Posts

Viongozi wawili wa serikali wauawa Kwa Kupigwa Risasi Kibiti

Image
Viongozi wawili wa serikali za mtaa katika Kijiji cha Mangwi wilayani Kibiti mkoani Pwani wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumatano, Juni 28. Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga zimeeleza kuwa waliouawa ni Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi, Shamte Makawa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus. Aidha, kamanda wa polisi amesema kuwa tayari askari wamekwenda eneo hilo kwa ajili ya hatua zaidi. Hadi sasa watu zaidi ya 37 tayari wameuawa katika mfululizo wa matukio ambayo bado Polisi hawajafahamu ni nani mhusika na lengo haswa la kufanya hivyo.

Rais Wa TFF Na Katibu Wake Watiwa Mbaroni

Image
Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wanashikiriwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wapo katika Kituo cha Polisi Salander Bridge ili kupisha uchunguzi dhidi yao.  Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba alipokuwa akihojiwa na kituo cha Radio EFM leo. Misalaba amesema ni kweli wanawashikilia na taarifa zaidi wataitoa baada ya kumaliza uchunguzi wao. Licha ya kuwa tuhuma zinazowakabili hazijawekwa wazi, lakini mwezi uliopita ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliripoti kuhusu mabilioni ya shilingi yaliyobainika kuchotwa kwenye akaunti za TFF na kulipwa kwa wadau wa soka kinyume cha sheria. Miongoni mwa waliotuhumiwa kunufaika na fedha hizo ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi na aliyekuwa msaidizi wake, Juma Matandika. We

MBUNGE WA CHADEMA ASIMAMISHWA KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE

Image
Siku kadhaa zilizopita kutoka Bungeni Dodoma Wabunge wa CHADEMA Halima Mdee wa Kawe na Ester Bulaya wa Bunda Mjini walisimamishwa kutohudhuria vikao vya Bunge, leo June 28, 2018 Mbunge Conchesta Rwamlaza wa Viti Maalum CHADEMA amesimamishwa. Conchesta Rwamlaza amesimamishwa kutohudhuria Vikao vitatu vya Bunge linaloendelea kwa kosa la kusema uongo mbele ya Bunge akimtuhumu Mbunge wa Muleba Kusini Prof. Anna Tibaijuka kujimilikisha ardhi yenye ukubwa wa ekari 400 kinyume cha sheria taarifa ambazo sio za kweli. Aidha, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imetoa msamaha kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari kwa kosa alilolifanya May 30, 2017 kudharau mamlaka ya Spika ikiwemo kupiga kelele Bungeni na kutupa karatasi ovyo. Nassari amepata msamaha huo kwa kuwa imeonesha ni mara yake ya kwanza kutenda kosa kama hilo kisha kupelekwa mbele ya Kamati.

Kafulila afunguka haya kuhusu Escrow

Image
DAR ES SALAAM: WAKATI gumzo nchi nzima likiwa ni wizi mkubwa ambao haujawahi kufanyika wa zaidi ya shilingi bilioni 300 kutoka akaunti iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ya Tegeta Escrow, imeelezwa kuwa baadhi ya wabunge walikuwa wakihatarisha maisha yao na wengine wamepoteza ubunge kwa sababu ya kupinga ufisadi huo. Vinara wa kufichua sakata hilo, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, David Kafulila na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ndiyo waliofichua mambo hayo kwa nyakati tofauti. Kafulila aliyehojiwa na gazeti hili wiki iliyopita alisema kundi lao la kupiga vita ufisadi huo lilikuwa hatarini kwa sababu kuna fedha zilikuwa zinatumika ili kuzima wizi huo. Marehemu Deo Filikunjombe (ushoto), Davidi Kafulila, Zitto Kabwe pamoja na David Silinde. “Hata wenzetu wabunge walikuwa wakitupinga na kwa kweli tulikuwa katika wakati mgumu, hata hivyo, hatukuacha kupigania jasho la umma ambalo lilikuwa limeliwa na watu wachache,” alisema Kafulila. Alisem

BABU KIKONGWE WA MIAKA 80 AISHI KWA KULA UDONGO

Image
  Katika hali ya kushangaza na kusikitisha sana, kikongwe mmoja aitwaye Athuman Ngusa Kulaba (80) amekuwa akiishi kwa kula udongo wa nyumba anayoishi kwa sababu ya kukosa chakula cha kibinadamu. Kikongwe huyo alikutwa na Uwazi hivi karibuni nyumbani kwake, Chanika wilayani Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam baada ya majirani kusema kwamba wamekuwa wakimshuhudia akipata mlo huo kwa karibu mwaka mmoja sasa. Baada ya kuona hali yake inazidi kuwa mbaya, mjumbe wa eneo hilo, John Kanguya na majirani  zake walimchukuwa hadi kwenye Kituo cha Afya cha Chanika kwa ajili ya kumpima afya yake ambapo madaktari walisema tayari alipatwa na ugonjwa wa safura ambapo tumbo lake limejaa minyoo. Uwazi lilishuhudia sehemu kubwa ya ukuta wa nyumba anayoishi kikongwe huyo ikiwa imemeguka kwa ajili ya kuchimbuliwa na kuliwa. Majirani walilieleza Uwazi kwamba, nyumba anayoishi kikongwe huyo aliachiwa kuilinda na mtu aliyetajwa kwa jina moja la Musada karibu miaka 20 iliyopita

Njia hizi 16 za kuondoa Sumu Mwilini

Image
NJIA 16 ZA KUONDOA SUMU MBALIMBALI MWILINI Mwili unaweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika na mwili kwa namna mbili, ama kupitia mazingira tunayoishi (viwanda, migodi nk) au kupitia vyakula na vinywaji ambavyo tunatumia kila siku. Sumu au taka pia zinaweza kuingia mwilini kupitia dawa mbalimbali hasa za kizungu tunazotumia kujitibia magonjwa mbalimbali. Mwili huzalisha hizi sumu au takataka (free radicals) kila mara kunapofanyika mmeng’enyo wa chakula mwilini mwako. Ishara zitakazokuonyesha mwili wako una sumu nyingi: -Uchovu sugu -Maumivu ya maungio -Msongamano puani -Kuumwa kichwa kila mara -Tumbo kujaa gesi -Kufunga choo au kupata choo kigumu -Kukosa utulivu -Matatizo mbalimbali ya ngozi ikiwemo chunusi -Pumzi mbaya -Mzunguko wa hedhi usio sawa -Kuishiwa nguvu -Kushindwa kupungua uzito -Kupenda kula kula kila mara Njia 16 za kuondoa sumu mbalimbali mwilini 1. Fanya mlo wako mmoja wa siku kuwa ni matunda pekee Amua moja ya mlo wako kw

MH.LOWASSA AWASILI MAKAO MAKUU YA POLISI LEO DAR KWA MAHOJIANO

Image
WAZIRI Mkuu Mstaafu na mgombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa, amewasili katika Makao Makuu ya Polisi jijini Dar saa nne kama alivyotakiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI). Lowassa alikuwa amefuatana na magari manne ya msafara wake pamoja na magari mawili ya polisi wenye siraha. Kabla ya kuwasili kwa Lowassa, aliyetangulia mapema leo alikuwa katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Mashinji aliyewasili kuhakikisha anaweka sawa maswala ya kisheria na msaada wowote utakaohitajika. Waandishi wa habari hawakuruhusiwa kusogea eneo la tukio kwani ulinzi umeimalishwa. Jana Edward Lowassa alipokea wito wa kumtaka aonane na DCI leo saa nne bila kukosa.

HII NDIO KAULI YA JUX BAADA YA KUMALIZA MASOMO YAKE

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Jux amesema haikuwa kazi rahisi hadi yeye kumaliza masomo yake ya elimu ya juu nchini China. Muimbaji huyo amesema kuwa katika miaka mitano aliyosoma kuna wakati alikuwa anakosa mitihani kwa sababu ya show lakini anaishukuru familia yake kwa kuwa karibu na yeye. “It’s not easy at all lakini nashukuru sana rafiki zangu ambao wamenizunguka, familia yangu ni watu ambao walikuwa wananipa sana moyo, walinieleza kila kitu kinawezekana usikate tamaa, naweza nikamaliza nikafanya vitu vyote, naweza nikafanya biashara, muziki na kusoma pia,” Jux ameiambia XXL ya Clouds FM. “Namshukuru Mungu nimemaliza leo, so kila kitu kinawezekana naweza nikakuambia muda wako tu unavyoupanga na changamoto zipo nyingi, kushindwa sio tatizo ila hutakiwa kuacha. Kuna mitihani kama miwili hivi nakumbuka nilikuwa nipo Bongo nina show wenzangu wakafanya lakini nilikuja nikarudia, so changamoto kama hizo zinapatikana na inabidi vitu vyote viende kwa wakati

Penny Afungukia Ujauzito Wake

Image
Pennieli Mungilwa.  MTANGAZAJI wa Kipindi cha Harusini kinachorushwa kupitia DSTV, Pennieli Mungilwa amefunguka kuumizwa na uzushi unaosambaa kuwa amenasa ujauzito kitu ambacho kinahatarisha uhusiano wake wa kimapenzi. Akizungumza na Star Mix , Penny alisema kuwa, jambo la mimba ni la heri lakini lazima lisemwe kwa ukweli siyo kuzusha kwa sababu linaleta matatizo makubwa sana kwa mtu ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mtu mwingine. “Yaani sina ujauzito wa mtu yeyote yule na hakuna mtu mbaye hapendi kupata lakini kwa mtu sahihi na wakati muafaka sasa mimi watu wakinibambika hilo wananiletea shida pia kwenye uhusiano wangu nilionao,” alisema Penny. Na Imelda Mtema | Ijumaa | Star Mix

Prof, Muhongo aibuka ajibu tuhuma

Image
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amesema hahusiki na mikataba yote ya madini. Muhongo alitoa maelezo hayo jana, ikiwa ni siku moja baada ya Nipashe kuripoti kutoonekana kwake bungeni bila ruhusa ya Spika. Aidha, Prof. Muhongo aliidokeza Nipashe chanzo cha kutokuwapo kwake katika chombo hicho cha kutunga sheria kwa wiki tano sasa. Baada Gazeti la Nipashe  jana liliripoti kuhusu kutoonekana bungeni kwa Mbunge huyo wa Musoma Vijijini (CCM) bila ruhusa ya Spika tangu uteuzi wake katika baraza la mawaziri utenguliwe wiki tano zilizopita. Katika ripoti hiyo ya jana, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alisema ofisi yake haina taarifa za mtaalamu huyo wa kimataifa wa jiolojia na haijui aliko tangu alipoachishwa nafasi ya uwaziri, muda mfupi baada ya Rais John Magufuli kukabidhiwa ripoti ya kamati ya kwanza ya uchunguzi wa mchanga wa dhahabu (makinikia) Mei 24, mwaka huu. Hata hivyo, jana asubuhi Prof. Muhongo kupitia simu yake ya

GONJWA LA ZARI THE BOSS LADY HOFU YATANDA,SIKU CHACHE MUMEWE KUFARIKI

Image
PRETORIA: Takriban siku 25 baada ya kifo cha aliyekuwa mumewe, Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’, staa wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, ameibua hofu kubwa kwa ndugu, jamaa na marafi ki baada ya kupata gonjwa la ghafla lililosababisha kukimbizwa hospitalini akiwa hoi.Kwa mujibu wa mpenzi wake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, mapema wiki hii, Zari alikimbizwa hospitalini huko Pretoria nchini Afrika Kusini na kulazwa kutokana na hali yake kuwa mbaya. Ilifahamika kwamba, Zari alikutwa na hali hiyo siku moja tu tangu mama yake mzazi, Halima Hassan naye alazwe jijini Kampala, Uganda kwa matatizo ya moyo kushindwa kufanya kazi hivyo kupishana kwa saa kadhaa za kukimbizwa hospitalini. NI SIKU CHACHE TANGU AKABIDHIWE OFISI YA IVAN Ilielezwa kwamba, Zari ambaye ni mfanyabiashara wa Uganda mwenye makazi Afrika Kusini alikutwa na hali hiyo ikiwa ni siku chache tangu alipoanza kufanya kazi kwenye ofi si ya Ivan aliyokabidhiwa hivi karibuni huko Pretoria, Juni

HISTORIA YA MUUZA MADAWA YA KULEVYA NGULI DUNIANI PABO ESCOBAR

Image
Katika milima inayotazamana na mji wa Medellín nchini Colombia, yapo majengo ya kifahari kabisa ndani ya milima hiyo ambayo kwa sasa majengo haya yanatumika kama nyumba ya watawa wa Kanisa Katoliki lakini kabla ya watawa hawa kupewa majengo haya mwaka 2007, majengo haya yalikuwa ni gereza ambalo lilijengwa mwaka 1991 kumuhifadhi mfungwa maalumu raia wa Colombia.Gereza hili lilikuwa ni tofauti kabisa na magereza yote ambayo umewahi kuyasikia kwani gereza hili licha ya kuwa mali ya serikali lakini michoro yake ilichorwa na kubuniwa na mfungwa mwenyewe. Si hivyo tu, bali hata maaskari magereza ambao walikuwa wanalinda gereza hili walichaguliwa na mfungwa mwenyewe na hata polisi wa nchi ya Colombia walikuwa hawaruhusiwi kusogolea gereza hilo hata umbali wa maili 12. Kama hiyo haitoshi gereza hili lilikuwa na uwanja wa mpira wa miguu, lilikuwa na bafu lenye Jaccuzi, lilikuwa na bar, lilikuwa na maporomoko ya maji (water falls) yaliyobuniwa kiustadi, na pia chumba (sel