Posts

Steve Nyerere aporomosha jambo lingine leo

Image
Muigizaji na mchekeshaji maarufu nchini Steve  Nyerere amemuombea msamaha msanii wa muziki Nay wa Mitego kwa kuwaita wasanii wa filamu wote walioandamana kupinga uingizwaji wa filamu kutoka nje ya nchi kuwa ni 'Matahira' Akizungumza leo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Steve Nyerere amesema kwamba yawezekana  Nay wa Mitego alikuwa na hasira hivyo akashindwa kutumia lugha sahihi ya kuwaelekeza wasanii wenzake walivyokuwa wanakosea ndio maana alitoa lugha yenye maneno makali ijapokuwa alikuwa sahihi kukosoa maandamano yale. "Kwanza naomba nimuombee msamaha ndugu yangu Nay wa Mitego, hakuwa na nia mbaya lakini hakutumia maadili kufikisha ujumbe wake, Unajua sisi watanzania hatupendi kuambiwa ukweli na hata tukisemana tuna lugha zetu laini za kusemeshana. Nay wa Mitego mpaka kutoa maneno makali vile ujue anaipenda tasnia yetu ya filamu alikuwa kaaumia, si unajua hata yeye alishawahi kuwa huku anatuonea huruma na anatupenda mimi niseme

Kambi ya Upinzani Walivyogoma Kusoma Hotuba Yao Bungeni

Image
Msemaji wa upinzani katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, Ally Salehe amesusa kusoma hotuba yake ya upinzani kuhusu wizara hiyo baada ya kuamriwa kuacha kusoma baadhi ya maneno yakiwamo yanayohusu Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar na mgogoro wa CUF. Hali  hiyo imetokea bungeni leo Jumatatu baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju kusimama na kupinga baadhi ya maneneo aliyotumia kama  “Kila wizara imekiona cha moto, wamebanwa mpaka wamevunjwa mbavu” na kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imeathirika vibaya na kisu cha ngariba kwa kukata bajeti yake. Baada ya malumbano, Mwenyekiti wa Bunge, Musa Zungu alitoa uamuzi kuwa maneno yaliyoandikwa kuanzia ukurasa wa tatu hadi wa saba kwenye hotuba hiyo yasisomwe wala kurekodiwa kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge. Baada ya uamuzi huo, Salehe alisema basi asingeendelea kuisoma hotuba yake na yaliyobaki anamwachia ‘ngariba’ afanye anavyotaka.

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI MKOANI DODOMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Abdallah Bulembo mara baada ya kuwasili mkoani Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya k

Rais Magufuli amefanya uteuzi huu leo April 24

Image
Rais Dkt @MagufuliJP amemteua Prof. Chibunda kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Mmarekani aliyekamatwa Korea Kaskazini atambuliwa

Image
Bw Kim amekuwa akifunza katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Pyongyang (PUST) Chuo kikuu kimoja nchini Korea Kaskazini kimesema raia wa Marekani aliyekamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa nchi hiyo Jumamosi alikuwa mhadhiri katika chuo hicho. Wamesema jina lake ni Kim Sang-duk, lakini pia amekuwa akifahamika kamaTony Kim. Mhadhiri huyo ambaye ni Mmarekani wa asili ya Korea amekuwa akifunza katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Pyongyang (PUST) kwa wiki kadha kabla ya kukamatwa kwake. Chuo kikuu hicho hata hivyo kimesema masuala yaliyopelekea kukamatwa kwa Bw Kim hayana uhusiano wowote na chuo hicho. Bw Kim alikamatwa alipokuwa anajiandaa kuondoka Pyongyang. Maafisa wa Korea Kaskazini bado hawajasema sababu iliyochangia kukamatwa kwake. Shirika la habari la Korea Kusini Yonhap limesema Bw Kim, ambaye umri wake ni miaka hamsini hivi, alikuwa anashiriki katika mipango ya kutoa misaada na alikuwa Korea Kaskazini kufanya mashauriano

NGORONGORO KITOVU CHA UTALII KINACHOWAVUTIA WATU MASHUHURI DUNIANI

Image
Na Jumia Travel Tanzania Inaonekana mwaka 2017 umeanza vizuri katika sekta ya utalii nchini Tanzania kutokana na watu kadhaa mashuhuri kuzuru vivutio vyake. Sehemu ambazo zimeonekana kuwavutia watu wengi zaidi ni hifadhi ya mbuga ya Serengeti na bonde la Ngorongoro. Alianza mwigizaji maarufu wa filamu kutokea Hollywood nchini Marekani, Will Smith na mkewe Jada Pinkett-Smith. Mwanzoni mwa mwezi Machi walitua nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kujivinjari katika mbuga ya Serengeti. Wakiwa huko familia ya Smith walikutana na msanii mwingine kutokea huko huko Marekani, lakini huyu yeye ni mwanamitindo na mrembo, Chanel Iman. Haikupita muda mrefu sana tangu watu hao mashuhuri kuwepo nchini, kwani siku chache zilizopita aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Taifa la Israel, Bw. Ehud Barak naye alitembelea mbuga ya Serengeti pamoja na Ngorongoro. Hii ni ishara nzuri kwa sekta ya utalii nchini ambapo kupitia watu hawa maarufu wen

MFANYABIASHARA Achomwa Visu 14 na Kaka’ke..!!!

Image
 Mfanyabiashara wa samaki, Warioba Mtatiro, mkazi wa Kijiji cha Etalo, Musoma Vijijini, amedaiwa kujeruhiwa vibaya kwa kisu na kaka yake (jina tunalihifadhi). Tukio hilo la kusikitisha limetokea hivi karibuni katika Mtaa wa Nyamulinda, Kijiji cha Etalo, Musoma Vijijini. Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mtiti huo, Mtatiro alikuwa akicheza kamari maarufu mkoani Mara kwa jina la Magaramka na kaka yake ndiye aliyekuwa akichezesha. Alisema baada ya ‘kupunwa’, Mtatiro hakuwa na kiasi hicho cha fedha kilichohitajika katika mchezo huo ndipo ugomvi ukaibuka hadi kufikia hatua ya kaka kumchoma visu mdogo wake. “Mtatiro alipunwa shilingi mia tano. Sasa kaka yake akawa anamdai na yeye akawa hana ndipo alipoamua kuchukua kisu na kuanza kumchoma. “Alimchoma sehemu mbalimbali mwilini, kichwani na mgongoni na kumsababishia majeraha makubwa. Kwani alikuwa anachoma kisha anachomoa na kuchoma sehemu nyingine kama mara 14,” kilisema chanzo hicho. Chanzo hicho kilieleza kuwa, baa

Studio Aliyotekewa Roma na Wenzake Yafungwa

Image
Roma Mkatoliki na mwanaye Ivan. DAR ES SALAAM: Zikiwa zimepita wiki kadhaa tangu staa wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ na wenzake watatu, Moni, Imma na Bin Laden walipotekwa wakiwa kwenye Studio ya Tongwe Records iliyopo Masaki, Dar na kupatikana baada ya siku tatu wakiwa na majeraha, habari mpya ni kwamba studio hiyo imefungwa na haifanyi kazi kwa sasa. Wikienda lilifika kwenye studio hiyo na kuzungumza na chanzo kilichokutwa jirani yake ambapo kilieleza kwamba, tangu alipotekwa Roma na wenzake wakiwa ndani ya studio hiyo huku kompyuta na TV vikichukuliwa na watekaji hao, studio hiyo haijawahi kufunguliwa na haijulikani itafunguliwa lini kwani bado hofu ni kubwa. “Hofu ni kubwa sana tangu utekaji ufanyike, imebidi studio ifungwe na haijulikani itakuwa wazi lini, ukizingatia waliotekwa bado wako nyumbani wanauguza majeraha waliyoyapata na hali zao bado siyo nzuri hasa Roma,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kupata habari hizo,

Ishu ya Bongo Muvi Kuandamana… Nay wa Mitego, Mlela Hapatoshi

Image
BAADA ya wiki iliyopita mastaa wa filamu kuandamana kupinga uuzaji holela wa filamu za nje ya nchi kwa sababu zinawaharibia soko, hali imekuwa tete kwa msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na muigizaji Yusuf Mlela kutokana na kutoleana maneno makali, Wikienda lina data kamili. Akizungumza na Wikienda, Nay alisema anawashangaa wasanii wa filamu kuandamana kisa filamu za nje wakati zilianza kuuzwa hata kabla wao hawajafikiria kuanza kuigiza hivyo wanatakiwa kufanya kazi nzuri zenye ubunifu na siyo vinginevyo. “Nawashangaa sana Bongo Muvi kuandamana, muvi za nje zipo tangu enzi na enzi hata kabla wao hawajaingia kwenye sanaa hiyo, wanatakiwa kufanya kazi maana wamekosa ubunifu pia waache upuuzi,” alisema Nay. Baada ya Nay kuzungumza hayo Mlela naye alimjibu kwa kumwambia kwamba anatakiwa kukaa kimya kwani wanachofanya wanatetea haki yao kwani Nay alikuwa chokoraa tu lakini sasa amefanikiwa ndiyo anaongea maneno yasiyofaa kwa ku

Jokate aivuruga UVCCM ni baada ya kuteuliwa

Image
UTEUZI wa Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006, Jokate Mwegelo kuwa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, unaonekana kutaka kuivuruga jumuiya hiyo. Mjadala mkubwa umeibuka kuhusu uteuzi huo, ambapo baadhi ya wanachama na viongozi wa juu wa jumuiya hiyo wamedai kuwa haukufuata kanuni na taratibu za umoja huo. Vyanzo vya kuaminika kutoka katika umoja huo vimeliambia MTANZANIA kuwa baadhi ya viongozi wa juu wa UVCCM hawakushirikishwa katika uteuzi huo uliofanywa na kigogo mmoja wa umoja huo. Taarifa za ndani zinaeleza kuwa uteuzi huo haukushirikisha wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wala Baraza Kuu la UVCCM, ambalo halikukutana kumthibitisha Jokate kama kanuni zinavyoelekeza. Kwa mujibu wa kanuni za jumuiya hiyo, wajumbe wa kamati ya utekelezaji hawazidi 10, ambapo miongoni mwao ni Mwenyekiti wa umoja huo Taifa, Makamu Mwenyekiti Taifa, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na mjumbe mmoja kutoka makao ma

NAPE NNAUYE ATOA NENO HILI KUHUSU VURUGU ZA CUF

Image
Kufuatia watu wanane kuibuka wakiwa na silaha na kusababisha vurugu kwenye mkutano wa viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), Wilaya ya kinondoni, Dar, Jumamosi iliyopita, Mbunge wa Mtama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Moses Nnauye ametia neno kwa kusema kuwa hizo ni siasa za kinung’ayembe. Vurugu za CUF juzi Jumamosi. Jana Nape aliandika kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Twitter:  “Siasa ni ushindani wa hoja na siyo nguvu! Tunakwenda wapi huku jamani? Wanavamia na kutoroka!!?? How!!? Siasa imevamiwa na manung’anyembe sasa! Tafsiri ya nung’ayembe ni mwanamke asiyeolewa anayehangaika ya maisha ya kurukaruka. Tukio la kufanyiwa fujo mkutano wa CUF lilijiri katika Hoteli ya Niva iliyopo Mabibo, Dar ambapo ilidaiwa kuwa, wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono Maalim Seif waliumizwa kwa kupigwa na wavamizi waliodaiwa ni wale wanamuunga mkono Profesa Lipumba. Katika vurugu hizo, pia wandishi wa habari ambao walijitete lakini walishambuliwa ni pamoja na F

Ngoma, Bossou kuikosa Prisons

Image
MSHAMBULIAJI Donald Ngoma na Vincent Bossou watakosekana katika kikosi cha Yanga kinachotarajiwa kuivaa Tanzania Prisons kutoka Mbeya katika mechi ya hatua ya ya robo ya fainali ya mashindano ya Kombe la FA itakayofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na wataingia uwanjani huku wakiwaheshimu wapinzani wao kutokana na uzoefu waliokuwa nao kwenye ligi na mashindano mbalimbali. Mwambusi alisema kuwa wamejiandaa na ushindani na changamoto kutoka kwa Prisons ambayo wachezaji wake wamekaa pamoja muda mrefu. 'Hatutawadharau Prisons, mpira hauna historia, tusubiri tuone dakika 90, ila tutamkosa Vincent ambaye ni mgonjwa aliumia jana (juzi) na leo (jana) amekwenda hospitali, Ngoma ndio hatokuwapo kabisa, aliumia tangu tulipokuwa safarii, tunasema mchezo wa kesho utakuwa mgumu zaidi, " alisema Mwambusi. Aliongeza kuw

Gabo Afunguka Kuonja Penzi la Wema Sepetu

Image
  Staa wa Bongo Movie, Salim Ahmed ‘Gambo’ na Madame Wema Sepetu KUFUATIA uwepo wa madai kuwa amelionja penzi la mwigizaji Wema Sepetu, mkali anayekimbiza kwa sasa katika soko la sinema kwa Bongo, Salim Ahmed ‘Gambo’ amebanwa na Risasi na kufungukia uhusiano wake na Wema Sepetu. Awali, mwanahabari wetu alihakikishiwa na msanii mmoja (jina tunalihifadhi) kuwa kabla ya kuvuja kwa picha za sinema za Wema na Gabo za filamu hivi karibuni, wawili hao waliwahi kuanguka dhambini miaka kadhaa iliyopita. “Kwani unafiri ukaribu wa Wema na Gabo ni filamu tu? Kuna zaidi ya filamu, walishawahi kutoka miaka ya nyuma na ndio maana umeona hivi karibuni imekuwa rahisi tu kwao kufanya tena kazi pamoja,” alisema msanii huyo. Baada ya kupata ubuyu huo, mwanahabari wetu alimtafuta Wema ili kuweza kumsikia anazungumziaje ishu hiyoi lakini bahati mbaya mrembo huyo hakuweza kupokea simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, pia hakujibu. Alipoulizwa Gabo kuhusiana na madai hayo, alisem

Watumishi 52,436 kuajiriwa

Image
SERIKALI inakusudia kuajiri watumishi wapya wa umma 52,436 katika mwaka ujao wa fedha. Aidha, madaktari wapya 258 waliokuwa waende kufanya kazi nchini Kenya, lakini wakakwama kutokana na kuwekewa pingamizi la kimahakama na wenzao wao huko na hivyo Rais, Dk John Magufuli kuamuru waajiriwe mara moja nchini, watarajiwa kuanza kazi keshokutwa Jumatatu. Hayo yalisemwa bungeni juzi usiku na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki alipokuwa anatoa ufafanuzi wa lini Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa kada nyingine, kama ilivyoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (CCM). “Azma ya serikali, kwanza kabisa hatuwezi kuajiri wananchi wote, tumekuwa tukisikia hapa wahitimu hawana ajira, wengine wanaendesha bodaboda… tunapopanga idadi ya watumishi wa kuajiriwa, tunaangalia mambo mengi, kuanzia mahitaji, vipaumbele hadi uwezo wa kibajeti. “Tayari tumeshaanza kutoa vibali vya ajira zaidi

Atembezwa Nusu UCHI Na Kisha Kulazimishwa Kula Kinyesi kwa Kosa la Kumtukana Mama Yake

Image
Wanawake wa kijiji cha Kisungamile kilichopo katika Kata ya Matai wilayani Kalambo katika mkoa wa Rukwa wamemwadhibu Vitus Nyami (26) kwa kumtembeza nusu uchi na kulazimisha kula kinyesi cha ng’ombe kwa kosa la kumtukana mama yake mzazi matusi ya nguoni. Aidha wanawake hao walitumia mfuko wa ‘salphate’ kufunika sehemu za siri za kijana huyo kisha wakaanza kumtembeza mitaani kijijini  humo huku wakiimba nyimbo za kabila la Kifipa wakilaani tabia ya kijana huyo ya kumtukana mama yake mzazi matusi ya nguoni kila kukicha . Walidai kukasirishwa na tabia ya kijana huyo wa kiume kumtukana mzazi wake wa kike matusi ya nguoni, hivyo walilazimika kumfunga kamba na kumtembeza mitaani kijijini humo akiwa nusu uchi. Mwenyekiti wa kijiji cha Kisungamile, Didas Musa alikiri kutokea kwa mkasa huo juzi ambapo mtuhumiwa huyo alitembezwa mitaani kwa saa sita kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana. Akifafanua alisema kuwa licha ya adhabu hiyo ya kutem

Ukiwa na tabia hizi 7, lazima mwanaume akukimbie

Image
1. CHOKOCHOKO Wanaume wengi huwa hawapendi chokochoko. Hawapendi mwanamke ambaye yeye kila wakati ni kuanzisha chokochoko ambazo zinazalisha ugomvi. Wanaume wengi hawapendi mabishano. Hawapendi ugomvi hivyo mwanamke anapokuwa hodari wa kuleta chokochoko, huepukwa. Ni vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa kuchimbachimba vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani. Kinywa chake kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi wake, yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye. Mara nyingi mwanaume akiona mke au mpenziwe ni mtu wa kupenda chokochoko, mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo wake kukaa naye mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane na marafiki baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe na muda wa kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala. 2. KUTORIDHIKA Wanaume wengi wanachukia kuwa na wanawake wasioridhika. Baadhi ya wanawake hata uwape nini huwa hawar

Faida za kula parachichi kiafya

Image
Tunda hili lina virutubisho vingi na muhimu kwa afya zetu, na inaelezwa kuwa tunda hili huenda likawa ni mbadala wa vyakula kama nyama nyeupe kwa jinsi lilivyo na malighafi zote zilizo muhimu ndani yake. Zifuatazo ndizo faida  za tunda hili; Tunda hili linapotengenezwa kama kinywaji (juis) husaidia kuondoa maumivu ya tumbo na kuponya vidonda vya tumbo pamoja na kurekebisha udhaifu mwingine tumboni. Parachichi huweza kumpatia mtu uwezo mzuri wa kuona, huku majani yake yakielezwa kuongeza damu na kusheheni vitamin A, B, C na E. Parachichi linauwezo wa kukuza nywele kwa haraka zaidi na kuifanya ngozi ya mwili kuwa katika unyororo. Unachotakiwa kufanya ni; Hakikisha ya kwamba unakata vijipande vidogo vidogo kisha paka katika nywele zako au ngozi yako, acha baada ya dk kumi na tani kisha na nawa uso wako kwa maji ya uvuguvugu. Tunda hili husaidia wanawake katika kuifanya hedhi iende vizuri kila mw

Watumishi 52,436 kuajiriwa

Image
SERIKALI inakusudia kuajiri watumishi wapya wa umma 52,436 katika mwaka ujao wa fedha. Aidha, madaktari wapya 258 waliokuwa waende kufanya kazi nchini Kenya, lakini wakakwama kutokana na kuwekewa pingamizi la kimahakama na wenzao wao huko na hivyo Rais, Dk John Magufuli kuamuru waajiriwe mara moja nchini, watarajiwa kuanza kazi keshokutwa Jumatatu. Hayo yalisemwa bungeni juzi usiku na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki alipokuwa anatoa ufafanuzi wa lini Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa kada nyingine, kama ilivyoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (CCM). “Azma ya serikali, kwanza kabisa hatuwezi kuajiri wananchi wote, tumekuwa tukisikia hapa wahitimu hawana ajira, wengine wanaendesha bodaboda… tunapopanga idadi ya watumishi wa kuajiriwa, tunaangalia mambo mengi, kuanzia mahitaji, vipaumbele hadi uwezo wa kibajeti. “Tayari tumeshaanza kutoa vibali vya ajira zaidi

Sakata la Lugumi bado halijachacha

Image
Dar es Salaam. Sakata la mkataba baina ya Kampuni ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi, halijafa; ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeliibua ikionyesha madoa lukuki. Sakata hilo lilikuwa kama limezikwa baada ya kamati iliyoundwa na Bunge kulichunguza na baadaye kukabidhi ripoti ofisi ya Spika ambayo ilisema ingeishauri Serikali cha kufanya. Juni 30 mwaka jana, Naibu Spika Tulia Ackson alilieleza Bunge kuwa ametumia kanuni ya 117(17) kuikabidhi Serikali matokeo ya uhakiki uliofanywa na kamati ndogo iliyoundwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC). Alisema matokeo ya ripoti hiyo yana maoni, ushauri, mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto zilizoainishwa na taarifa ya kamati ya PAC na hivyo kuzuia wabunge kujadili suala hilo. Lakini, ripoti ya CAG iliyotolewa wiki iliyopita imeibua upya sakata hilo, ambalo linahusu utekelezwaji mbovu wa mkataba wa uwekaji mashine za kielektroniki za kuchukua alama za