Posts

Wamarekani Wafanikisha Upasuaji Mkubwa wa Wanafunzi Lucky Vincent

Image
May 18, 2017 Mtoto Wilson      Watoto watatu wa shule ya msingi ya Lucky Vicent walionusurika katika ajali ya basi, wamefanyiwa upasuaji na sasa wapo wodini wakiendelea na mazoeazi, ila Doreen, jana alipewa MAPUMZIKO maalumu akiwa anaandaliwa tayari kwa UPASUAJI wa uti wa mgongo ‘spine’  unaofanyika leo.   Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliyeshiriki katika kuwasafirisha watoto hao, ameandika katika ukurasa wake wa facebook akisema  watoto hao kwa sasa wamewekwa kwenye vyumba vya peke yao.   Mtoto Doreen Upasuaji huo umefanyika katika Hospitali ya Mercy, Sioux City, Marekani.   Amefafanua upasuaji waliofanyiwa na kusema mtoto Saidia alifanyiwa upasuaji wa mfupa wa kulia wa nyonga, mkono wa kulia na kuwekewa ngao kwenye shingo atakayotakiwa kukaa nayo kwa wiki sita.   “Kwa upande wa mtoto Wilson, yeye amefanyiwa upasuaji wa nyonga ya kulia, kiwiko cha kulia kilichokuwa kimevunjika mara tatu na kiwiko cha kushoto,” amesema

IMEFICHUKA! Mume wa Zari anasumbuliwa na ugonjwa huu

Image
KAMPALA: Habari mbaya zilizolifikia mtandao huu zinadai kuwa, aliyekuwa mume wa staa wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tycoon Ivan Ssemwanga yu hoi bin taaban akisumbuliwa na maradhi ya shambulio la moyo (Coronary Artery Disease). Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya jijini Kampala, Uganda ambako ndiko maskani yake yalipo maeneo ya Munyonyo, pamoja na kwamba ana makazi Pretoria, Afrika Kusini, Ivan alionekana hadharani kwa mara ya mwisho akiwa amedhoofu na rangi ya ngozi kupauka, tofauti na alivyozoeleka kuwa na rangi nyeusi yenye mng’aro alipotinga kwenye Pati ya Blankets and Wine iliyofanyika Kampala hivi karibuni. Chanzo kilichomshuhudia Ivan kilitonya: “Sisi wenyewe tulipomuona kwenye Blankets and Wine Party akiwa na rafiki yake, Ed Cheune, kwanza hatukumtambua, lakini tulipomuangalia vizuri ndipo tukamjua ni yeye. Ukweli tulishtuka sana na tulijua anaumwa. “Tofauti na alivyozoeleka kuwa ni mtu wa bata, lakini siku hiyo alikuwa mpole sana. Al

Vladimir Putin nipo tayari kutoa siri za mkutano wa Trump na maafisa wa Urusi

Image
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameingilia sakata inayomkabili Rais wa Marekani Donald Trump kutokana na uhusiano wake na Urusi. Rais Putin amepinga madai ya uvujaji siri za Marekani kwa Urusi na kueleza kuwa yuko tayari kutoa kumbukumbu za mkutano wa viongozi hao kwa bunge na Seneti za Marekani ikihitajika. Putin ametania hali hiyo na kusema kuwa mkutano haukufanyika unavyodhaniwa. Majarida mbalimbali ya Marekani yamefichua kuwa Rais Trump aliwapa viongozi wa Urusi taarifa kuhusu Islamic State ambazo zina uwezo wa kuhatarisha watoaji wa taarifa hizo. Haya yanajiri huku taarifa zikienea kuwa Bw Trump alijaribu kushawishi uchunguzi unaoendelea kuhusu ushirikiano wa wawakilishi wake na Urusi. Bwana Trump alikutana na waziri wa kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov na Balozi wa Urusi nchini Marekani Sergei Kislyak katika ikulu ya White house Jumatano, wiki iliyopita. Mkutano huo unajiri wakati uchunguzi

MARADHI YA GESI TUMBONI (COLIC): Msokoto wa tumbo

Image
MARADHI YA GESI TUMBONI (COLIC): Msokoto wa tumbo Ikiwa mtu atakula kwa wingi vyakula vinavyoleta gesi halafu vyakula hivyo visisagike vizuri tumboni, hukusanya gesi tumboni na kufanya mingurumo humo na kumsababishia maumivu, humkosesha mtu utulivu na kumfanya kutoka jasho na machovu bila ya kufanya kazi. Mtu hujisikia mara kwa mara aende haja kubwa na akienda hapati choo. Pia humsababishia mtu kuumwa kwa mgongo au kiuno. Ikiwa gesi hii itakosa kutoka kwa njia ya haja kubwa, basi yaweza kupanda juu na kufanya presha sehemu au karibu ya moyo na kusababisha maumivu ya moyo. TIBA:  Chukua asali robo lita , unga wa arki susi vijiko vitatu vikubwa na unga wa habat soda vijiko viwili vikubwa. Koroga zote pamoja kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni.

Mastaa wa Bongo waonyesha hisia zao walivyoguswa na msiba wa Dogo Mfaume

Image
 Leo May 17, 2017 tasnia ya muziki Tanzania imejawa na huzuni baada ya kutangazwa taarifa za kifo cha Mwimbaji Dogo Mfaume aliyefariki akiwa Muhimbili Hospital ambako alitarajia kufanyiwa upasuaji wa kichwa. Kutokana na kusambaa kwa taarifa hizo za majonzi ambazo zimegusa hisia za watu mbalimbali wakiwemo mastaa wa muziki, watu hao wameelezea masikitiko yao kupitia social media wakiongozwa na mastaa Diamond Platnumz, Nay wa Mitego na wengine…

PRINCE WILLIAM AMTEMBELEA MTOTO MWENYE KANSA

Image
Prince William kutokea familia Malkia Elizabet II, Siku ya jana alifanya ziara ya kutembelea hospitali ya Royal Marsden iliyopo Sutton- Uingereza. Katika ziara hiyo Prince William aliweza kumtembelea mtoto Daisy Wood mwenye miaka 6, anaeugua ugonjwa wa kansa, kisha kuzungumza nae pamoja na wazazi wake. Hii ni mara ya 10 kwa mwana wa mfalme Prince William kutembelea hospital hiyo tangu kuchaguliwa kuwa anasimamia Royal Marsden NHS Foundation Trust.

Wanawake 11 wateuliwa kuwa mawaziri Ufaransa kati ya mawaziri wote 22

Image
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameteua baraza la mawaziri lenye usawa wa kijinsia kuambatana na ahadi ya mapema ambapo 11 kati ya mawaziri 22 ni wanawake. Sylvie Goulard ndiye waziri mpya wa ulinzi huku bingwa wa olimpiki wa mchezo wa kupigana na panga Laura Flesseng, akiteuliwa kuwa waziri wa michezo. Bruno Le Maire ameteuliwa kuwa waziri wa uchumi, Gérard Collomb waziri wa masuala ya ndani, huku naye François Bayrou ndiye waziri wa sheria. Rais huyo mpya wa Ufaransa ana matumaini kuwa kikosi hicho kitazoa kura nyingi kwenye uchaguzi wa ubunge mwezi ujao. Alitimiza ahadi yake ya kuwepo usawa kwenye baraza la mawaziri, lakini kati ya nafasi muhimu tano , ni moja ya tu ya ulinzi ilimuendea mwanamke. Mawaziri wengine ni pamoja na Jean-Yves Le Driana, ambaye ameteuiliwa kuwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni. Wengine ni pamoja na: Agnès Buzyn - Afya Murielle Pénicaud - Kazi Mounir Mahjoubi - Masuala ya dijitali Françoise Nyssen - Utamaduni Jean-Michel

DAWA ZA KULEVYA ZAMUUMIZA MSANII MADEE ALI

Image
Rais wa Manzese, Madee Ali amefunguka kwa uchungu kuwataka vijana wanaojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya kuacha mara moja na kutafuta njia za kupunguza mawazo ili kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na janga hilo. Madee amefunguka hayo akiwa kwenye Planet Bongo ya East Africa radio na kusema kuwa janga la dawa za kulevya limezidi kukithiri hali ambayo kwa vijana wa sasa kutimiza miaka 40 limekuwa  jambo la nadra sana. Aidha Madee amelazimika kuwaasa vijana kutokana kifo cha Msanii mwenzake Dogo Mfaume kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na za dawa ya kulevya. "Madawa yanatumaliza sana jamani. Nawaomba wadogo zangu, ndugu zangu tubadilishe njia za kupunguza mawazo.  Najua stress ni nyingi na ndio zinatukimbiza huko, tuachane na madawa maana hayana msaada zaidi  kutumaliza kwa wingi. Ukiangalia matokeo ya dawa za kulevya kwa umri huu ukifikisha miaka zaidi ya 40 inakubidi umshukuru Mungu sana'' - Madee alliongeza.

Takukuru wanasa mali za mhasibu wao, Ana magorofa 7, Nyumba 9, Viwanja 37, Magari 5

Image
Miongoni mwa mali zinazomweka mhasibu huyo katika kundi la matajiri katika nchi hii inayotambuliwa kimataifa kama mojawapo ya mataifa maskini, ni pamoja na viwanja 37, maghorofa saba, nyumba za kawaida tisa, magari matano na pikipiki. Maghorofa, nyumba za kawaida na viwanja vya mhasibu huyo ambaye alishafukuzwa kazi tangu mwaka jana viko kwa mtawanyiko katika maeneo mbalimbali nchini yakiwamo ya ghali karibu na bahari, Kigamboni na Mbweni jijini Dar es Salaam na pia Bagamoyo mkoani Pwani. Kwingineko kuliko na mali hizo ni Kinondoni (Dar), Musoma, Nyegezi na Kiseke jijini Mwanza. Hata hivyo, chanzo cha uhakika kimeiambia Nipashe kuwa hivi sasa mali hizo ziko chini ya himaya ya Takukuru, baada ya kuzinasa kufuatia idhini ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyotokana na ombi la taasisi hiyo. Mei 9, mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilitoa amri ya zuio la mali za Gugai ambaye anakabiliwa na tuhuma za kujilimbikizia mali kinyume cha Sheria ya Kuzuia n

Q-Chillah, Ray C, TID, Matonya, Marlaw na Besta Turudisheni Muziki Wetu

Image
Stori: BRIGHTON MASALU | RISASI JUMATANO | RISASI VIBES “ NINACHO-KIPATA, nagawana na wenzangu maskini zaidi yangu, wenye dhiki kama mimi, waliopoteza wazazi wao kwa ugonjwa wa Ukimwi… wale wenzangu na mimi wasiojiweza kitandani, yaani wa leo wa kesho, dua nawaombea… moyo wangu wa mbigili… kila mtu wamchoma….” “Hebu tathmini kisha nipe jibu…,hivi kwa nini hutaki kunijibu, mitihani yote nimeshinda…nadhani ni wakati penzi letu sisi liwe wazi, roho yangu inauma…maumivu sasa basi…Sasa basi, niko thabiti, nielewe pesa siyo mapenzi, kwa utenzi huu nielewe baby, nakuhitaji mpenzi, wewe ndiyo faraja yangu…” TID “Umenikataa bila sababu, umeninyanyasa bila aibu… nimepata mwingine tabibu sasa wanifuatafuata nini? Kama ni pendo langu nilikupa lote, nilikujali kwa kila kitu na kukupa mahaba yote, sikudhani ungenidharau na kuniletea wengine…sikudhani ungenigeuka na kuanza kuninyanyasa, pesa na magari yako yalikufanya uwe kiburi, uliniacha ukaenda zako na kusahau utu

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 17.05.2017

Image
 

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI LEO TAREHE 17/05/2017

Image

Malima aachiwa kwa dhamana ya mil 5

Image
Tuesday, May 16, 2017 Aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Fedha, Mhe Adam Malima ameachiwa leo kwa dhamana ya shilingi milion 5 katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la shambulio. Malima ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Mkuranga amedaiwa kumzuia Ofisa huyo kufanya kazi yake ya kumkamata Ramadhani Kigwande kwa kosa la kumshambulia Mwita Joseph. Wakati akisoma mashtaka yaliyokuwa yakimkabili Mhe Malima, Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono alidai kuwa Mei 15,2017 katika eneo la Masaki kwa makusudi Malima alimzuia Ofisa wa polisi H.7818 PC ABDU kufanya kazi yake halali. Wakili Kombakono aliendelea kudai kuwa mshtakiwa huyo akiwa na nia ya kumzuia Mwita Joseph ambaye ni Ofisa oparesheni wa kampuni ya Priscane Business Enterprises  wakati alipokuwa akimkamata kwa kupaki vibaya gari namba T 587 DDL alimshambulia(Mwita) na kumsababishia maumivu. Kwa upande wa mshtakiwa wa kwanza, Ramadhani Mohammed Kigwande (Dereva wa Malima) naye anakabili

Mwanaye Madega Aua, Naye Auawa Ajalini

Image
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa TFF, Iman Omary Madega. MWANDISHI WETU | CHAMPIONI |HABARI MWENYEKITI wa zamani wa Yanga, Imani Madega amepata msiba mkubwa baada ya mwanaye, Omary Madega kupata ajali iliyosababisha kifo na baadaye kuuawa kwenye ajali nyingine. Omary anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 32, aliuawa wakati akiwakimbia madereva wa bodaboda katika eneo la Chalinze mkoani Pwani akiwa anatumia gari la baba yake mdogo, Madega ambaye kitaalamu ni mwanasheria. Akizungumza na Championi Jumatano , Madega aliyeonyesha masikitiko makubwa alisema gari lililosababisha ajali ni Mitsubishi Pajero, mali yake. “Nina msiba mkubwa sana ndugu yangu. Nilisafiri kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze ambako nilipitiliza kwenye project yangu. Nikiwa huko gari lilisumbua.  “Nikamuita Omary ambaye ni mtoto wa kaka yangu aje alishughulikie. Alipofika pale alikuwa na fundi, akamchukua na mtu ambaye amekuwa akisimamia nyumba yangu ninapokuwa Dar es Salaam pamoja na msimamizi wa

Faida Za Pilipili Kichaa Kiafya Na Kitiba

Image
Tuesday, May 16, 2017 Afya Pilipili kichaa inaweza kustawi sehemu mbalimbali na inahitaji siku 100 za ukuwaji. Hustawi zaidi kwenye mazingira ya joto na unyevunyevu.Mmea huu hukua kufikia urefu wa futi mbili hadi nne. Ina wingi wa vitamini A pia ina vitamini B, vitamini E, vitamini C, Riboflavin, Potassium, Manganese. - Jamii nyingi hususa Marekani na bara la Asia wana historia ya kutumia pilipili kichaa kama tiba. Ni dawa yenye nguvu sana na matumizi mengi, hutumika sana kwa kusafisha damu na  kutoa sumu mwilini, pia hutumika kusisimua mzunguko wa damu na kuweka sawa uwiano wa tindikali(acid)mwilini. Pilipili kichaa imetumika kwa maradhi tofauti tofauti ikiwemo moyo, gauts, kupooza homa, kikohozi, tonsilatis, kichefuchefu  hemorhoids  kwa miaka mingi huko Asia na mashariki ya mbali. MAAJABU YA PILIPILI KICHAA; 1.Kutibu kidonda-Hii inaweza kuwa ni ajabu kwa walio wengi lakini ni tiba liyothibitishwa na imekuwa

Kauli ya Kamanda Sirro Kuhusu Askari Aliyefyatua Risasi Angani

Image
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro, leo amezungumza na waandishi wa habari akieleza juu ya mzozo uliotokea baina ya aliyewahi kuwa waziri katika serikali ya awamu ya nne, Adam Malima na Polisi katika eneo la Masaki lililopelekea askari huyo kufyatua risasi kadhaa hewani. Kamishna Sirro alieleza kuwa Mheshimiwa Adam Malima alikuwa ameegesha gari lake eneo ambalo haliruhusiwi kwa ajili ya maegesho ndipo alipokuja mfanyakazi wa kampuni ambayo ni wakala wa ukusanyaji wa madeni, kukamata teksi bubu pamoja na magari yaliyoegeshwa vibaya akiamuru gari la Malima lipelekwe “yard” ya kampuni hiyo. Lakini dereva wa Malima likataa na akaamua kuondoa gari katika eneo lilipokuwa limeegeshwa, ndipo askari wa Polisi alipoingilia tukio lile. “Yule dereva bado alikataa kupeleka gari yard, matokeo yake akaliondoa lile gari na askari wetu alipoona analiondoa lile gari akalirukia na kuingia kwa nguvu kisha akamlazimisha dereva kulirudisha gari lilip