Posts

KULIKONI !? Sumaye Kujiuzulu ujumbe wa bodi CRDB, KISA?!

Image
Waziri Mkuu mstaafu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Mashariki, Frederick Sumaye, amejiuzulu ujumbe wa bodi ya Benki ya CRDB ili atekeleze zaidi majukumu yake ya kisiasa. "Nina shughuli nyingi za kisiasa ambazo zitaninyima nafasi ya kuhudhuria vikao vya bodi.  Sipendi pia kuona CRDB ikihusishwa na msimamo wangu kisiasa. Hii ni taasisi huru ambayo ina wanahisa wengi ambao sitapenda kuona maslahi yao yakiingiliwa kutokana na siasa,"  amesema Sumaye.

Uthibitisho wa Simba kufika FIFA

Image
Ushahidi kuwa klabu ya Simba imewasilisha malalamiko yake kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), umepatikana. Kitendo cha Simba kuwasilisha rufaa hiyo na picha ikionyesha ushahidi huo, inaonekana kuwakwaza zaidi ya mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wameanza sherehe za ubingwa. Baadhi ya mashabiki wa Yanga, wameonekana kukerwa na jambo hilo huku wakiwaita Simba “Wazee wa pointi za mezani”. Lakini mashabiki wa Simba wamekuwa wakijibu mapigo na kusema, “Haki ni haki” na sheria itafuata mkondo wake. Yanga na Simba zimemaliza ligi zikiwa na pointi 68 kila moja, lakini Yanga ina wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa GD. Silaha ya Simba, inabaki kuwa suala la pointi za Kagera na kama kweli Fifa itaamuru irejeshewe, basi itafikisha pointi 71 na kutangazwa kuwa bingwa. Simba ilishinda rufaa yake kupitia kamati ya Saa 72 ambayo ilibaini kuwa kweli beki Mohammed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano wakati Simba ilipolala kwa mabao 2-1 katika mechi ya ligi

WATANZANIA 11 WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMBAKA KWA ZAMU MAMA MJAMZITO AFRIKA KUSINI

Image
Wanaume 11 ambao ni raia wa Tanzania wamekamatwa na Polisi na kufikishwa Mahakamani wiki hii Johannesburg Afrika Kusini .Radioni na Mtandaoni Johannesburg wiki hii kumeripotiwa kuwa kosa lililofanya Wanaume hao 11 kukamatwa na Polisi ni kumbaka Mwanamke mjamzito mwenye umri wa miaka 22 aliyekuwa akitoka kazini saa kumi na moja alfajiri.Mwanamke huyo alikuwa akitoka kazini na Mfanyakazi mwenzake ambaye ni Mwanaume ambapo ghafla walivamiwa na kundi la Wanaume wenye silaha za moto na wakamvuta Mwanamke huyo kabla ya kumpiga Mfanyakazi mwenzake ambae baadae alifanikiwa kutoroka.Baada ya Mfanyakazi huyo kutoroka aliwapigia simu Polisi na wakafanikiwa kuwahi eneo la tukio na kukuta Wanaume hao wakimbaka kwa zamu Mwanamke huyo mwenye ujauzito wa miezi mitatu.Polisi wapatao kumi waliingia kwenye jengo tukio lilikofanyika na kumuokoa Mwanamke huyo aliyekua kwenye hali mbaya ambapo walimpeka Hospitali huku Watuhumiwa wakichukuliwa na kupandishwa Mahakamani siku ya Jumatano.

Dalili za Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo

Image
Hapo kabla tulisoma kwa kirefu kuhusu vidonda vya tumbo, kisha tukasoma kuhusu dawa mbadala ya vidonda vya tumbo, tukasoma tena kuhusu chakula cha mgonjwa wa vidonda vya tumbo, na leo tunaendelea kuangalia dalili za ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni pamoja na; Kuchoka choka sana bila sababu maalum Kuuma mgongo au kiuno Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia Kizunguzungu Kukosa usingizi Usingizi wa mara kwa mara Maumivu makali sehemu ya mwili Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali. Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali Kichefuchefu Kiungulia Tumbo kujaa gesi Tumbo kuwaka moto Maumivu makali sehemu kilipo kidonda Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi Kutapika nyongo Kutapika damu au kuharisha Sehemu za mwili kupata ganzi Kukosa hamu ya k

WACHIMBAJI WA MADINI WAFARIKI KWA KUKOSA HEWA MGODINI TANZANIA

Image
Wachimbaji wawili wadogo wa madini ya dhahabu katika kijiji cha Masuluti kata ya Magulilwa tarafa ya Mlowa wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamefariki dunia baada ya kukosa hewa. Wananchi wa Msuluti kata ya Magulilwa wilaya ya Iringa wakiwa wamebeba mmoja kati ya miili ya wachimbaji wadogo wawili waliokufa mgodini kwa kukosa hewa leo Miili ya wachimbaji wadogo wawili katika mgodi ya Mamweli Msigwa ukiingizwa kwenye gari la polisi Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi katikati mwenye kofia nyeusi akionyeshwa shimo la mdogi wa dhahabu ambalo limesababisha vifo vya watu wawili Wananchi wakiwa eneo la tukio Askari polisi na wananchi wakitazama mgodi huo uliouwa Milili ya wachimbaji wadogo wawili walipoteza maisha mgodini leo Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julius Mjengi kushoto akitazama shimo la mgodi katika kijiji cha Msuluti kata ya Magulilwa wilaya ya Iringa ambalo wachimbaji wawili wadogo wawili walipoteza maisha kwa kukos

BIZARI: KIUNGO CHA MBOGA CHENYE FAIDA NYINGI

Image
Inawezekana katika maisha yako hujawahi kula mboga iliyowekwa kiungo kinachoitwa bizari, kama umewahi, inawezekana pia hujawahi kujua faida zake mwilini. Bizari (Turmeric) ni kiungo cha mboga jamii ya mimea unaochimbwa kama mizizi, mfano wa tangawizi, lakini tangawizi yenyewe ina rangi ya njano na hujulikana pia kama ‘manjano’ kutokana na rangi yake. Kiungo hiki kinatumiwa sana katika Bara la Asia na hasa India na China. Kutokana na umuhimu wake kiafya, vyakula vingi hupikwa kwa kuchanganya na kiungo hiki ambacho sasa kimeenea dunia nzima, ikiwemo Tanzania. FAIDA ZA BIZARI KIAFYA Bizari hutumika na watu wengi kama kiungo cha mboga cha kuongeza ladha katika mchuzi na pengine kuweka rangi, lakini kuna faida nyingi unazozipata unapotumia kiungo hiki kila mara katika mapishi yako. Inaelezwa kuwa bizari ina virutubisho vyenye uwezo wa kuimarisha kinga ya mwili, mara 8 zaidi ya Vitamin C na Vitamin E, ina uwezo wa kushusha kiwango cha lehemu (cholesterol) na kuzuia

WACHEZAJI WA RUVU SHOOTING WAPATA AJALI SINGIDA

Image
Habari tulizozipata hivi punde ni kwamba msafara wa timu ya Ruvu Shooting umepata ajali mbele kidogo ya Singida wakiwa safarini kurejea nyumbani.Taarifa kutoka kwa mmoja wachezaji waliokuwapo inasema kwamba gari likiwa katika mwendo tairi lilipasuka na kusababisha gari kuhama njia na kuparamia miti iliyokuwa jirani.Hakuna mtu yoyote aliyeumia sana japo kuna mchezaji mmoja ambaye amepata majeraha ya kawaida. Taarifa zaidi tutawaletea hivi punde....

Rais Magufuli akabidhi rasmi uenyekiti EAC kwa Rais Museveni

Image
Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo (Jumamosi) amemkabidhi rasmi uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa Rais Yoweri Museveni. Muda mfupi kabla ya kumkabidhi nafasi hiyo, Rais Magufuli ambaye alikuwa mwenyekiti wa EAC kwa miaka miwili amewashukuru wanachama wa jumuiya hiyo kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo miezi michache baada ya kuingia madarakani. “Mliniamini mkanichagua licha ya kuwa madarakani kwa muda mfupi,”amesema Rais Magufuli ambaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa EAC, mapema mwaka jana. Rais Magufuli amesema anaimani na Rais Museveni kuwa atafanya kazi nzuri kutokana na uzoefu wake. “Yaliyonishinda kuyatatua, atayatatua yeye (Rais Museveni),”amesema. Mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo, Rais Museveni ambaye sasa ni mwenyekiti wa EAC amesema atahakikisha anatumikia nafasi hiyo kwa nguvu na uwezo wake wote.

MREMBO ALIPIA BANGO KATIKATI YA JIJI AKITANGAZA KUWA BIKIRA,ADAI ANASAKA TENDO KABLA HAJAFA

Image
Katika hali isiyo ya kawaida, muigizaji wa vipindi vya TV mwenye umri wa miaka 40 amelipia ‘Bango’ kubwa katikati ya jiji akijitangaza kuwa ni bikira anayetafuta mwanaume wa kufanya naye tendo la ndoa ili asife bila kujua uhondo wake.Kwa mujibu wa Daily Mirror, Aranya ‘Pui’ Pathumthong ambaye ni muigizaji wa Thailand, aliyeweka bango hilo katika jiji la Bankok, karibu na wilaya ya Lat Phrao amesisitiza kuwa yuko ‘serious’ na tangazo hilo ambalo ameliweka baada ya matangazo yake kupitia mitandao ya kijamii ya mahusiano nchini humo kushindwa kuzaa matunda. Tangazo lake limeandikwa, “I Want You. “40 and a virgin. Pui Aranya is looking for a husband!”Let me get it once before I die.” Linaonesha namba ya simu pia.Aranya ameviambia vyombo vya habari nchini humo kuwa ameamua kusaka mwanaume kwa mtindo huo ili aweze kuonja raha ya penzi kabla hayafa.Hata hivyo, Polisi jijini humo wameamuru Bango hilo liondolewe ingawa limelipiwa na kuongeza kuwa wanahitaji kumhoji mwanamk

Marekani: Mtoto Doreen Amemaliza Kufanyiwa Upasuaji wa Uti wa Mgongo

Image
  Taarifa ya Mbunge Lazaro Nyalandu Latest UPDATE: Mei 18, Alhamisi Saa 4:30 Usiku (Masaa ya Afrika Mashariki) Habari za HIVI PUNDE kutoka Hospitali ya Mercy, Sioux City IA MTOTO Doreen amemaliza KUFANYIWA UPASUAJI wa UTI wa MGONGO, kwa KILE ambacho MADKTARI wamesema kumefanikiwa kwa UFANISI Mkubwa, KUPITA matarajio yao. MTOTO Doreen alikuwa afanyiwe UPASUAJI kwa makadrio ya MASAA 5:30, LAKINI zoezi HILO lilikamilika kwa muda wa MASAA 4:00, Huku TEAM ya “Surgical Support” IKIWA na watu 6, na kwa PAMOJA wakiongozwa na MADAKTARI BINGWA 2, Dr. Meyer na Dr. Durward. MTOTO Doreen amehamishwa KUTOKA chumba cha UPASUAJI na kupekewa ICU, na MADAKTARI wamesema KWAKUWA hali yake imeridhisha SANA, BAADAYE Leo watamtoa ICU ambako wamempumzisha baada ya UPASUAJI, na kumrudisha WODI ya WATOTO ambako ataendelea na MAPUMZIKO. MUNGU amesikia MAOMBI ya WATANZANIA na WOTE waliotoa SALA na DUA zao kwa ajili ya MTOTO Doreen POPOTE Duniani

STAA WA FILAMU YA KUCH KUCH HOTA HAI REEMA LAGOO AMEFARIKI DUNIA

Image
Reema Lagoo, muigizaji mkongwe kutokea nchini India aliyekuwa akiishi katika mji wa Mumbai amefariki dunia kwa kuugua kifua.Lagoo amefariki akiwa katika hospitali ya Dhirubhai Ambani, masaa machache baada ya kufikishwa hospitalini hapo. Marehemu amepata umaarufu kupitia filamu ya “Kuch Kuch Hota Hai”, Kabla ya umauti wake amekuwa akigiza mara nyingi kama mama kwenye filamu kama vile “Hum Aapke Hain Koun” na “Kal Ho Na Ho”.Lagoo mwenye miaka 59 kabla mauti kumfika, alifikishwa hospitalini hapo lakini alikuwa akilalamika juu ya maumivu makali ya kifua, Alisema msemaji wa Hospitali hiyo Bw. Ram Naraian.Kabla ya mauti kumfika, marehemu amewahi kuigiza filamu kama vile “Maine Pyar Kiya”, “Saajan”, “Vaastav, na “Hum Saath-Saath Hain”., pia alikuwa akionekana kwenye tamthilia iitwayo “Naamkaran”, inayooneshwa Star Plus

Vyakula 9 Hatari kwa Kupunguza Nguvu za Kiume

Image
  1.Soya (Soy):  Ina kiwango kikubwa cha Isoflavones ambayo ni kiuhalisia ni estrogen. Ulaji wa soya ni sawa na kula kidonge kimoja cha uzazi wa mpango (birth control pill). Kwa kuelewa zaidi madhara ya soya kwa wanaume soma hapa.   2. Licorice:  Huu ni mzizi ambao hutumika hasa kuondoa tatizo la msongo (stress) kwa watu wanaokumbwa na tatizo hilo. Pia mzizi huo hutumika kama sukari kwenye vinywaji kama chai au kahawa badala ya kutumia sukari ya kawaida. Hata hivyo mzizi huu una estrogen ambayo hushusha kiwango cha homoni ya kiume ya testosterone kwa wanaume. Kuna utafiti ulifanywa ambapo wanaume 7 wenye afya walipewa gramu 7 za vidonge vya licorice kila mmoja kila siku. Vidonge hivyo vilikuwa na kiasi cha gramu 0.5 za glycyrrhizic (kiambata kilichomo ndani ya licorice kinachopunguza testosterone kwa mwanaume). Baada ya siku 4 tu kiasi cha homoni ya testosterone kwa kila mwanaume aliyefanyiwa utafiti huo kilipungua kwa kiwango cha nusu ya kiasi cha homoni

SERENGETI BOYS MGUU NDANI KOMBE LA DUNIA,YAIBUTUA ANGOLA AFCON U-17 NCHINI GABON

Image
Timu ya vijana chini ya miaka 17 ya Tanzania ‘Serengeti Boys’ imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza kwenye michuano ya AFCON U17 baada ya kuifunga Angola kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa Kundi B uliochezwa Uwanja wa L’Amittee mjini Libreville,nchini Gabon. Vijana wa Serengeti Boys ndio walikua wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya sita kipindi cha kwanza baada ya Kelvin Naftal kupasia kamba kwa kichwa akiunganisha krosi ya Nickson Kibabage. Dakika ya 18 Angola walisawazisha bao hilo kupitia kwa Pedro baada ya kutumia vizuri makosa ya safu ya ulinzi ya Serengeti Boys na kufanya timu zote kwenda mapumziko zikiwa sare kwa kufungana 1-1.Kipindi cha pili Serengeti waliongeza kasi kutafuta bao na kufanikiwa kufunga dakika ya 69 mfungaji akiwa ni Abdul Suleiman baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Yohana Mkomola. Serengeti Boys imefikisha pointi 4 baada ya kupata pointi moja kwenye mchezo wa kwanza kufuatia kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Mali ambao ndio ma

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MAY 19,2017

Image