakiwa wa saba, Ally Mussa Majeshi yaliyosomwa mahakamani na shahidi wa 10 wa upande wa mashtaka, Sajini Atway Omary baada ya kupokelewa kama kielelezo.Maelezo hayo yalisomwa baada ya Jaji Salma Maghimbi anayesikiliza kesi hiyo, kutoa uamuzi mdogo wa kukataa pingamizi la upande wa utetezi kupinga maelezo hayo yasipokelewe kama kielelezo.Jopo la utetezi linaloundwa na mawakili Hudson Ndusyepo, Majura Magafu, Emmanuel Safari na John Lundu walikuwa wakipinga wakisema mshtakiwa aliyatoa baada ya kuteswa na polisi. Baada ya kutupilia mbali pingamizi hilo na kuungana na hoja za mawakili wa Serikali, shahidi huyo wa 10 akatakiwa kuyasoma maelezo hayo neno kwa neno. Akisoma maelezo hayo, shahidi huyo ambaye ndiye aliyeyaandika katika Kituo cha Polisi Kigoma Oktoba 5, 2013, alisema mshtakiwa alimw

Jaji Warioba ashauri Viongozi wakutane na Wazungumze

Image
Waziri Mkuu wa zamani, Joseph Warioba amewataka viongozi wa kisiasa kujenga utamaduni wa kukutana wanapogundua kuna matukio yanayoashiria uvunjifu wa amani. Jaji Warioba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba amesema waasisi wa Taifa walijenga umoja na misingi ya maendeleo ambayo kuna dalili ya kutoweka. Amesema hayo leo Alhamisi Oktoba 26,2017  jijini Dar es Salaam akifungua mdahalo wa mashauriano juu ya kuhamasisha, kusisitiza, kulinda na kudumisha amani, umoja na maridhiano nchini. Amesema viongozi wa dini wamekuwa na kawaida ya kukutana wanapoona mambo hayaendi sawa jambo ambalo ni zuri na linapaswa kuendelea. Jaji Warioba amesema kuna viashiria vya kutoweka kwa amani na viongozi wa kiserikali na kisiasa wanapaswa kuiga kile wanachofanya wenzao wa dini. "Amani ikitoweka kuirudisha ni shida au kuiendeleza. Viongozi hasa hawa wa kisiasa wawe wepesi kukutana na kuzungumza, tuache malumbano na hasa viongozi wa kisiasa

MASKINI LULU,MANGE KIMAMBI AMSHAMBULIA MTANDAONI KUHUSU KESI YAKE

Image
Mnajua watanzania mna double standards sana! Juzi juzi a lot of you mlikuwa mnamsapoti Magu kuwafukuza shule watoto wanaopata mimba wakiwa shule, kina Mange tukawa tunawatetea kuwa wale ni Watoto hawaju wafanyalo nyinyi mkawa mnasema kama wameweza kuvua chupi sio watoto acha wafukuzwe ila leo kwa Lulu mnasema alikuwaga mtoto Kanumba alikuwaga anambaka. Mnaona jinsi mnachekesha? Watoto wa maskini kufukuzwa shule sababu ya mimba sio Watoto ila mtu maarufu kuuwa bila kukusudia mnasema ni mtoto, so stupid. . Anyways, let me be truthful why nimeshindwa kuwa na huruma na Lulu au upande wa Lulu. Sababu ni jinsi tu alivyoishi her life the last 5 years. Hakuonyesha hata chembe ya regret for what happened.Mostly hakuwa na huruma na familia ya marehemu. Lulu alitakiwa afikirie kuwa yeye ndio sababu Kanumba hayupo duniani leo, angeonyesha ubinadamu na utu kwa kumsaidia mama wa marehemu ambae alikuwa anamtegemea mwanae kwa kila kitu. Angalau angeonyesha remorse kwa kumjali yul

Mwakyembe Kuivaa Kampuni Iliyomdhurumu Mil.25 Mzee Majuto

Image
WAZIRI wa Habari,  Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amefunguka na kusema kuwa Mzee Majuto amedhurumiwa pesa milioni 25 na kampuni ya filamu ambayo jina lake amelihifadhi na kudai atatumia hata mshahara wake kuhakikisha anawafunga watu hao.  Mwakyembe amesema hayo leo Oktoba 27, 2017 alipokutana na wasanii mbalimbali kujadili changamoto za kazi ya sanaa nchini na kusema katika vitu ambavyo atapambana navyo ni pamoja na watu wanaowadhurumu wasanii haki yao na kuwaibia kazi zao za sanaa.  “Nilipopita Tanga nilikutana msanii nguli wa filamu Mzee Majuto nilikwenda kumjulia hali na bahati nzuri saizi anaendelea vizuri, Mzee Majuto akaniomba kitu kimoja na kuniambia naumwa nahitaji pesa lakini nimeshafanya kazi na kampuni hii akanionyesha na kuwa ameshatengeneza filamu zaidi ya 100 na kampuni hiyo kwa mkataba wa kulipwa fedha ndogo tu shilingi milioni 25. “Lakini huu ni mwaka wa  pili hajalipwa hata senti tano sasa hayo ndiyo mambo ambayo sifurahii, nimeshapeleka taarifa kwa

WANAWAKE MIL 14 HUUGUA SARATANI YA MATITI KILA MWAKA DUNIANI

Image
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt Julius Mwaiselage Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt Julius Mwaiselage amesema kuwa tatizo la saratani limekuwa likiongezeka siku hadi siku duniani kote na takwimu zinazotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni [WHO] zinaonyesha kwamba kila mwaka wagonjwa wapya milioni 14.1 hugundulika na wagonjwa milioni 8.8 hufariki dunia. Ugonjwa wa Saratani ya Matiti Unavyoonekana Ameyasema wakati wa mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akizungumzia matembezi ya hisani ya kuhamasisha uchunguzi mapema wa saratani ya matiti inayotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu. Ameongeza kuwa taasisi yao kwa kushirikiana na Hoteli ya Kunduchi Beach na Hospitali ya Aga Khan ndiyo imeandaa matembezi yatakayoanzia Ocean Road saa 12.30 asubuhi na kuhitimishwa saa 4.00 katika taasisi hiyo ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

JPM Abadili Maamuzi kwa Wakuu wa Mikoa Wawili Baada tu ya Kuwaapisha

Image
RAIS John Magufuli amewataka Mkuu wa Mkoa wa Dodoma aliyeapishwa leo, Bi. Christine Mndeme ahame kituo na kwenda kufanya kazi kama Mkoa wa Ruvuma huku akimtaka Mkuu wa Mkoa Ruvuma, Mahenge ahamie Mkoa wa Dodoma. Rais ametoa agizo hilo mara baada ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu wa Wizara na Manaibu katibu wakuu aliowateua jana baada ya kufanya mabadiliko machache katika safu yake ya uongozi. “Mkuu wa Mkoa wa Dodoma mpya, Christine Mdemi atakuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma badala na Dkt. Binilith Mahenge atakwenda Dodoma,” alisema Magufuli. Aidha Rais amewataka Wakuu wa Mikoa wapya, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu wapya wakashirikiane na viongozi wengine kwenye maeneo yao kutatua shida za wananchi na kutengeneza mikakati ya kukuza uchumi katikamaeneo yao ya kazi. “Kila mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya akaangalie matatizo yaliyopo na kitu gani anaweza kufanya kuongeza uchumi wa eneo lake,” alisisitiza Rai Magufuli. Pia ametoa onyokwa watendaji watakao

Mganga Mkuu Afunguka Kuhusu Vifo vya Watoto Wachanga 9

Image
Mganga Mkuu Mkoa wa Arusha Dkt. Wonanji Timoth amekanusha taarifa za kufariki kwa watoto 9 waliokuwa kwenye Incubator kutokana na katizo la umeme hapo jana hospitali ya Mt. Meru, na kusema kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote. Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Dkt. Timoth amesema kwamba watoto waliofariki walikuwa wanne na sio 9 kama inavyoelezwa kwenye taarifa iliyosambaa mitandaoni, na wamefariki kwa matatizo mengine lakini sio kukatika kwa umeme. Dkt. Timoth ameendelea kwa kueleza kwamba moja ya sababu iliyofanya watoto hao kufariki ni mama kuchelewa kufika hospitali kujifungua kwa kuwa alijifungulia nyumbani, pamoja na hatari kubwa wanazopata watoto njiti.

Matukio yaliyojiri ikiwa ni pamoja na babu abebwa mgongoni kwenda kupiga kura kenya

Image
Leo tarehe 26 Oktoba, 2017 Taifa la Kenya limefanya uchaguzi wa Rais, ambapo kiongozi wa vyama vya upinzani nchini humo, Raila Odinga amesusia uchaguzi huo. Rais Uhuru Kenyatta akipiga kura mapema leo jijini Nairobi katika Shule ya Msingi Mutomo Hadi sasa taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari nchini humo zinaeleza kuwa mtu mmoja amshauawa kwenye vurugu zilizotokea mjini Kisumu na wengine 20 wakijeruhiwa kwenye vurugu zilizoongozwa na wafuasi wa vyama vya upinzani. Misururu mirefu ya wapiga kura, katika shule ya msingi ya Kayole One, Embakasi Central jijini Nairobi Wafuasi wa upinzani wakiweka magogo katikati ya barabara mjini Migori Jaji Mkuu nchini Kenya, George Maraga akipiga kura mapema leo katika shule ya msingi ya Bosose, Nyamira Rais wa zamani wa Kenya, Mwai Kibaki akipiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Munaini, Othaya. Mpiga kura akiwa na Babu yake mgongoni akimpeleka kupiga kura katika kituo cha shule ya msingi Kaare Kaunti ya Thar