Takukuru wanasa mali za mhasibu wao, Ana magorofa 7, Nyumba 9, Viwanja 37, Magari 5

Miongoni mwa mali zinazomweka mhasibu huyo katika kundi la matajiri katika nchi hii inayotambuliwa kimataifa kama mojawapo ya mataifa maskini, ni pamoja na viwanja 37, maghorofa saba, nyumba za kawaida tisa, magari matano na pikipiki.
Maghorofa, nyumba za kawaida na viwanja vya mhasibu huyo ambaye alishafukuzwa kazi tangu mwaka jana viko kwa mtawanyiko katika maeneo mbalimbali nchini yakiwamo ya ghali karibu na bahari, Kigamboni na Mbweni jijini Dar es Salaam na pia Bagamoyo mkoani Pwani. Kwingineko kuliko na mali hizo ni Kinondoni (Dar), Musoma, Nyegezi na Kiseke jijini Mwanza.
Hata hivyo, chanzo cha uhakika kimeiambia Nipashe kuwa hivi sasa mali hizo ziko chini ya himaya ya Takukuru, baada ya kuzinasa kufuatia idhini ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyotokana na ombi la taasisi hiyo.
Mei 9, mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilitoa amri ya zuio la mali za Gugai ambaye anakabiliwa na tuhuma za kujilimbikizia mali kinyume cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  Namba 11 ya mwaka 2007.
 Amri ya zuio la mali za Gugai ilitolewa na Mahakama hiyo kutokana na ombi la Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) chini ya kifungu namba 38(1)(a) na (b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 katika shauri namba 13 la 2017.
Mali hizo ni nyumba saba za ghorofa moja moja zilizopo maeneo ya Wilaya ya Kikondoni jijini Dar es Salaam, nyumba nane, viwanja 37, magari matano na pikipiki moja.
Katika orodha ya mali hizo zinazoshikiliwa na Takukuru, na ambayo Nipashe imeona nakala yake, inaonyesha kuwa mali za mhasibu huyo wa zamani zilizowekewa zuio la Mahakama ni nyumba nne za ghorofa moja moja zilizoko kiwanja na 64 kitalu Ununio, Kinondoni, Nyumba tatu za ghorofa moja zilizoko kiwanja na 150 kitalu 8 Bunju na Kinondoni, nyumba nne zilizoko Kiwanja na 225 Kitalu 6, Mbweni JKT,  Kinondoni.
Nyingine ni nyumba zilizoko kwenye kiwanja namba 62 na 63 kitalu C, Kinondoni, nyumba iliyoko kiwanja namba 29 kitalu L, Majita,  Musoma, nyumba namba 713 PPF Kiseke, Mwanza na nyumba iliyoko kwenye kiwaja namba 438 bloku D, Nyegezi, Mwanza.
VIWANJA 37
Katika orodha ya viwanja ni pamoja na kiwanja namba 14 kitalu J, Bunju, Kinondoni, Kiwanja namba 47 kitalu B, Mwongozo, Kigamboni, kiwanja namba 184 kitalu B, Buyuni,Temeke, kiwanja namba 103 Kitalu L, Kaole, Bagamoyo, kiwanja namba 104 Kitalu L, Kaole, Bagamoyo na kiwanja namba 209 kitalu B, Kibaha.
Vingine ni kiwanja namba 195 kitalu 3, Kihonda, Morogoro, kiwanja namba 993 kitalu L, Kiegeya,  Morogoro, kiwanja namba 868 Kitalu Q, Lukobe, Morogoro, kiwanja namba 34 kitalu K, Kisasa B, Dodoma, kiwanja namba 32 kitalu N, Itega, Dodoma, kiwanja namba 39 Kitalu M, Itega, Dodoma, kiwanja namba 24 kitalu B, Chidachi, Dodoma, kiwanja namba 64 Nzuguni, Dodoma, kiwanja namba 230 Kitalu B, Nyegezi, Mwanza na kiwanja namba 439 Kitalu D, Nyegezi, Mwanza.
Viwanja vingine ni kiwanja namba 275 Kitalu 2, Nyamhongolo, Mwanza, kiwanja namba  277 kitalu 2 Nyamhongolo, Mwanza, kiwanja namba  296 kitalu 2, Nyamhongolo, Mwanza, kiwanja namba  297 kitalu 2, Nyamhongolo, Mwanza, kiwanja namba 286 kitalu G, Nyamagana, Mwanza, kiwanja namba 287 kitalu G, Nyamagana, Mwanza, kiwanja namba 90 kitalu 5, Bugarika, Mwanza, kiwanja namba 126 kitalu A, Makoko, Musoma, kiwanja namba 622 kitalu A, Gomba , Arusha, kiwanja namba 621 na 623, kitalu A, Gomba na Arusha, kiwanja namba 737 kitalu C, Mwambani, Tanga
Kiwanja namba 1,2 na 3 kitalu J, Mwambani,Tanga, kiwanja namba 4 kitalu J Mwambani, Tanga, kiwanja namba  5 kitalu J, Mwambani Tanga, kiwanja namba 18 kitalu J, Mwambani Tanga, kiwanja namba 7,9 kitalu J, Mwakidila, Tanga na kiwanja namba 11, 13 kitalu J, Mwakidila, Tanga
ORODHA YA MAGARI
Orodha ya magari ya mhasibu huyo wa zamani Takukuru inahusisha magari matano ambayo ni gari namba T 180 DBQ , Mitsubish Canter; gari namba T 581 BQU, Toyota Hillux; gari namba T 814  CSC Nissan Murrano; gari namba T 679 ASD Toyota RAV 4 na gari namba  T 913 DHE Suzuki. Pia inashikiliwa pikipiki yenye namba zz usajili MC 837BCL
Kutokana na maombi ya DPP mahakama imeamuru mali zilizotajwa za Gugai ziwe chini ya zuio la Mahakama.
Pia mawakala wake na watu wengine wote wanaomwakilisha wamezuiwa kuuza au kuhamisha umiliki au kuweka dhamana mali zote zilizowekewa zuio.
Aidha, Msajili wa hati ameagizwa kusajili zuio hilo kama kizuizi dhidi ya mali zote zilizotajwa.
Pia Msajili Msaidizi wa magari ameagizwa asiruhusu uhamishaji wa umiliki wa vyombo vya moto vilivyowekewa zuio mpaka mahakama itakapoelekeza vinginevyo.

Comments

Popular posts from this blog