Wamarekani Wafanikisha Upasuaji Mkubwa wa Wanafunzi Lucky Vincent
Watoto watatu wa shule ya
msingi ya Lucky Vicent walionusurika katika ajali ya basi, wamefanyiwa
upasuaji na sasa wapo wodini wakiendelea na mazoeazi, ila Doreen, jana
alipewa MAPUMZIKO maalumu akiwa anaandaliwa tayari kwa UPASUAJI wa uti
wa mgongo ‘spine’ unaofanyika leo.
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro
Nyalandu aliyeshiriki katika kuwasafirisha watoto hao, ameandika katika
ukurasa wake wa facebook akisema watoto hao kwa sasa wamewekwa kwenye
vyumba vya peke yao.
Upasuaji huo umefanyika katika Hospitali ya Mercy, Sioux City, Marekani.
Amefafanua upasuaji waliofanyiwa na
kusema mtoto Saidia alifanyiwa upasuaji wa mfupa wa kulia wa nyonga,
mkono wa kulia na kuwekewa ngao kwenye shingo atakayotakiwa kukaa nayo
kwa wiki sita.
“Kwa upande wa mtoto Wilson, yeye
amefanyiwa upasuaji wa nyonga ya kulia, kiwiko cha kulia kilichokuwa
kimevunjika mara tatu na kiwiko cha kushoto,” amesema
Amesema Doreen yeye amefanyiwa
upasuaji wa nyonga, taya katika upasuaji uliochukua saa nne. Leo Doreen
atafanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo.
Comments
Post a Comment