SPIKA WA BUNGE, JOB NDUGAI. SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, ametishia kuwafukuza kazi watumishi wanne wa Bunge wanaofanya kazi kwenye ofisi za Kambi Rasmi ya Upinzani ikiwa wataendelea kuandika hotuba alizoziita zenye maneno machafu dhidi ya uongozi wa Bunge. Aliyasema hayo bungeni jana wabunge walipoazimia kuwasamehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (Chadema) waliokutwa na hatia ya kukidharau chombo hicho cha kutunga sheria. Ndugai mbali na kuipongeza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kazi nzuri ya kuwahoji viongozi hao waliolalakiwa, alisema amebaini kuna ‘mchezo mchafu’ dhidi ya uongozi wa Bunge unaofanywa na wanaoandika hotuba za upinzani. Alisema hotuba kadhaa za upinzani zimekuwa na maneno yanayoashiria kudharau Bunge, hasa Kiti cha Spika. “Nimefanya utafiti wangu. Kw