Faida za kula parachichi kiafya


Tunda hili lina virutubisho vingi na muhimu kwa afya zetu, na inaelezwa kuwa tunda hili huenda likawa ni mbadala wa vyakula kama nyama nyeupe kwa jinsi lilivyo na malighafi zote zilizo muhimu ndani yake.

Zifuatazo ndizo faida  za tunda hili;

Tunda hili linapotengenezwa kama kinywaji (juis) husaidia kuondoa maumivu ya tumbo na kuponya vidonda vya tumbo pamoja na kurekebisha udhaifu mwingine tumboni.

Parachichi huweza kumpatia mtu uwezo mzuri wa kuona, huku majani yake yakielezwa kuongeza damu na kusheheni vitamin A, B, C na E.

Parachichi linauwezo wa kukuza nywele kwa haraka zaidi na kuifanya ngozi ya mwili kuwa katika unyororo.

Unachotakiwa kufanya ni;
Hakikisha ya kwamba unakata vijipande vidogo vidogo kisha paka katika nywele zako au ngozi yako, acha baada ya dk kumi na tani kisha na nawa uso wako kwa maji ya uvuguvugu.

Tunda hili husaidia wanawake katika kuifanya hedhi iende vizuri kila mwezi.

Pia majani yake yanapochemshwa kama chai na mtu kunywa husaidia kuondoa matatizo mwilini, ikiwa ni pamoja na uchovu, udhaifu na kujisikia ovyo, kuumwa kichwa, koo (throat), tumbo, mapafu na uvimbe.

Hali kadhalika, unapotafuna majani yake husaidia kutibu vidonda vya mdomo (ufizi) na kuimarisha meno pamoja na kuondoa maumivu.

Hayo ni baadhi ya machache kati ya mengi yanayofanywa na ulaji wa parachichi na majani yake. Endelea kutembelea muungwana blog kila wakati.

Comments

Popular posts from this blog