Lowassa kumuunga mkono Uhuru Kenyatta.
SIASA za Ukanda wa Afrika Mashariki zimechukua sura mpya baada ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa kutangaza rasmi kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta. Kenyatta aliyeunga ushirika pamoja na William Rutto, anaingia katika kinyang’anyiro cha kuwania awamu ya pili ya kuiongoza Kenya huku upande wa upinzani ukiwa umepitisha jina la Raila Odinga kupeperusha bendera ya upinzani. Wakati Lowassa akitangaza kumuunga mkono Kenyatta, kwa upande wake Odinga tayari ilishajulikana wazi urafiki wake na Rais Dk. John Magufuli ambao umeanza miaka mingi tangu akiwa Waziri wa Ujenzi. Hatua hiyo ya Lowassa ambaye anatajwa kuwa mwanasiasa mwenye ushawishi nchini na Afrika Mashariki imekuja baada ya kutembelewa jana nyumbani kwake Monduli na wabunge zaidi ya 20 na maofisa kutoka Kaunti ya Kajiado nchini Kenya. "Mimi naamini Uhuru Kenyatta anao uwezo mkubwa wa kuwaunganisha vema wananchi wa Kenya n