HII NDIO KAULI YA JUX BAADA YA KUMALIZA MASOMO YAKE
Msanii wa Bongo Fleva, Jux amesema haikuwa kazi rahisi hadi yeye kumaliza masomo yake ya elimu ya juu nchini China.
Muimbaji
huyo amesema kuwa katika miaka mitano aliyosoma kuna wakati alikuwa
anakosa mitihani kwa sababu ya show lakini anaishukuru familia yake kwa
kuwa karibu na yeye.
“It’s
not easy at all lakini nashukuru sana rafiki zangu ambao wamenizunguka,
familia yangu ni watu ambao walikuwa wananipa sana moyo, walinieleza
kila kitu kinawezekana usikate tamaa, naweza nikamaliza nikafanya vitu
vyote, naweza nikafanya biashara, muziki na kusoma pia,” Jux ameiambia
XXL ya Clouds FM.
“Namshukuru
Mungu nimemaliza leo, so kila kitu kinawezekana naweza nikakuambia muda
wako tu unavyoupanga na changamoto zipo nyingi, kushindwa sio tatizo
ila hutakiwa kuacha. Kuna mitihani kama miwili hivi nakumbuka nilikuwa
nipo Bongo nina show wenzangu wakafanya lakini nilikuja nikarudia, so
changamoto kama hizo zinapatikana na inabidi vitu vyote viende kwa
wakati mmoja lakini muda wako ni kitu ambacho kinaweza kukufanya ukawa
sawa, namshukuru Mungu nimemaliza kwa hiyo sasa hivi ni muziki
biashara,” ameongeza.
Comments
Post a Comment