Posts

Waziri Lukuvi: "Bomoabomoa hainihusu"

Image
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amefunguka na kusema zoezi la bomoabomoa linaloendelea jijini Dar es Salaam katika maeneo ya Kimara na Kibamba yeye halimuhusu hivyo awataka watu wamuulize Waziri wa ujenzi, uchukuzi Waziri Lukuvi alisema zoezi linaloendelea Kimara na Kibamba ni sheria ya barabara ndiyo inayofanya ile kazi na siyo yeye na kuwataka watu wamtafute Waziri husika ili aweze kuwapa maelezo juu ya jambo hilo. "Hapana siwezi kuzungumzia hilo nenda kamuone Waziri wa Ujenzi kwani Sheria ya barabara ndiyo inayofanya ile kazi siyo mimi hivyo siwezi kuzungumza lolote kwenye hilo jambo kwani mimi bomoabomoa hiyo hainihusu, kwani kila mtu anaapa kwa kipande chake na mimi siyo Waziri wa jumla, Waziri wa jumla ni Waziri Mkuu" alisema Lukuvi  Aidha Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimelaani vikali zoezi la bomoabomoa linaloendelea katika maene

Taarifa muhimu kwa wote walioomba na watakaoomba kazi Serikalini

Image
Mtakumbuka Serikali katika mwaka wa fedha uliomalizika 2016/2017 iliahidi kutoa Ajira serikalini zaidi ya 52,000 kwa Watanzania, ambapo katika siku za hivi karibuni Serikali imekuwa ikitoa vibali vya kuajiriwa watumishi wa kada mbalimbali ikiwemo Waalimu wa Sayansi, Kada za Afya na maeneo mengine kulingana na mahitaji. Kama mnavyofahamu mojawapo ya jukumu la msingi la kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni pamoja na kuendesha mchakato wa ajira kwa niaba ya waajiri mbalimbali na hatimae kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi wanaofaulu usaili, ambapo tangu Serikali ilipoanza kutoa vibali baada ya kusitishwa tumeshapokea jumla ya vibali kwa ajili ya mamlaka za Ajira 239, kati ya hivyo vipo ambavyo vimeshafanyiwa kazi na vingine mchakato wake unaendelea katika hatua mbalimbali. Aidha, baadhi ya vibali ambavyo mchakato wake umeshakamilika ni pamoja na  kibali cha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambayo tulipokea jumla ya  maombi ya kazi 6,8

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 25.08.2017

Image

MAGAZETI YA UDAKU LEO

Image
  

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image

RAIS MAGUFULI ASEMA NIMEAMUA KUPAMBANA NA RUSHA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli amesema kuwa Tanzania ikifanikiwa kuondoa rushwa angalau kwa kwa asilimia 80 nchi itafanikiwa kuondoa matatizo mengi. Rais Magufuli ameyazungumza hayo leo hafla ya kuwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es salaam akiwemo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU. “Tukifanikiwa kupunguza rushwa angalau kwa asilimia 80 nchi ittafanikiwa kuondoa matatizo mengi, na ni vema mtambue kuwa hatua hizi tunazochukua zimeanza kuwavutia wafadhili wengi na wawekezaji,” “Na mimi kama kiongozi wenu nimeamua kupambana na rushwa kikweli kweli na ninawaomba nyote mshirikiane kuondoa rushwa katika maeneo yenu ya kazi,” amefafanua Rais Magufuli.

RAIS MAGUFULI ATAJA KITU KINACHOMKERA TAKUKURU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameelezwa kutoridhishwa na taratibu za uchunguzi na uendeshaji wa mashitaka ya rushwa zinavyochukua muda mrefu na ametoa wito kwa viongozi wa TAKUKURU kufanyia kazi eneo hilo ili vita dhidi ya rushwa ionekane ikizaa matunda haraka. Rais Magufuli ameyazungumza hayo leo hafla ya kuwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es salaam akiwemo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU. Hata hivyo Rais Magufuli ameipongeza TAKUKURU kwa kazi wanayoifanya lakini huku akitaka juhudi ziongezwe zaidi ili watu wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa vya kutoa na kupokea rushwa washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.

NDOA YA MISS TANZANIA, MTOTO WA MAKAMBA… USIPIME!

Image
Victoria Martin na Thuwein Makamba. DAR ES SALAAM: Ni historia! Harusi ya Mrembo aliyetinga Top Five ya Miss Tanzania 2007, Victoria Martin na mtoto wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, Thuwein Makamba imeacha gumzo la aina yake kutokana wawili hao kuangusha sherehe baa’kubwa. NI TANGA Wawili hao walifanya tendo hilo jema kwa Mwenyezi Mungu, Ijumaa iliyopita mkoani Tanga ambapo waalikwa waliizungumzia kama ni ndoa ya kihistoria kwani kwa kipindi hiki, haijawahi kufungwa ndoa na watu kunywa, kula hadi kusaza kwa kiasi hicho. CHANZO KINAIFUNGUKIA Chanzo makini ambacho kilianza kushuhudia sherehe za wawili hao kuanzia send off hadi harusi, kilisema matukio hayo yote yalipambwa na kufuru ya vinywaji na vyakula kiasi ambacho kila aliyeingia ukumbini alitoka akiwa nyang’anyang’a. “Yani kwa kipindi hiki cha Magu (Rais Dk John Pombe Magufuli) sherehe kubwa kuandaliwa kwa kiwango hiki ni tukio la aina yake maana watu kwa kweli hawa

MZEE MAJUTO: BADO NAUMWA JAMANI

Image
Mzee Majuto. Ikiwa ni siku chache tangu muigizaji mkongwe,  Amri Athman Amri ‘King Majuto’ kupata unafuu kufuatia upasuaji aliofanyiwa kutokana na tatizo la ugonjwa wa ngiri (hernia), hali yake bado haijatengemaa na anatumia muda mwingi kulala, Amani limezungumza naye kwa tabutabu. Jumatatu ya wiki hii, mwandishi wetu alimpigia simu mzee huyo kwa lengo la kumjulia hali na kufanya naye mazungumzo mengine, lakini King Majuto alisikika kwa shida na kudai amelala na anahitaji muda mwingi wa kupumzika na kwamba bado anaumwa na anasikia maumivu makali. Hata hivyo, mwandishi aliendelea kumdadisi kwa kina ili kujua ni nini hasa kinachoendelea kumsumbua kwani kama ni tatizo la awali alishafanyiwa upasuaji, ambapo aligoma kabisa kuendelea na mazungumzo na kugeuka ‘mbogo’ kwa muda kwa madai ya kutopenda mazungumzo na wanahabari. “Bado nimelala jamani na sijui unataka nini tena? Naumwa na ninasikia maumivu sana na sitaki kuzungumza zaidi maana nimechoka, elewa

TFF Yaomba Radhi kwa Makosa ya Uandishi Ngao ya Jamii

Image
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeomba radhi wanafamilia wote wa mpira wa miguu nchini kutokana na makosa ya kiuandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho wa Ngao ya Jamii iliyotolewa Jumatano Agosti 23, 2017 kwa klabu ya Simba. Ngao hiyo ilitolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha timu za Simba SC na Yanga SC zote za Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo, Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Yanga na kutwaa ngao hiyo. Makosa yaliyoonekana katika ngao hiyo ya jamii ni kukosewa kuandikwa kwa neno “SHIELD” ambapo liliandikwa “SHEILD” na hivyo kupoteza maana yake ya msingi. Katika taarifa ya TFF iliyotolewa leo Agosti 24 wamesema kwamba “Watanzania hususani wanafamilia ya mpira wa miguu popote pale, TFF hatujapokea vizuri mwonekana wenye makosa kwenye Ngao hiyo ya Jamii kama ambavyo wadau hawajapokea vema suala hili.” Kuonyesha kukerwa na uzembe huo uliofanywa na baadhi ya viongozi wake, Kaimu K

MIMBA YA ‘MATAMBARA’ YAMUUMBUA HUSNA

Image
Husna Maulid. MIMBA ya Husna Maulid ilikuwa ya  kughushi.  Imemuumbua baada ya kugundulika kuwa hakuwa nayo, badala yake alikuwa akiweka matambara tumboni kuonesha ana mimba. Kwa  mujibu chanzo makini, Husna hakuwa na mimba, lakini alikuwa akiweka matambara hayo kwa ‘utashi’ wake ili aonekane tu ana ujauzito lakini hakuwahi kuwa nayo. “Nilikuwa  na MIMBA ya kughushi aliyokuwa akiiweka Video Queen wa Bongo, Husna Maulid imemuumbua baada ya kugundulika kuwa hakuwa nayo, badala yake alikuwa akiweka matambara tumboni kuonesha ana mimba. ninashangaa sana kwa nini Husna, alikuwa akiweka matambara ili aonekane ana mimba kitu ambacho wengi waliamini hivyo,” kilisema chanzo. Gazeti hili lilimtafuta Husna ili kuzungumzia ishu hiyo ambapo badala ya Husna kujibu hoja, aliangua kicheko na kusema yote ni ya walimwengu. “Daah sijui nizungumzeje hiyo ishu maana yote ni ya walimwengu bwana wee yaache si unajua tena mjini hapa,”  alisema Husna.

MAJI YA MOTO YALIVYO NA FAIDA MWILINI

Image
KUNA tiba nyingi za kitabibu zilizogawanyika katika makundi mbalimbali. Kuna zile za hospitali ambazo ni lazima zinunuliwe, lakini kuna tiba ambazo kwa ushauri wa daktari hata wewe unaweza kuziandaa bila kutumia gharama kubwa. Moja ya tiba hizo ni kunywa maji ya moto. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, maji moto yanatibu magonjwa mengi ikiwemo figo, kutoa sumu mwilini na kuyeyusha mafuta tumboni. Pia hurahisisha mzunguko wa damu, huondoa sumu kwenye ubongo na kusafisha haja ndogo. Kunywa maji ya moto kila unapotaka kwenda kufanya kazi ya nguvu au mazoezi iwe kama kinga na inashauriwa kila siku unywe glasi nane ili kutoa taka na kila kisichotakiwa kubaki mwilini, kupitia jasho. Wataalamu wa afya wanasema kuwa ni vyema pia kunywa maji ya moto yenye ndimu au limao kabla ya kifungua kinywa ili kurahisisha mfumo wa mwili kwa siku nzima. Mwinyimvua Pazi, Mtaalamu wa Chakula na Lishe kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anasema kuwa maji yanarahisisha uyeyushaji wa chakula

Paparazzi Maarufu Akutwa Amejinyonga

Image
Mwili wa marehemu ukiondolewa eneo la tukio. Wakazi wa Chalinze na vitongoji vyake mkoani hapa, Jumatano iliyopita walikumbwa na simanzi baada ya paparazzi na mpiga picha wao maarufu, Mogela Msimbe kukutwa amejinyonga kwenye nyumba iliyokuwa ikiendelea kujengwa muda mfupi baada kuaga kuwa anakwenda kushuhudia tukio la wapenzi wawili waliodaiwa kunasiana wakizini ambalo nalo lilidaiwa kutokea siku hiyo. Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliyekataa kutaja jina lake, alisema siku ya tukio marehemu ambaye alikuwa mpiga picha na mwandishi wa habari wa kujitegemea alionekana kuwa na mawazo mengi lakini ghafla zikasambaa taarifa kuwa kuna mwanaume na mwanamke ambao walizisaliti ndoa zao na kwenda kujivinjari gesti, walinasiana wakiwa katika tendo la usaliti. Uvumi huo ulisambaa kwa kasi eneo hilo na kusababisha umati kujazana Kituo cha Afya cha Chalinze, mkoani hapa ambapo watu hao walionasiana walidaiwa kupelekwa kwa ajili ya huduma ya

Mwili wa mwanaharakati wa Tembo kuagwa leo

Image
Wayne Lotter enzi za uhai wake. MWILI wa mwanaharakati wa kupinga ujangili na biashara haramu ya meno ya tembo wa nchi za Afrika Wayne Lotter, aliyepigwa risasi na kuuawa jijini Dar es Salaam Jumatano iliyopita unatarajiwa kuagwa leo katika viwanja vya Baobao Villlge Masaki jijini Dar. Wayne ambaye alikuwa mwanzilishi wa PAMS Foundation, taasisi ambayo imekuwa katika mstari wa mbele kusaidia kupambana na uwindaji haramu na biashara ya pembe za ndovu nchini Tanzania aliuawa na watu wasiofahamika Agosti 16 mwaka huu wakati anatoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere akielekea nyumbani kwake Masaki. Akizungumza na wana habari kwa niaba ya wana familia, jana Krissie Clark alisema wanatarajia kuuaga mwili wa mwanaharakati huyo leo kisha kuusafirisha kwenda nyumbani kwao Afrika Kusini kwa maziko. Alisema kuuawa kwa Wayne hakutawafanya kurudisha nyuma mapambano dhidi ya ujangili na badala yake wameelekeza nguvu zao katika Afrika ili kutokomeza kabisa ujangili kama ili

Daktari Feki Aliyenaswa Muhimbili, Adakwa Tena Hospitali ya Amana

Image
Daktari ‘feki’ Abdallah Juma akiwa chini ya ulinzi wa Askari Polisi waliofika katika hospitali hiyo mara baada ya kupata taarifa. Mkazi  wa  jiji la Dar es Salaam, Abdallah Juma aliyewahi kukamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akidaiwa kujifanya daktari amenaswa tena katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa kufanya kazi katika hospitali hiyo wakati sifa za udaktari hana. Juma amenaswa leo ndani ya Hospitali ya Amana, majira ya mchana, akijifanya daktari, baada ya kuwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo. Kukamatwa kwa Juma  kunakuja ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tokea Juni 19 mwaka huu alipo kamatwa katika hospitali ya Muhimbili kwa kujifanya daktari. Katika hospitali ya Muhimbili kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu  huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amana,Zainab Hoti akizungumza waandishi habari juu

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete afurahia mavuno Shambani Kwake Chalinze

Image
Rais mstaafu wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete ameendelea na kuwekeza nguvu zake katika kilimo wakati huu ambao amestaafu majukumu yake ya Urais. Rais Kikwete kutumia ukurasa wake wa instagram amepost picha nne akiwa shambani kwake Msoga Chalinze katika shamba la mahindi wakivuna, Rais mstaafu Kikwete alikuwa akivuna na mkewe Mama Salma Kikwete.