Mahabusi ajinyonga rumande

Mtuhumiwa anayedaiwa kupatikana na meno ya tembo yenye thamani ya Sh500 milioni, Daudi Matola (41) mkazi wa Wilaya ya Namtumbo amekutwa amekufa akiwa mahabusu mjini hapa.

Anadaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kutumia suruali aliyoifunga kwenye dirisha la choo cha mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Songea.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji amesema tukio hilo lilitokea Machi 9 saa 9:55 usiku.

Mwombeji amesema inadaiwa siku ya tukio Matola akiwa mahabusu alienda chooni ambako alijinyonga kwa kutumia suruali yake.

Comments

Popular posts from this blog

PICHA ZA UTUPU ZILIZOPIGWA NA MWANAFUNZI WA UDOM ILI KUTANGAZA SOKO LA MWILI WAKE. TAZAMA HAPA

ZITTO KABWE AWAPONDA LOWASSA NA MAGUFULI