FAHAMU MADHARA YA KUTOBOA PUA, MDOMO NA ULIMI!
Katika zama hizi za utandawazi na muingiliano baina ya tamaduni zetu za asili na tamaduni za kimagharibi, imekuwa ni kawaida kwa vijana wa rika tofauti na jinsia zote kutoga ulimi, mdomo, kitovu ama kivimbe cha nyusi kwa sababu tofauti tofauti sana. Hivyo basi, ni muhimu sana kufahama ukweli kuhusu faida ama hasara za kutoga ulimi ama mdomo kabla hujatekeleza azma yako ya kutoga viungo hivi vya mwili. Kutoga Ulimi ama Mdomo kunaweza kukusababishia madhara yasiyotarajiwa. Matokeo mazuri zaidi ya kutoga ulimi ama mdomo ni kutokutokea kwa kidonda ama kivimbe, wakati matokeo mabaya kutokea kwa baadhi ya watu ni pamoja na kuvunjika kwa meno/jino, kuvuja kiasi kikubwa cha damu, ama maambukuzi ya bakteria kwenye kidonda. Kutoga ulimi hujumuisha kutumika kwa sindano inayopenyezwa katikati ulimi ili kupitisha na kuhifadhi kipini, ama ndoana ama hereni ya urembo. Kazi hii ya kutoga ulimi mara nyingi ganzi huwa haitumiki. Baada ya kutoga, kuvimba kwa ulimi na maumivu ya m