Steve Nyerere aporomosha jambo lingine leo

Muigizaji na mchekeshaji maarufu nchini Steve  Nyerere amemuombea msamaha msanii wa muziki Nay wa Mitego kwa kuwaita wasanii wa filamu wote walioandamana kupinga uingizwaji wa filamu kutoka nje ya nchi kuwa ni 'Matahira'
Akizungumza leo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Steve Nyerere amesema kwamba yawezekana  Nay wa Mitego alikuwa na hasira hivyo akashindwa kutumia lugha sahihi ya kuwaelekeza wasanii wenzake walivyokuwa wanakosea ndio maana alitoa lugha yenye maneno makali ijapokuwa alikuwa sahihi kukosoa maandamano yale.
"Kwanza naomba nimuombee msamaha ndugu yangu Nay wa Mitego, hakuwa na nia mbaya lakini hakutumia maadili kufikisha ujumbe wake, Unajua sisi watanzania hatupendi kuambiwa ukweli na hata tukisemana tuna lugha zetu laini za kusemeshana. Nay wa Mitego mpaka kutoa maneno makali vile ujue anaipenda tasnia yetu ya filamu alikuwa kaaumia, si unajua hata yeye alishawahi kuwa huku anatuonea huruma na anatupenda mimi niseme mumsamehe tuu" - alisema Steve.
Aidha Steve Nyerere ameongeza kuwa kwa hali ilivyo katika tasnia ya filamu Tanzania hakuna haja ya maandamano pamoja na kurushiana maneno kwenye mitandao bali kinachotakiwa ni kukalishana chini waigizaji wote na kuangalia mahali walipojikwaa na kufanya marekebisho.
"Mtandaoni hatutaweza kumaliza hili tatizo kinachotakiwa hapa ni tukae chini na tuongee tunataka nini. Msibague kuandamana kwa ajili ya faida yenu wenyewe ila tujenge hoja ambayo tukubaliane wote tuiombe serikali itusaidie wote kwa ujumla na siyo watu wachache wanaojifanya manabii hawataki kukosolewa" Steve Nyerere alisistiza.

Comments

Popular posts from this blog