Posts

WAZIRI NCHEMBA ASEMA HAYA KUHUSU MTU ALIYEMTISHIA BASTOLA NAPE

Image
Baada ya tukio la mtu ana anayedaiwa kuwa ni Askari kanzu kuonekana akimtishia Bastola Waziri za zamani wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo na Mbunge wa Mtama Nape Nnauye  February 23, 2017 wakati alipotaka kuongea na Waandishi wa habari muda mchache baada ya taarifa ya Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya Wizara aliyokuwa akiiongoza.  Leo March 24, 2017 Waziri wa Mambo ya Ndani, ya nchi Mwigulu Nchemba alitumia ukurasa wake wa Intagram na kusema..>>’ Mh.Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu ‘ ‘ Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiaskari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini ‘ – Mwigulu Nchemba ‘ Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoong

MBUNGE HUSSEIN BASHE AMWANDIKIA UJUMBEE HUU NAPE NNAUYE

Image
Leo March 23, 2017 kumefanyika mabadiliko katika Baraza la Mawaziri ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   Dkt. John Pombe Magufuli   amemteua aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria   Dkt. Harrison George Mwakyembe   kuongoza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo ilikuwa chini ya   Nape Nnauye . Baada ya mabadiliko hayo watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa wamekuwa wakilizungumzia hilo katika page zao za mitandao ya kijamii miongoni mwao ni Mbunge wa Nzega Mjini  Hussein Bashe   ambaye aliamua kuandika ujumbe kupitia account yake ya Twitter huku akimtaka Nape Nnauye kutovunjika moyo. Bashe ameandika>>> “Karibu back bench tutumikie Taifa letu, Majimbo yetu na Chama chetu usivunjike moyo. It’s just beginning of a New journey.”   Follow Hussein M Bashe   @HusseinBashe Karibu back bench tutumikie Taifa letu, Majimbo yetu na Chama chetu usivunjike moyo. It's just beginning of a New journey. @ Nnauye_Nape 10:25 AM - 23 Mar 2017

Maneno ya Waziri Nape mchana huu Kuhusu Ripoti ya Tukio la Makonda

Image
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo  Nape Nnauye jana March 20, 2017 alifanya ziara makao makuu ya Clouds Media Group baada kuwepo taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenda kwenye kituo hicho akiwa na askari wenye silaha na kuwataka watangazaji wa Kipindi cha SHILAWADU kurusha kipindi chake. Waziri Nape aliunda Tume ya uchunguzi ya watu watano wakiongozwa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo na kutoa saa 24 kwa tume hiyo kuzungumza na Makonda na watu wake kisha leo March 21 iwasilishwe. Baasa ya kuona anapigiwa simu nyingi za kuhoji hatua iliyofikiwa hadi sasa Waziri Nape ametoa majibu kupitia Account yake ya Twitter na kusema ’Kuna simu nyingi juu ya ripoti. Nawaomba tutulie Kamati wanamalizia kazi yao, ikikamilika tutataarifiwa muda na mahali nitakapokabidhiwa!‘

WAZIRI MAHIGA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI WATEULE NCHINI

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) leo tarehe 22 Machi, 2017 amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Mabalozi Wateule 7 wanaowakilisha nchi zao nchini kutoka Hungary, Belarus, Guinea, Botswana, Niger, Cyprus na Bangladesh. Pichani Balozi Mahiga akipokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Hungary nchini, Mhe. Laszlo Eduard Mathe mwenye makazi yake Nairobi, Kenya.  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akipokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Belarus nchini, Mhe. Dmitry Kuptel mwenye makazi yake Addis Ababa, Ethiopia.  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa na Balozi Mteule wa Guinea nchini Mhe. Sidibe Fatoumata KABA mwenye makazi yake Addis Ababa, Ethiopia mara baada ya kupokea Nakala zake za Hati

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO YA BALAZA LA MAWAZIRI

Image

MBUNGE ZITTO KABWE AMPONGEZA KAMANDA TUNDU LISSU BAADA YA USHINDI WAKE

Image
CHAMA cha ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe, kimempongeza Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, kwa kushinda kiti cha urais wa Chama cha Wanasheria (TLS) katika uchaguzi uliofanyika juzi jijini Arusha. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Msafiri Mtemelwa, alisema Lissu anastahili pongezi kwa kufanikiwa kushinda nafasi hiyo kutokana na changamoto zilizomkumba katika kuisaka. Alisema kuwa licha ya kupitia misukosuko mingi iliyokuwa inaonyesha njia ya kumkwamisha kufikia malengo yake, Lissu hakukata tamaa na alionyesha ujasiri. Mtemelwa alisema kupata nafasi hiyo kwa kiongozi kutoka upinzani ni dalili njema na kipimo kwa wapinzani na kwamba anapaswa kuitendea haki nafasi hiyo kwa ustawi wa vyama hivyo vya upinzani. “Mimi niseme tu kwamba, Lissu anastahili pongezi," Mtemelwa alisema. "Tunahitaji watu kama hawa, watu majasiri. Pamoja na kwamba ali

Nape aunda tume kuchunguza uvamizi wa Makonda Clouds

Image
Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ameunda kamati ya kuchunguza kuhusu tukio lililofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kutaka apewe matokeo ndani ya saa 24. Nape ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari  mara baada ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uaandaji wa Clouds Media Groups, Ruge Mutahaba kuthibitisha kuwa Makonda alivamia kituo hicho, Ujumaa usiku akiwa na polisi wenye silaha.  “Matukio kama haya hutokea pindi nchi inapotaka kupinduliwa, lakini kama Rais yupo na nchi haijapinduliwa  basi kuingia ndani ya chombo cha habari na silaha, huku ni sawa na kunajisi uhuru wa habari,” alisema Nape

RUGE MUTAHABA AFUNGUKA YOTE JUU YA RC MAKONDA KUVAMIA KITUO CHAO

Image
Stori iliyotrend jana siku nzima kuhusu Mkuu wa Mkoa Paul Makonda Kuvamia kituo cha Polisi na Bunduki usiku wa Ijumaa imedhibitishwa leo na Mkurugenzi wa Kituo hicho Ruge Mutahaba akiongea katika kipindi cha 360 Ruge Mutahaba amefunguka A to Z na Kuelelezea tukio lilivyotokea mpaka Mkuu huyo wa mkoa kuchukua recordings za dada ambaye alirekodiwa na Shilawadu lakini hawakuweza kurusha kwa vile stori haukubalance.... Ruge Amedai Makonda ni Rafiki yake lakini kwa hilo inabidi aombe radhi Watanzania Kwa vile Radio ya Clouds inasikilizwa na watu wengi Tanzania...

NEWS ALERT: Mkuu Wa Mkoa Anusurika Kufa Kwa Kugongwa Gari Akifanya Mazoezi Asubuhi Hii

Image
Watu wawili wamenusurika kifo baada ya kuwagonga wananchi waliokuwa katika mazoezi asubuhi ya leo Jumamosi Machi 18,2017 mjini Iringa huku mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza na katibu tawala Wamoja Ayubu wakinusurika katika ajali hiyo. Ajali hiyo imetokea nje ya lango la kamanda wa polisi mkoa wa Iringa dakika tatu tu baada ya kuanza mazoezi kuelekea uwanja wa Samora. Ajali hiyo imesababishwa na dereva taxi kuwaparamia wafanya mazoezi hao. Taarifa kamili inakuja hivi punde...

Mahabusi ajinyonga rumande

Image
Mtuhumiwa anayedaiwa kupatikana na meno ya tembo yenye thamani ya Sh500 milioni, Daudi Matola (41) mkazi wa Wilaya ya Namtumbo amekutwa amekufa akiwa mahabusu mjini hapa. Anadaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kutumia suruali aliyoifunga kwenye dirisha la choo cha mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Songea. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji amesema tukio hilo lilitokea Machi 9 saa 9:55 usiku. Mwombeji amesema inadaiwa siku ya tukio Matola akiwa mahabusu alienda chooni ambako alijinyonga kwa kutumia suruali yake.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN, MJINI DODOMA LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017. Picha na IKULU Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi jambo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017.

Waziri Ndalichako awaambia maofisa elimu kuhakikisha somo la Skauti linawekwa kwenye masomo ya ziada

Image
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amewataka maofisa elimu wa shule za msingi na sekondari nchini, kuhakikisha vyama vya skauti vinakuwa na masomo ya ziada katika shule hizo. Profesa Ndalichako aliyasema hayo hivi karibuni akiwa jijini Arusha kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, katika maadhimisho ya siku ya skauti Afrika ambayo kwa mwaka huu yalifanyika nchini. “Kama rais wa skauti na waziri mwenye dhamana ya elimu, naomba nitoe wito kwa maofisa elimu wote wa mikoa kuhakikisha suala la skauti shuleni linakuwa ni sehemu ya masomo ya ziada. Nasema hivyo kwa sababu mikoa mingine hapa washiriki ni wachache na nauliza kwanini tunawanyima vijana kushiriki kwenye mambo ambayo yana manufaa kwa Taifa,” alisema. “Tunataka wafanye nini, wakienda vijiweni hatuwaruhusu, hivyo tuwatengenezee mazingira na tutumie nguvu walizonazo katika mambo yatakayowajenga kuwa raia w

Zitto Kabwe ampongeza Kikwete kwa kuzindua taasisi yake ya maendeleo

Image
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete leo amezindua Taasisi ya Maendeleo ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF).Taasisi hiyo imeundwa ili kusaidia Tanzania na Afrika katika kuimarisha amani, afya, utawala bora na maendeleo endelevu. Taasisi hiyo inajikita katika maendeleo endelevu kwa kusaidiana na wadau wengine kukabiliana na umaskini, kusaidia mkulima mdogo, kulinda mazingira na kukabiliana na athari za tabia nchi. Baada ya uzinduzi huo Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amempongeza Rais huyo mstaafu kupitia akaunti yake ya Facebook: “Hongera Sana Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuzindua Mfuko Wa Wakf Wa Jakaya Kikwete Foundation. Natumai utaitumikia vema nchi yetu na bara la Afrika katika ustaafu wako. Jambo moja kubwa uwekeze kwalo ni kuandaa Viongozi Vijana. Naona timu imesheheni watu wenye uwezo mkubwa. Kila la kheri.

HUYU NDIYE ALIYEMFUNDISHA OSAMA BIN LADEN UGAIDI

Image
Anaandika.Emanuel john. Ni Ali Mohamed alikuwa double agent wa CIA na EIJ( Egyptian islamic jihad) ambayo ndio ilipelekea kuundwa kwa ALQAEDA huku yeye akiwa mwendesha mafunzo wa mbinu za kivita na kijasusi wa kwanza kwenye kambi zao kwa ajili ya kuwaandaa na mapambano dhidi ya utawala wa kisovieti nchini Afghanistan miaka ya 90. yeye ndiye mwalimu wa kwanza wa Osama bin Laden na Ayman Zawahiry( kiongozi wa sasa wa Alqaeda) Ali anaelezwa kuwa mtu mwenye uzito wa kilo 90, urefu futi 6 huku akielezwa mtu aliye fiti kimwili, aliyebobea kwenye sanaa za mapigano( martial art),mwenye ufahasa mzuri wa lugha za kiingereza,kifaransa,kiyunani na kiarabu. alikuwa mwenye nidhamu ya juu, mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri, mwenye kujichanganya na watu na uwezo wa kupata marafiki kwa urahisi. Uhusiano wake na CIA kwa mara ya kwanza aliingia marekani kama mkalimani wa Ayman Zawahiry( kiongozi wa sasa wa alqaeda) wakati alipoenda kuchangisha michango kusaidia wana mgambo katika harakat

Hatimaye RC Paul Makonda aanza kazi tena leo hii baada ya kurejea toka Afrika ya Kusini

Image
Picha ikimuonyesha RC Makonda akizindua ujenzi wa barabara ya zege leo jijini Dar. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezindua Barabara ya Shimo la Udongo, Kilwa EPZ iliyopo Kurasini ya Umbali wa Kilomita 1. – Barabara hiyo iliyojengwa kwa kiwango cha zege na kampuni ya wazalendo ya Grant Tech imegharimu takribani milioni 350.

Msukuma afunguka mazito, Ni kuhusu alivyokamtwa na Polisi

Image
JOSEPH Kasheku “Msukuma” Mbunge waa Jimbo Geita Vijijini na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Geita ametoa siku tano za kuombwa na radhi na wanaodaiwa kuwa ni maofisa usalama wa Taifa waliotoa taarifa za uongo dhidi yake na kusababisha akamatwe Mjini Dodoma, anaandika Charles William. Juzi Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, liliwatia nguvuni Msukuma, Hussein Bashe, Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini na Adam Malima, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mkuranga kwa madai ya kupanga kufanya vurugu katika Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika jana. Wanasiasa hao walikamatwa na kuhojiwa, kabla ya kuachiwa kwa dhamana. Hata hivyo Msukuma amesema hawezi kukaa kimya juu ya suala hilo na kwamba wapo maofisa usalama waliosambaza taarifa juu yake na kusababisha hofu lazima wamuombe radhi. “Hawa ni wapiga dili, Rais lazima aiangalie upya Idara ya Usalama wa Taifa. Wameniundia mimi zengwe, mpaka nikakamatwa, na nchi ikawa kwenye presha, kama chama kisipozungum

KINANA AFUNGUA SEMINA ELEKEZI YA MABADILIKO NDANI YA CHAMA KWA WENYEKITI NA MAKATIBU WA CCM MJINI DODOMA LEO

Image
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akifungua semina elekezi kuhusu mabadiliko ndani ya Chama, kwa Wenyeviti na Makatibu wa mikoa na wa wilaya na watendaji, leo katika Ukumbi wa Sekretarieti katika Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Washiriki wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Washiriki wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Washiriki wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Katibu wa Sekretarieti ya CCM, Anamringi Macha (kulia) akiratibu semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Washiriki wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani y